Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Dozi zaidi ya laki 8 za awali za chanjo zimetengwa kwa ajili ya nchi 9 barani Afrika ambazo zimeathiriwa pakubwa na ongezeko la wagonjwa wa mpox, WHO na mashirika mengine ya afya yamesema.
Mwezi Septemba, baada ya kukabiliwa na ukosoaji kutokana na kasi ndogo ya ugavi wa chanjo hizo, WHO iliidhinisha chanjo ya majaribio ya kampuni ya Bavarian Nordic’s na kuahidi kuifanyia tathmini chanjo nyingine inayotengenezwa na kampuni ya dawa ya Japan, KM Biologic.
Aidha WHO ilianzisha mpango wa kusaidia kuleta chanjo ya mpox, vipimo na matibabu kwa watu walio hatarini zaidi katika nchi masikini duniani, juhudi sawa na zilizofanyika wakati wa janga la COVID-19.

Katika taarifa yake, shirika la afya duniani limesema, chanjo hizi mpya zitatolewa kwa nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Liberia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini na Uganda, huku zaidi ya asilimia 85 ya chanjo hizo zitatolewa kwa DRC iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Mpox.
Kulingana na takwimu za hivi karibuni, bara Afrika limerekodi wagonjwa wanaofikia elfu 46, huku vifo vikivuka watu elfu moja.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.