Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Ethiopia, Tume ya kutetea haki za binadamu inasema inachunguza mauaji ya watu 48, wanaodaiwa kuuawa katika jimbo la Oromia na watu wenye silaha.

Waasi wa Oromo Liberation Army (OLA), ambao wanaorodheshwa na serikali ya Ethiopia kama magaidi, wanatuhumiwa kutekeleza mauaji hayo wiki iliyopita katika Wilaya ya Shewa.
Afisa wa Wilaya hiyo, ni miongoni mwa watu hao waliouawa baada ya kushambuliwa katika eneo hilo ambalo wakaazi bado wanaishi kwa mashaka, baada ya watu wengine kutekwa.
Tangu mwaka 2018, waasi hao wamekuwa wakidaiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya wananchi na maafisa wa usalama, madai ambayo kundi hilo limeendelea kukanusha.
Waasi wa OLA, wanakadiriwa kuwa maelfu ya wapiganaji ambao wameendelea kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, lakini wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema kundi hilo halijipanga vizuri kuwa tishio kwa serikali jijini Addis Ababa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.