Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Rais wa Ghana walalamika baada ya rais kuzindua sanamu yake mwenyewe
- Raia wa Ghana walalamika baada ya rais kuzindua sanamu yake mwenyewe
- Hawa ndio washirika wa karibu wa Trump kote duniani
- Je, nani anaweza kuwa katika baraza la mawaziri la Trump?
- Mataifa sita kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya chess nchini Tanzania
- Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Waendesha mashtaka waanza kutupilia mbali mashtaka ya Trump
- Droni za Shahid zaupiga mji mkuu wa Ukraine usiku kuchaKyiv wakati wa
- Australia kupiga marufuku watoto kuingia mitandao ya kijamii
- Je, mchakato wa kipindi cha mpito wa kukabidhiana madaraka ukoje?
- Trump ameshinda – lakini hatakuwa katika Ikulu ya White House kwa siku 74
Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni jina langu ni Cantona Joseph
Gachagua ainua mikono, aondoa kesi aliyolenga kuzima kutimuliwa ofisini

Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua. Picha|Maktaba
MAHAKAMA ya Rufaa imemruhusu aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua kuondoa kesi ya kutaka kusitisha kutimuliwa kwake katika Mahakama Kuu.
Kupitia kwa wakili Paul Muite, Bw Gachagua aliwaambia Majaji Patrick Kiage, Aggrey Muchelule na George Odunga kwamba suala hilo limepitwa na wakati kwa vile maagizo ya muda aliyotaka kuzuia kuapishwa kwa Prof Kithure Kindiki kuwa naibu wa rais, yaliondolewa.
Prof Kindiki aliapishwa kuwa Naibu Rais wa tatu mnamo Novemba 1, 2024 siku moja baada ya Mahakama Kuu kuondoa agizo la kumzuia kushikilia wadhifa huo.
Bw Muite alifahamisha mahakama kwamba tayari amewasilisha rufaa, akipinga mamlaka ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, kuteua jopo la majaji.
Mahakama Kuu iliamua kwamba mamlaka yaliyotekelezwa na Jaji Mkuu chini ya Kifungu cha 165(4) cha katiba- kuhusu uteuzi wa jopo ili kuamua masuala mazito ya kikatiba, ni ya kiutawala na Naibu Jaji Mkuu anaweza kuteua majaji kwa niaba ya Jaji Mkuu.
‘Suala hili linastahili uamuzi wake kikamilifu na tunaomba kesi iondolewe lakini mahakama itoe maagizo kuhusu rufaa hiyo,’ Bw Muite alisema.
Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor kupitia kwa wakili Prof Githu Muigai hakupinga kuondolewa kwa kesi hiyo.
Bw Gachagua aliondolewa ofisini Oktoba 17 na Rais Ruto akamteua Rais Kindiki siku iliyofuata na uteuzi wake ukaidhinishwa na Bunge la Kitaifa.
Naibu Rais aliyetimuliwa na walalamishi wengine walikimbia mahakamani na kupata agizo la kuzuia kujazwa kwa nafasi yake kusubiri uamuzi wa kesi hizo.
Wakiondoa agizo hilo Alhamisi iliyopita, majaji hao watatu walisema mfumo wa kikatiba haukunuia hali ambayo afisi ya Naibu Rais ingesalia wazi isipokuwa kipindi kifupi kinachohitajika kuijaza ikibaki wazi.
“Kwa hivyo, maslahi ya umma yanahitaji kwamba afisi ya naibu wa rais isibaki wazi,” walisema majaji.
Bw Gachagua alipinga kuondolewa kwake akishikilia kuwa mashtaka ya kuondolewa kwake hayakuthibitishwa au kuungwa mkono na ushahidi.
Alisema Bunge ilienda kinyume na katiba na kumnyima haki ya kusikilizwa kwa haki chini ya Ibara ya 25(c) na ya 50 ya katiba ilikiukwa na Seneti ilipoamua kuendelea na hoja ya kumuondoa madarakani bila kumpa fursa ya kusikilizwa. .
Naibu huyo wa rais wa zamani aliteta kuwa shughuli hiyo ilifanywa haraka kwa nia ya pekee ya kuepuka kuchunguzwa na mahakama. Bw Gachagua na washirika wake walikuwa wamewasilisha kesi 32 katika Mahakama tofauti nchini lakini hawakufaulu kusimamisha mchakato wa kumtimua katika Bunge la Kitaifa na katika seneti.
Mateso, kilio, wafanyakazi wa kaunti wakicheleweshewa mishahara kwa hadi miezi minne

Gavana wa Bungoma Ken Lusaka, ni moja ya kaunti ambazo hazijalipa wafanyakazi kwa muda kutokana na uhaba wa fedha. Picha|Maktaba
WAFANYAKAZI wa serikali za kaunti kote nchini wanakabiliwa na wakati mgumu kufuatia kucheleweshwa kwa mishahara kwa miezi kadhaa.
Chanzo kikuu cha masaibu yao ni uhaba wa pesa uliosababishwa na kucheleweshwa kwa mgao wa kila mwezi kwa kaunti kutoka Hazina ya Kitaifa.
Kufadhaika sasa kunaongezeka huku wafanyikazi hao wakihisi kupuuzwa—hasa baada ya wafanyikazi wa serikali ya kitaifa kupokea nyongeza ya mishahara huku wafanyikazi wa kaunti wakikosa kuzingatiwa.
Baadhi ya kaunti kama Kakamega na Kisumu zinalazimika kukopa pesa kutoka kwa taasisi za kifedha ili kulipa mishahara.
Katika Kaunti ya Bungoma, hali ni mbaya, huku wafanyikazi wakipokea mishahara wao mara ya mwisho Julai pekee. Ucheleweshaji huo umezua shida kubwa ya kifedha kwa wafanyikazi.
“Mimi ni afisa aliyevunjika moyo sana jioni hii. Nimetembelea hospitali tatu tofauti kutafuta matibabu, lakini bila mafanikio. Mbaya zaidi, sina pesa za kulipia matibabu yangu kwa sababu ya kutolipwa mshahara wangu, na hakuna habari kuhusu ni lini, au ikiwa, tutalipwa. Ni Mungu pekee anayeweza kuingilia kati ili kutuokoa kutokana na hali hii isiyovumilika—hakuna chakula, hakuna nauli, hakuna matibabu, hakuna mshahara,” akasema afisa mmoja kutoka kaunti ya Bungoma.
Kaunti za Kusini mwa Bonde la Ufa, zikiwemo Nakuru, Laikipia, Narok, Nyandarua, na Kericho, zimegeukia mikopo ya benki ili kulipa mishahara baada ya kukosa pesa kutokana na kucheleweshwa kwa mapato.
Huko Laikipia, watumishi wa umma bado hawajapokea mishahara yao ya Septemba. Daktari kutoka Hospitali ya Nyahururu alisema kuwa, “baadhi yetu hatujalipwa kwa miezi 3 hadi 6. Wazazi wanakidhi vipi mahitaji ya watoto bila mshahara?”
Mjini Nakuru, barua iliyoandikwa Oktoba 28 kutoka kwa Katibu wa Kaunti Dkt Samwel Mwaura ilithibitisha kucheleweshwa kwa mishahara, ikitaja masuala ya kuunganisha Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii katika mfumo wa malipo.
“Tuliambiwa ucheleweshaji huo ulitokana na masuala ya makato ya SHA. Tunasubiri tu,” alisema.
Katika eneo la Pwani, Mombasa ndiyo kaunti pekee ambayo imetimiza wajibu wake wa kulipa mshahara kwa wakati. Kaunti zingine, kama vile Tana River, wafanyikazi wanasubiri mishahara, na zaidi ya wafanyikazi 2,000 bado hawajalipwa.
Huko Taita Taveta na Lamu, wahudumu wa afya na wafanyikazi wengine wa kaunti pia hawajapata mishahara kutokana na utekelezaji wa makato ya SHIF.
“Bado hatujapokea mishahara yetu ya Oktoba na kila tunapouliza, tunaambiwa tuwe wavumilivu wakati wanaendelea na utekelezaji wa makato ya SHIF,” alisema daktari ambaye aliomba tubane jina lake kwa vile hana mamlaka ya kuzungumza na waandishi wa habari.
KPLC yapiga mnada jengo la Kanu kujilipa bili ya stima ya Sh212 milioni

Baadhi ya maafisa wa chama cha Kanu. Picha|Maktaba
BAADA ya kesi iliyochukua zaidi ya miongo miwili, jumba la Kanu House lililoko katikati mwa jiji la Nakuru limepigwa mnada baada ya wamiliki wake kushidwa kulipa bili ya stima ya zaidi ya Sh221 milioni ambayo usimamizi wake unadaiwa na kampuni ya umeme, KPLC.
Kulingana na Madalali wa Solai Auctioneers, walioteuliwa na KPLC kupiga mnada mali hiyo, kufikia Jumatatu, walikuwa wamepata mnunuzi ambaye alikuwa tayari kulinunua jengo hilo, linalomilikiwa na chama cha KANU, kwa Sh70 milioni.
“Tulipata anayetaka kulinunua jengo hilo la orofa mbili kwa Sh70 milioni, kufikia Jumatatu jioni mnada ulipofungwa. Pesa hizo ni za kununua jengo na ardhi ambako limejengwa,” akasema Bw Daniel Muturi wa Solai Actioneer aliyeendesha mnada huo.
Hata hivyo, thamani kamili ya mali hiyo iliyo na vyumba vingi vya kibiashara ni karibu Sh150 milioni.
Kampuni ya KPLC iliwasilisha kesi mahakamani mnamo 2004 dhidi ya chama cha Kanu.
Maafisa wa Kanu ambao majina yao yaliorodheshwa kwenye stabadhi ya mahakama ni Julius Sunkuli (aliyekuwa naibu katibu mkuu), Yusuf Haji (aliyekuwa mweka hazina), Bonaya Godana (Katibu Mpanga Ratiba).
KPLC ilidai kuwa Kanu ilifeli kulipa bili ya umeme kwa kipindi cha miaka minane.
Kampuni hiyo ya kusambaza umeme nchini ilitaka Kanu iamriwe ilipe Sh212,816,986 pamoja na riba, kuanzia tarehe ya kuwasilishwa kwa kesi hiyo.
Uamuzi wa kwanza kuhusu kesi hiyo ulitolewa mnamo Agosti 7, 2009 na Jaji J.B. Havelock.
Jaji huyo aliipata Kanu na kosa na kuiamuru ilipe malimbikizi yote ya bili ya stima iliyokuwa ikidaiwa na KPLC.
“Tunatumai kuwa Marekani itaimarika zaidi,” asema rais wa Ukraine

Rais wa Ukraine amesema uhusiano kati ya Marekani na bara la Ulaya “lazima uthaminiwe na hauwezi kupotea” baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa kilele wa viongozi wa Ulaya mjini Budapest , Volodymyr Zelensky amesema: “Tunatumai kuwa Marekani itaimarika zaidi.”
“Hii ndiyo aina ya Amerika ambayo Ulaya inahitaji,” amesema. “Na Ulaya yenye nguvu ndiyo ambayo Amerika inahitaji – huu ni uhusiano kati ya washirika ambao lazima uthaminiwe na hauwezi kupotea.”
Kulingana na shirika la habari la AFP, Zelensky pia ameuambia mkutano huo kuwa “haitakubalika kwa Ukraine” ikiwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin atapewa makubaliano yoyote.
Raia wa Ghana walalamika baada ya rais kuzindua sanamu yake mwenyewe

Rais wa Ghana anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo anakabiliwa na mzozo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzindua sanamu yake alipokuwa katika ziara ya Ukanda wa Magharibi mwa nchi hiyo.
Sanamu hiyo imesimikwa kwa heshima ya mipango ya maendeleo ambayo Rais amesimamia akiwa madarakani, Waziri Kwabena Okyere Darko-Mensah alisema.
Lakini Waghana wengi wamekuwa wakidhihaki usimikwaji wake nje ya hospitali katika jiji la Sekondi – wanaiona kama njia ya “kujitukuza”.
“Watu wa Ukanda wa Magharibi wanastahili jambo bora zaidi ya maonyesho ya kujionyesha ,” Mbunge wa upinzani Emmanuel Armah Kofi-Buah alichapisha kwenye X.
Akufo-Addo, ambaye atang’atuka madarakani Januari baada ya mihula miwili madarakani, amejigamba kuwa ametimiza asilimia 80 ya ahadi zake kwa Waghana.
Alizindua sanamu hiyo iliowekwa mbele ya hospitali ya Effia-Nkwanta ya jimbo la Sekondi , Jumatano wakati wa ziara yake ambayo imepewa jina la “safari ya shukrani”.
Katika hafla hiyo, Darko-Mensah, ambaye anasimamia Kanda ya Magharibi, aliangazia miradi kadhaa muhimu iliyoanzishwa chini ya rais.
Lakini sanamu hiyo imezua wimbi la ukosoaji, huku baadhi ya Waghana wakihoji umuhimu wake wakati miradi kadhaa muhimu haijakamilika.
Harris akubali kushindwa, ampongeza Trump

Rais mteule wa Amerika Donald Trump akisalimiana na mshindani wake katika uchaguzi uliokamilika, Kamala Harris, awali. Picha|Maktaba
WASHINGTON DC, AMERIKA
MAKAMU wa nchini Amerika ambaye alikuwa mgombea urais wa chama cha Democratic Kamala Harris amekubali kushindwa na Donald Trump na amewataka wafuasi wake kuendelea kutetea maono ya maendeleo ya nchi hiyo.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake katika Chuo Kikuu cha Howard mjini Washington Jumatano jioni, baada ya Trump kupata zaidi ya kura 270 za majimbo zinazohitajika kushinda kwenye uchaguzi wa urais, Harris aliwahimiza wafuasi wake kutokata tamaa.
Trump alirejea kisiasa kwa namna ya kushangaza, miaka minne baada ya kukataa kukubali kushindwa, jambo lililosababisha machafuko na vurugu katika makao ya serikali ya Amerika.
“Nakubali kushindwa katika uchaguzi huu, lakini sikubali kushindwa kwa mapambano yaliyochochea kampeni hii,” alisema Harris.
“Nisikilizeni ninaposema mwanga wa ahadi ya Amerika utaendelea kung’aa, mradi tusikate tamaa kamwe,” aliongeza sauti yake ikiwa imekauka baada ya kampeni kali zilizochukua wiki 13.
Wakati huo huo, Harris alimpigia simu Trump kumpongeza kwa ushindi wake baada ya kuchaguliwa tena kuongoza taifa hilo.
Aliongeza kuwa yeye (Harris) na Rais Joe Biden watasaidia kufanikisha mabadiliko ya mamlaka kwa njia ya amani.
Katika hatua nyingine, Rais Biden pia alizungumza na rais mteule Trump kwa njia ya simu ambapo alimpongeza kwa ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Novemba 5 na kumkaribisha kuitembelea ikulu ya White House akijiandaa kuchukua hatamu za uongozi.
Kukubali hadharani kwa makamu huyo wa rais kulimaanisha mwisho wa mchakato wa uchaguzi uliodumu kwa zaidi ya siku 100.
Trump alishinda uchaguzi wa Jumanne na kuwa rais wa 47 wa nchi hiyo huku akitwaa takriban majimbo matano kati ya saba muhimu yenye ushindani.
Trump na makamu wake JD Vance, wataingia madarakani Januari 20, 2025 kwa muhula wa miaka minne.
Hawa ndio washirika wa karibu wa Trump kote duniani

Kama ilivyo desturi ya kidiplomasia, pongezi zilimiminika kwa Donald Trump kutoka duniani kote baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi. Hebu tuangalie baadhi ya marafiki wa karibu wa Trump na washirika wake:
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel: “Kurejea kwa historia kubwa”
- Trump alisemekana kusikitika wakati Netanyahu alipopongeza ushindi wa Biden mwaka 2020, lakini anasisitiza kuwa wana “uhusiano mzuri sana”
Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary: “Ushindi unaohitajika sana kwa ulimwengu!”
-kama “mmoja wa watu wanaoheshimika zaidi” duniani.
- Mapema mwezi huu, Orbán alisema: “Tutafungua chupa kadhaa za champagne ikiwa Trump atarudi”. Trump awali alimuelezea Orbán -ambaye anatuhumiwa kuwa kiongozi wa kimabavu na
Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia: “Kazi nzuri, Mheshimiwa Rais”
- Meloni alimpigia simu Trump Jumatano usiku kumpongeza na kuthibitisha “urafiki wao wa kina na wa kihistoria”, aliandika kwenye mtandao wa X
Javier Milei, Rais wa Argentina: “Unaweza kuitegemea Argentina kuifanya Marekani kuwa kubwa tena”
- Akizungumzia kumhusu Milei katika mkutano wa hadhara mwezi Machi, Trump alisema: “Ni mtu mkubwa kwa Trump. Anampenda Trump, nampenda, kwa sababu anampenda Trump.”
Je, nani anaweza kuwa katika baraza la mawaziri la Trump?

Wakati wa kampeni yake, Donald Trump alitoa ahadi chache – baadhi kuu kuliko nyingine – kuhusu nani anataka kumuona katika utawala wake. Je ni nani anayeweza kumteua amsaidie katika muhula wake wa pili:
Susie Wiles: Ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika kinyang’anyiro cha urais wa Trump, na anaweza kuwa mkuu wake wa majeshi . Aliyekuwa mshauri wa sera za ndani Brooke Rollins pia anachukuliwa kuwa mtu anayeweza kutekeleza jukumu hilo.
Robert F Kennedy Jr: Trump alisema – ikiwa atachaguliwa – mgombea binafsi wa zamani na mtu anayetilia shaka chanjo anaweza kumteua . Lakini haijahakikishiwa kuwa Seneti ingemthibitisha Kennedy katika wadhifa wa baraza la mawaziri.
Mike Pompeo: Mkurugenzi wa zamani wa CIA na waziri wa mambo ya nje katika urais wa wa awali wa Trump anatajwa kuwa miongoni mwa wale wanaowania kuwa waziri wa ulinzi .
Ric Grenell: Aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Ujerumani na kaimu mkurugenzi wa ujasusi wa kitaifa katika utawala wa mwisho wa Trump. Anachukuliwa kuwa mtu anayewania kuwa katibu wa serikali au mshauri wa usalama wa kitaifa .
Elon Musk: Tumeona na kusikia mengi ya Elon Musk – mtu tajiri zaidi duniani alihusiaka sana katika uchaguzi huu. Trump alidokeza kumpa Musk jukumu lisilo la Baraza la Mawaziri katika utawala wake kusaidia kuondoa taka za serikali katika kile bilionea huyo aliita ” Idara ya Ufanisi wa Serikali.’’
Mataifa sita kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya chess nchini Tanzania,

Wachezaji wa Chess kutoka nchi sita, yakiwemo Tanzania, Poland, Ujerumani, India, Nigeria na Msumbiji, wanatarajiwa kuchuana katika shindano la kupanda viwango la Shirikisho la Kimataifa des Echecs (FIDE).
Mashindano hayo yanayofanyika Desemba 14 na 15, ni mashindano ya mara ya nne ya kufanyika katika Chuo Kikuu cha Jordan mjini Morogoro mashariki mwa Tanzania.
Waandaaji wanajivunia uwepo wa timu hizo za kimataifa katika mashindano hayo, huku wakionyesha umuhimu wake katika kuinua hadhi ya Tanzania katika mchezo wa chess.
“Tunafuraha kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ambapo tayari tuna mataifa sita yamedhibitisha kushiriki,” alisema Dkt Konrad Czernichowski, mmoja wa waandaaji na pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jordan cha Morogoro.
Dkt Konrad aliongeza kuwa, “Pamoja na washiriki kutoka mataifa sita, ni fursa ya kipekee kuinua Tanzania kwenye jukwaa la dunia la mchezo wa chess. Viwango vya Chess sio nambari tu ni onyesho la ustadi, kujitolea, na huwa na hadhi ya kimataifa.”
Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, mchezaji wa mchezo wa chess kutoka Tanzania, Shedrack Mwakajila, ambaye hivi karibuni aliiwakilisha nchi yake kwenye Olympiad ya Chess mjini Budapest, alitembelea Klabu ya Jordan Chess na kucheza mchezo huo na wachezaji mbalimbali
Katika ziara yake, nyota huyo alikabiliana na wachezaji wengi mara moja dhidi yake na baadaye kucheza dhidi ya mchezaji mmoja mmoja. Wapinzani wawili tu ndio waliibuka washindi; mwanafunzi wa chuo hiko Inocent Agustino Herman na Dkt Konrad.
Dkt Konrad alimsifu Mwakajila kama mfano mzuri wa kuigwa na wachezaji chipukizi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Dkt Konrad pamoja na washiriki wa kimataifa na fursa ya kupata viwango vya FIDE, mashindano ya Desemba yanatarajiwa kukuza wasifu wa chess wa Tanzania, kuwapa wachezaji wa ndani jukwaa la kimataifa na kuhamasisha vijana zaidi kujihusisha na mchezo huo.
Chess ni mchezo wa aina gani?

Wataalamu wa elimu wametaja mchezo wa Chess kuwa wenye umuhimu mkubwa katika kukuza vipaji, uwezo wa kufikiria kwa undani na kusuluhisha matatizo yanayokumba jamii, na ubunifu.
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Waendesha mashtaka waanza kutupilia mbali mashtaka ya Trump

Wizara ya sheria na mwendesha mashtaka maalum wa Marekani Jack Smith, wako katika majadiliano kuhusu jinsi ya kumaliza mashtaka dhidi ya Donald Trump, shirika la habari washirika na BBC la CBS linaripoti.
Vyanzo vinataja sera ya muda mrefu ya kutomshtaki rais aliyeko madarakani.
Smith kwa sasa anaongoza kesi nyingi dhidi ya Trump, ambaye atakuwa rais wa kwanza kuchukua madaraka wakati akikabiliwa na kesi kadhaa.
Hii ni pamoja na kesi ya madai ya matumizi mabaya ya nyaraka za siri, na ile inayohusu juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake kwa uchaguzi wa 2020 ambapo Joe Biden alishinda.
Droni za Shahid zaupiga mji mkuu wa Ukraine usiku kucha Kyiv wakati wa shambulio la drone usiku kucha

Urusi imefanya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani aina ya shahed usiku kuanzia saa sita katika mji mkuu Kyiv. Tahadhari ya mashambulizi ya anga ilidumu kwa muda wa saa nane ambapo onyo lilitangazwa usiku wa manane, na kurushwa – saa nane asubuhi.
Wanajeshi wa Urusi walishambulia mji mkuu huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani. Mabaki ya ndege hizo zinazojulikana kama UAVs yalianguka kwenye nyumba za kibinafsi, karakana, vituo vya biashara, vituo vya matibabu, na Barabara.
Watu kadhaa walijeruhiwa na kupelekwa hospitali kufuatia mashambulizi hayo.
Ni wilaya gani za Kyiv zilizoathiriwa

Ripoti za kwanza za meya wa Kyiv kuhusu mashambulizi ya droni hizo zilizoanguka zilionekana saa mbili asubuhi.
Kutokana na shambulio la usiku kucha mjini Kyiv, wilaya tano ziliharibiwa, na kuna majeruhi.
Gereji iliungua moto katika wilaya ya Holosiivskyi, wimbi la shambulio hilo liliharibu vyumba kadhaa katika jengo la makazi. Moto ulizuka katika kituo cha huduma karibu, gazeti la Vitaliy Klitschko liliripoti.
Makombora ya Ukraine
Kwa jumla, wakati wa usiku huo, jeshi la anga la Ukraine lilipiga ndege 36 zisizo na rubani za Urusi za UAVs katika mikoa ya Odesa, Mykolaiv, Kyiv, Sumy, Kirovohrad, Zhytomyr, Cherkasy, Chernihiv na Zaporizhia.
Miundombinu ya reli pia iliharibiwa, haswa vipengele vya usambazaji wa umeme na nyimbo.
Australia inapanga kupiga marufuku kuingia kwenye mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16

Serikali ya Australia inasema itaanzisha sheria ya kupiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kuingia kwenye mitandao ya kijamii ambayo “itakuwa mfano wa kuigwa duniani”
Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema sheria zinazopendekezwa, zitakazowasilishwa bungeni wiki ijayo, zinalenga kupunguza “athari” za mitandao ya kijamii ambayo yanawapata watoto nchini Australia.
“Hii ni ya akina mama na akina baba… Wao, kama mimi, wana wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wetu mtandaoni. Nataka familia za Australia zijue kwamba serikali inawaunga mkono,” alisema.
Ingawa maelezo mengi bado hayajajadiliwa, serikali ilisema marufuku hiyo haitatumika kwa vijana ambao tayari wako kwenye mitandao ya kijamii.
Je, mchakato wa kipindi cha mpito wa kukabidhiana madaraka ukoje?

Rais mteule Donald Trump ataapishwa kuwa rais tarehe 20 Januari 2025.
Ni wakati huu ambapo kisheria atachukua mamlaka na majukumu ya urais.
Kabla ya Januari, mchakato wa kuhesabiwa kwa kura za wawakilishi maalum ndio unaoendelea.
Kila jimbo kwa ujumla hutoa kura za wawakilishi kwa yeyote atakayeshinda wingi wa maarufu. Hii itathibitishwa tarehe 17 Desemba.
Bunge jipya la Marekani kisha litakutana tarehe 6 Januari kuhesabu kura za wawakilishi na kuthibitisha matokeo, hivyo kuthibitisha rasmi rais ajaye.
Ilikuwa ni sehemu hii ya mchakato ambao wafuasi wa Trump walijaribu kusitisha walipovamia Ikulu ya Marekani mnamo 2021 baada ya kukataa kukubali kushindwa na Joe Biden.
Trump ameshinda – lakini hatakuwa katika Ikulu ya White House kwa siku 74

Wakati Donald Trump amepata ushindi unaomrejesha Ikulu ya White House, bado si rais rasmi – na itachukua zaidi ya miezi miwili kabla ya kurejea katika Ofisi ya Oval.
Makabidhiano ya madaraka ya Marekani ni tofauti sana na jinsi mambo yanavyofanyika nchini Uingereza. Mnamo Julai, Sir Keir Starmer aliapishwa kama waziri mkuu ndani ya saa chache baada ya uchaguzi kumalizika na kabla ya Rishi Sunak hata kubeba vitu vyake.
Trump ataapishwa Januari 20 na Joe Biden atasalia madarakani hadi wakati huo – ingawa atakuwa na kikomo cha kisiasa katika kile anachoweza kufanya.
Trump anapaswa kuiruhusu Ukraine kushambulia maeneo lengwa Urusi – balozi wa zamani

Balozi wa zamani wa Donald Trump wa Nato anasema anatumai “ataruhusu Ukraine kushambulia vikosi vya [Urusi] upande wa pili wa mpaka” ili kumaliza mkwamo wa vita.
Akizungumza na BBC, Kay Bailey Hutchinson alisema serikali ya Kyiv inapaswa kulenga “kupata makubaliano ambayo yatawapendelea” baada ya mazungumzo na Trump.
Siku za nyuma, Trump alikosoa kiasi cha matumizi ya misaada ambayo Marekani imejitolea kwa Ukraine chini ya Joe Biden, na inaonekana kwa kiasi kikubwa kutounga mkono juhudi za vita za Ukraine.
Hutchinson pia anasema Trump atatafuta kuhakikisha “biashara huria na ya haki” na China, au kurudisha viwanda nchini Marekani ili kubuni fursa za ajira nyumbani.
Je, Harris atakuwa na kazi baada ya kushindwa uchaguzi?

Kamala Harris ataendelea kutumikia kipindi chake kilichosalia kama makamu wa rais pamoja na Rais Joe Biden, hadi wakati wa makabidhiano ya madaraka kwa Donald Trump na JD Vance tarehe 20 Januari.
Lakini baada ya Rais-Mteule Trump na Makamu wa Rais-Mteule JD Vance kuapishwa, wote wawili Biden na Harris hawatakuwa na nafasi yoyote ya kisiasa katika serikali ya Marekani.
Tofauti na siasa za Uingereza, hakuna nafasi sawa ya “kiongozi wa upinzani” – Harris atakuwa hana kazi. Na si kwamba hawezi kupata fursa zingine.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.