Trump asema amepata ‘ushindi wa ajabu’

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Donald Trump anawahutubia wafuasi wake sasa . Anasema kwamba hii itakuwa “zama za dhahabu” kwa Marekani.

“Huu ni ushindi mzuri sana kwa watu wa Marekani, ambao utaturuhusu kuifanya Marekani kuwa kubwa tena,” anaongeza, akitumia kauli mbiu yake ya kampeni.

Trump ametangaza ushindi, ingawa bado hajapata kura rasmi zinazohitajika za wawakilishi maalum wanaopiga kura kumchagua rais

.

Trump ashukuru familia, akiwemo mke wake Melania

Trump amemshukuru mkewe Melania, akimwita Mama wa Taifa

Amesifu kitabu chake, akisema ndio “namba moja kwa mauzo nchini”.

“Amefanya kazi nzuri,” amesema, akiongeza “amekuwa na bidii ya kusaidia watu”.

Pia amewashukuru “watoto wake wa kipekee,” akiwataja kila mmoja wao wakisimama naye jukwaani.

Trump anamwalika Vance kuhutubia umati

Baadaye, Trump amempongeza mtu ambaye anasema atakuwa makamu wa rais ajaye wa Marekani: JD Vance.

Kisha, akamwomba kuhutubia umati wa watu kidogo.

Vance akapata muda wa kuelezea kampeni ya Trump kama “kitu cha kipekee katika siasa kuwahi kutokea”.

Trump amesema Vance alikuwa chaguo bora

Jimbo la Pennsylvania latabiriwa kumwendea Trump

Jimbo muhimu la Pennsylvania limetabiriwa kuwa litachukuliwa na Donald Trump.

Kura za wawakilishi maalum 19 za jimbo hilo zinamfanya kufikia 265 kwa jumla, pungufu kidogo tu ya 270 zinazohitajika kushinda urais.

.

Msisimko usio wa kawaida ulishuhudiwa wakati Fox News ilipokadiria ushindi wa Donald Trump katika kinyang’anyiro cha urais.

Unapata hisia ya jinsi ambavyo hata wafuasi wake hawaamini wanachokiona.

Wengi walikuwa tayari kusubiri kwa muda zaidi kabla ya matokeo.

Wafuasi wa Trump wanasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mgombea wao

.

Donald Trump anatarajiwa kuzungumza kutoka makao makuu ya kampeni yake huko Florida muda wowote kutokea sasa.

Wafuasi wa Trump wanasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa mgombea wao.

Kuna kamera ndani ya ukumbi uliojaa pomoni na muda mfupi uliopita umati wa watu walikuwa wakiruka juu na chini, mbwembwe zikiwa zimetanda kila sehemu.

.
.

Miongoni mwa watakaokuwepo ni Elon Musk, ambaye amemfanyia kampeni ya kukata na shoka Trump, pamoja na washirika wa kisiasa Robert F Kennedy Jr na Tulsi Gabbard

Wafuasi wa Trump washerehekea ushindi katika majimbo mawili muhimu

Picha zinaonyesha wafuasi wa Donald Trump wenye furaha, wakisherehekea katika baadhi ya sehemu za Marekani huku mteuzi wao wa rais akisonga mbele katika matokeo yaliyotarajiwa.

Wengine wamevalia kofia zilizoandikwa (Make America Great Again – kauli mbiu ya kampeni ya Trump), wengine wamejifunika bendera ya Marekani.

.
.
.
.

Harris hatazungumza usiku wa leo na umati unaondoka

th

Takriban dakika 30 zilizopita, uwanja huu katikati mwa Chuo Kikuu cha Howard ulikuwa umejaa wafuasi wa Kamala Harris tayari kusherehekea.

Lakini kwa makadirio kutoka North Carolina na Georgia, ukumbi wa karamu ya usiku wa uchaguzi wa Harris ghafla umesalia mahame.

Mamia ya wafuasi wanatiririka wakiondoka, wengi sasa wanakataa kuzungumza na vyombo vya habari kwani uwezekano wa ushindi wa Harris unaonekana kupotea.

Harris pia hatarajiwi kuzungumza kwenye hafla hiyo

Pendekezo la haki ya uavyaji mimba huko Florida limeshindwa

xx

Pendekezo linalofuatiliwa kwa ukaribu la kurejesha haki za uavyaji mimba huko Florida liko mbioni kushindwa, hili ni pigo kubwa kwa juhudi za kupanua haki ya uavyaji mimba.

Pendekezo hilo lingeruhusu uavyaji mimba wa hadi wiki 24, lakini linapaswa kupata 60% ili kupita.Florida ni mojawapo ya majimbo 10 katika uchaguzi huu ambapo wapiga kura wanaulizwa kuhusu hatua za utoaji mimba.

Hili linakuja baada ya miaka miwili ya Mahakama ya Juu ya Marekani kutoa uamuzi uliofuta haki ya kitaifa ya kutoa mimba, na kusababisha majimbo mengi kuanzisha marufuku au vizuizi vikali dhidi ya uavyaji mimba.

Wanaharakati huko Florida walihimiza marekebisho hayo kama njia ya kupuuza sheria iliyoanza kutumika mapema mwaka huu, ambayo ilipiga marufuku utoaji mimba baada ya wiki ya sita ya ujauzito.

Katika chaguzi zilizopita, mipango ya kupanua haki za utoaji mimba ilipata mafanikio, ikiwa ni pamoja na katika majimbo ya kihafidhina kama vile Kansas.

Uavyaji mimba pia uko kwenye kura katika majimbo kama vile Missouri, Dakota Kusini na Arizona, ambayo yana sheria zinazozuia au kupunguza urahisi wa kuavya mimba.

Tangu uamuzi wa 2022 wa Roe v Wade, majimbo 22 yamebadilisha sheria za utoaji mimba, yakiwemo majimbo 13 ambapo yamepiga marufuku kabisa. Majimbo mengine yameweka vizuizi vya utoaji mimba baada ya wiki sita.

Msimamo wa utawala wa Biden-Harris wa Israel wawaponza huko Michigan

.

Dearborn, Michigan, jiji lenye Waarabu wengi, wapiga kura wote ambao wamezungumza na BBC, walisema wanampigia kura mgombeaji wa Green Party Jill Stein kwa sababu ya kukatishwa tamaa kwao na msimamo wa Biden-Harris wa kuunga mkono Israel.

Miongoni mwao ni Sajid Sayed, ambaye alikuwa akijitambulisha kama mfuasi wa Democrat. Sayed anasema hampendelei Donald Trump kuliko Kamala Harris, lakini Trump anaweza kuwashawishi baadhi ya wapiga kura kwasababu alitembelea jamii zao.

Rais huyo wa zamani alikuja Dearborn Ijumaa iliyopita kukutana na viongozi wa biashara.

“Alisikiliza shida zao,” Sayed anasema. “Alikula chakula cha jioni na wao. Alizungumza na viongozi.”

Kufikia sasa hakuna mtu ambaye amesema amempigia kura Trump – lakini wanafahamu ukweli kwamba kura yao kwa mtu mwingine inaweza kumpendelea Trump.

“Sijisikii vizuri kuhusu hilo,” Sayed anasema. Lakini, akaongeza, “Ikiwa Harris atashindwa, basi atajua kwamba hiki ndio chanzo chake.”

Upigaji kura wakamilika katika majimbo yote isipokuwa Hawaii na Alaska

xx

Vituo vya kupigia kura katika majimbo yote yamefunga, yakiwemo majimbo ya Pwani ya Magharibi.

Matokeo ya zaidi ya nusu ya majimbo tayari yametangazwa.

Matokeo hayo kufikia sasa yanawiana na kile kilichotarajiwa: Trump ameshinda katika majimbo ya kijadi ya Republican, huku Harris akinyakua ushindi katika ngome za Democratic.

Hakuna hata moja ya majimbo muhimu ambayo yametangazwa kufikia sasa.

Miongoni mwa majimbo ambayo upigaji kura umekamilishwa ni California, ngome ya jadi ya chama cha Democratic ambayo inatarajiwa kumpa Kamala Harris idadi kubwa ya kura 54 ya wawakilishi maalum.

Harris anaungwa mkono na wanawake wengi lakini sio kwa kishindo – kura za maoni

.

Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mgawanyiko wa kijinsia katika uchaguzi huu.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wanawake wanamuunga mkono Harris kwa karibu 54%, ikilinganishwa na 44% kwa Trump.

Lakini Rais Joe Biden alikuwa na mgawanyiko mkubwa wa kijinsia mnamo 2020, na 57% ya wanawake walimpigia kura.

Data ya kura ya maoni inaongezwa usiku kucha kwa hivyo hii sio idadi ya mwisho. Pia haifichui kile kinachotokea katika majimbo muhimu ambayo yeyote anaweza kushinda.

Ukiangalia kinyang’anyiro hicho, Trump anaongoza kwa wapiga kura wazungu – kundi kubwa zaidi – na Harris anaongoza kwa wapiga kura weusi.

Pia yuko mbele na wapiga kura wa Kihispania lakini inaonekana kama uungwaji mkono kwa Trump umeongezeka zaidi ya pointi 10 katika kundi hili ikilinganishwa na mwaka 2020.

Democrat wanatarajia kuhifadhi jimbo la Arizona baada ya kupata ushindi mdogo mwaka 2020

.

Katika eneo la Arizona waliokita kambi ni wafuasi wa chama cha Democrat ambapo waliberali wanatarajia kushinda jimbo hilo.

Mwaka 2020, Joe Biden alipata ushindi mdogo wa takriban kura 10,000 – na kuwa Democrat wa pili kushinda jimbo hilo katika miaka 70.

Upigaji kura ndio umekamilika katika jimbo hilo lote lakini muda umeongezwa katika Kaunti ya Apache baada ya kulalamikia mahakama kuhusu hitilafu.

Hitilafu zilizoripotiwa ni pamoja na masuala kama vile vichapishaji kutofanya kazi.

Mahakama ya Juu ya Arizona iliongeza muda wa kupiga kura kwa saa mbili. Inaripotiwa kuwa kuna wapiga kura wapatao 43,000 katika kaunti hiyo.

Kura za wawakilishi maalum 270: Je, wagombea hushinda vipi?

Kuna majimbo 50 nchini Marekani na mengi yao hupigia kura chama kimoja katika kila uchaguzi.

Lakini kuna majimbo machache – yanayojulikana kama majimbo muhimu – ambapo mgombea yeyote anaweza kushinda.

Majimbo haya ni Nevada, Arizona, North Carolina, Georgia, Wisconsin, Michigan na Pennsylvania.

Majimbo yenye watu wengi ndio muhimu zaidi, ikitafsiriwa kwa idadi ya kura 270 za wawakilishi maalum wanaomchagua rais zinazohitajika chini ya mfumo wa kura za majimbo.

Kuna kura 538 za wawakilishi hao ambazo mgombea anaweza kujinyakulia kwa jumla.

Rais ajaye atakuwa mgombea atakayepata kura 270 au zaidi za wawakilishi hao maalum.

Wagombea wote wawili watahitajika kushinda angalau majimbo matatu muhimu ili kuwapitisha kwenye idadi ya kura ambazo ni lazima kupata.

Trump ashinda katika jimbo la Florida huku shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea

,

Shangwe na nderemo zimetawala upande wa Donald Trump huko Palm Beach, Florida alipotangazwa kuwa anayetarajiwa kupata ushindi katika jimbo hilo.

Haikuwa na shaka kamwe kwamba angeweza kupata ushindi katika jimbo hilo ambalo kwa sasa Republican ndio wako kifua mbele.

Kulingana na mchambuzi wa BBC, Anthony Zurcher, siku za jimbo la Florida kuwa uwanja wa kutafuta ushindi wa urais zimepitwa na wakati.

Miaka 24 iliyopita, kura mia chache katika jimbo hilo zilikuwa kichocheo cha kupata urais kwa George W Bush wa chama cha Republican dhidi ya Al Gore wa Democrat.

Kwa sasa, 73% ya kura zikiwa zimehesabiwa, Donald Trump amekadiriwa kushinda jimbo hilo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment