Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kila mtu kwenye haya maisha kuna mambo ambayo anatamani yasingetokea.
Kuna mambo ambayo kila mtu anatamani angeyafuta kwenye kumbukumbu za maisha yake.
Hata yule unayemuona hodari, amefanikiwa na “unamuadmire”…
Anayo stori ambayo kuna wakati ilimkosesha ujasiri.
Na ilimfanya ajione hafai.
Hili ndio jambo muhimu la kukumbuka kwenye maisha yako.
Makosa ni sehemu ya kujifunza.
Yaani, kukosea kwenye maisha ni sehemu ya ubinadamu wetu.
Cha muhimu hapa, ni kujifunza kwa haraka pale unapokosea.
Na pia kuhakikisha unapunguza makosa kama hayo mbele ya safari.
Usiruhusu kosa moja lifute kujiamini kwako.
Usiruhusu kosa ulilofanya liue ndoto yako.
Mungu akusaidie ili ujisamehe na usonge mbele.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.