Afrika: CDC inahitaji hakikisho kutoka kwa Trump kuhusiana na chanjo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kituo cha udhibiti wa magonjwa barani Afrika, CDC, kimesema kinatafuta hakikisho toka kwa utawala wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump, kuhusu ikiwa utatimiza ahadi yake ya ufadhili na chanjo ya mpox iliyoahidiwa na mtangulizi wake.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden akisalimiana na mshauri wake mkuu Susie Wiles.
Rais mteule wa Marekani Joe Biden akisalimiana na mshauri wake mkuu Susie Wiles. REUTERS – Carlos Barria

Mwezi Septemba, Rais Joe Biden aliahidi kutoa dola milioni 500 na dozi milioni 1 za chanjo katika mpango wa kukabiliana na mlipuko wa mpox barani Afrika.

Aidha wakati huu wagonjwa wa mpox wakiongezeka na maambukizo kuanza kupungua barani Afrika, wafadhili nao wamepunguza kasi ya kutumiza ahadi za kifedha na chanjo, amesema mkurugenzi wa CDC.

Chanjo za mpox zikiwasili nchini DRC kusaidia katika vita dhidi ya msambao wa mpox
Chanjo za mpox zikiwasili nchini DRC kusaidia katika vita dhidi ya msambao wa mpox © AFP

Alipoulizwa kama ushindi wa Trump unaweza kuathiri uungaji mkono wa Marekani katika kuchangia huduma za afya barani Afrika, Mkurugenzi wa CDC John Kaseya alisema ataufuatilia utawala mpya kutimiza ahadi zilizopo.

Hivi majuzi Trump alisema atamruhusu mwanaharakati anayepinga masuala ya chanjo Robert F. Kennedy Jr. kufanya maamuzi kuhusu sera ya afya ya Marekani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment