Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

ACHA WAONDOKE. Najua unahuzunika kwa sababu watu uliowaamini na kuwapa nafasi katika maisha yako wamekuacha.
Pengine wameondoka katika kipindi ambacho unahitaji msaada wao katika kitu au jambo fulani.
“Kwanini watu wanakuja na kuondoka kwenye maisha yangu”.
Hili ni swali niliwahi kuulizwa na mtu mmoja, na yamkini na wewe umeshawahi kujiuliza hicho kitu.
Hiki kitu kinawatesa watu wengi sana. Nakumbuka mwaka jana mtu mmoja aliniuliza pia.
“Kaka mimi sina marafaki wa kudumu katika maisha yangu nifanyaje? “.
Hata mimi binafsi kuna kipindi nilitamani kumshikilia kila mtu ninayejuana naye, baadaye nikagundua kuwa:
HAUWEZI kuwazuia hata siku mmoja watu wasiondoke kwenye maisha yako, NEVER.
LAKINI, Daima unaweza kuwavutia watu sahihi katika maisha yako.
“You can’t stop peole from leaving you, but you can always attract right people in your life”.
Baada ya kujua hilo nilichofanya ni kwamba nilijikita zaidi katika kutengeneza sumaku ya kunasa watu muhimu katika maisha yangu na siyo kutengeneza uzio wa kwa baadhi ya watu wasiondoke.
Kuwavutia watu ni kitu kimoja lakini, kuwafanya watu wawe sehemu ya mtandao na maisha yako ni kitu kingine.
Kuna vitu vingi vinavyowavuta kwenye maisha yako, lakini yafuatayo ni machache.
1. HAIBA na TABIA zako (Personality): Ndege wanaofanana huruka kwa pamoja.
2. THAMANI YAKO KWAO: Kipepeo au nyuki hatui kwenye miiba, hufuata maua mazuri.
3. NAMNA UNAVYOWA-TREAT: Kama wewe unapenda tu kujaliwa, kusaidiwa au kuwanyonya wengine, AND you offer NOTHING in return. My friend expect RED CARDS NYINGI.
NOTE: Usiogope kuwapoteza watu katika maisha yako, lakini ogopa kuwa na utitiri wa watu kwenye maisha yako ambao hawana msaada wowote kwako.
Wataalamu wa mafanikio wanashauri, “Kuwa na Circle yako Ndogo yenye thamani katika kitu unachokifanya”.
Pia, usiteseke sana, tengeneza LEVELS za watu mbalimbali katika maisha yako kama vile medani katika michezo.
Wape Bronze Level, Silver na Golden. Kuwa makini usije ukawapa watu ambao hawafai, “GOLDEN LEVEL” wakakuvuruga na kukuacha njiani.

CHANGAMOTO unazopitia HUCHUJA watu watakonywea kikombe kimoja chai na wewe na wale ambao Machicha.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.