Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Unataka Kupandishwa CHEO Na Kuongezwa MSHAHARA Haraka?…
Aina 6 Za Mabosi Wakorofi na Jinsi Ya Kukabiliana Nao.
i. Wanafuatilia Kila Kitu
ii. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu
iii. Wanakuchukia Bila Kujua Sababu
iv. Wanaogopa Uwezo Wako
v. Wanaokupelekesha
vi. Wanaoamini Katika Mawazo Yao Tu!
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina Ya 3 Ya Mabosi
– Wanakuchukia Bila Kujua Sababu
Umeshawahi kuwa katika ofisi na unakuta bosi anakuchukia.
Na ukitafuta sababu unakuwa hauioni?
Kuna watu wako kwenye ofisi na wanajaribu kufanya kila kitu wanachoona kitawafanya wakubaliwe.
Lakini wanajikuta bado wanachukiwa na bosi wao.
Mara nyingi bosi wa namna hii huwa anakuchukia kwa sababu ambazo…
…mara nyingi ziko nje ya ofisi/hazihusiani na kazi kabisa.
Kuna watu wanakuchukia kwa sababu…
…jina lako limefanana na mtu ambaye waligombana naye huko nyuma.
Kuna wengine wanakuchukia kwa sababu ya umbo lako tu lilivyo.
Kuna wengine watakuchukia kwa sababu unavaa vizuri.
Ama kwa sababu unajivunia sana mwenzi wako au unaendesha gari zuri.
Usisahau kuna mabosi ambao wanaweza pia kuwa katika kundi hili…
…na wanakuchukia kwa sababu wanaamini umekuja kuwachunguza…
…na unapeka habari zao mahali fulani.
Ama kuna wengine wanaogopa kuwa utachukua nafasi yao.
Na hivyo wanaona njia nzuri ya kufanya ni kupambana na wewe mapema kabisa.
Mara nyingi bosi wa namna hii huwa anasumbuliwa na “Cognitive Dissonance”.
Kwa mujibu wa mwanasaikolojia maarufu Leon Festinger…
Kwenye kitabu chake cha “A Theory of cognitive Dissonance” (1957)…
Anaeleza kuwa hali hii huwa inatokea pale…
…kunapokosekana uwiano kati ya mtu anachokiamini na tabia yake ya wakati ule (Belief vs Behavior).
Mara nyingi bosi wa namna hii huwa anakuwa kuna vitu anaviamini kuhusu mambo fulani.
Lakini tabia zake zinapingana na kile anachokiamini.
Matokeo yake zile hasira na mahangaiko ya moyo (frustrations) anazihamishia kwa watu wengine.
Njia nzuri ya kukabiliana na bosi wa namna hii ni…
Kutengeneza uhusiano unaotokana na vitu ambavyo yeye anavipenda (Areas of interest/Common ground).
Mara nyingi mabosi hawa wakati pekee ambao wanakuwa na furaha na amani ni…
…pale ambapo wako kwenye wakati wa kufurahia vitu wanavyovipenda.
Kwa mfano, kama ni washabiki wa mpira wa miguu…
…timu yao inaposhinda inamuondoa kabisa kabisa ile hali ya kawaida na anakuwa na furaha.
Kumbuka kuwa bosi wa namna hii huwa anakuwa na “Moods swing” nyingi sana…
…(Hisia zake zinapanda na kushuka mara kwa mara).
Ni lazima ujifunze kumvizia wakati ambapo hisia zake ziko vizuri ndio uweke ajenda zako muhimu.
Ukikosea “timings” utakwaruzana naye kila siku.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.