Marekani: Salamu za pongezi zaendelea kutolewa kwa Donald Trump

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Viongozi wa dunia wameendelea kumpongeza rais mteule wa Marekani, Donald Trump baada ya ushindi alioupata dhidi ya Kamala Harris, viongozi wengi wa Ulaya wakiwa wa kwanza kufanya hivyo.

Bango lenye picha ya rais mteule wa Marekani Donald Trump likiwa na ujumbe wa kumpongeza ukisema ifanye Israeli kuwa kubwa tena mjini Tel Aviv, Israel, Jumatano Novemba 2024.
Bango lenye picha ya rais mteule wa Marekani Donald Trump likiwa na ujumbe wa kumpongeza ukisema ifanye Israeli kuwa kubwa tena mjini Tel Aviv, Israel, Jumatano Novemba 2024. AP – Oded Balilty

Rais wa Ufaransa ni miongoni mwa viongozi wa kwanza, waliompongeza Trump kwa ushindi alioupata, kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao yake ya kijamii.

Macron amemwambia Trump kuwa yuko tayari kuendelea kufanya kazi naye kwa kuheshimiana kama ilivyokuwa miaka minne aliyowahi kuwa madarakani.

Emmanuel Macron na Donald Trump, Tarehe  3 Desemba 2019.
Emmanuel Macron na Donald Trump, Tarehe 3 Desemba 2019. © Nicholas Kamm / AFP

Mkuu wa Tume ya Umoja wa UlayaUrsula von der Leyen hakuachwa nyuma kumpongeza Trump kupitia ukurasa wake wa X, akimwambia kuwa EU na Marekani zitaendelea kushrikiana na kuwaunganisha watu.

China kupitia Wizara ya Mambo ya nje, imesema Beijing, inatumai kuwa kutakuwa na ushirikiano wa amani na Washington DC na kila upande, utanufaika.

Donald Trump na Ursula von der Leyen walipokutana mjini Davos mwaka wa 2020.
Donald Trump na Ursula von der Leyen walipokutana mjini Davos mwaka wa 2020. AFP

Naye Waziri Mkuu wa IsraeliBenjamin Netanyahu amesema, ushindi wa Trump ni mwanzo mpya kati ya nchi yake na Marekani na kuelezea ushindi wake kama wa kihistoria.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amemwambia Trump kuwa anatumai uongozi wake utasaidia kurejesha amani Mashariki ya Kati na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yataimarika, huku rais wa mamlaka ya Palestina, Mahamud Abbas akisema anatumai Trump atasaidia kupatikana kwa taifa la Kipalestina.

Benjamin Netanyahu na  Donald Trump, mwezi Septemba mwaka wa 2020 jijini Washington.
Benjamin Netanyahu na Donald Trump, mwezi Septemba mwaka wa 2020 jijini Washington. AP – Alex Brandon

Viongozi wa mataifa ya Afrika, wakiongozwa na rais wa Nigeria Bola TinubuEmmerson MnangagwaEvariste Ndayishimiye na Felix Tshisekedi ni miongoni mwa marais waliompongeza Trump kwa ushindi.

Rais wa #China #XiJinping amempongeza rais mteule wa Marekani #DonaldTrump na kutoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa kudumu kati ya mataifa hayo mawili.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment