Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wanajeshi wa Israeli wameendelea kutekeleza mashambulio ya angaa kwenye ukanda wa Gaza kulenga kundi la Hamas, na kusababusha vifo vya Wapalestina 13 wakiwemo wale waliokuwa wanaishi kwenye kambi za wakimbizi.
Mashirika ya kiraia kwenye ukanda wa Gaza, yamethibitisha mauaji hayo, yakiwemo ya watu wanne wa familia moja, Mashariki mwa mji huo.
Mashambulio mengine yametokea katika kambi ya wakimbizi, Mashariki mwa mji wa Khan Yunis na kusababisha vifo vya watu watatu na kuwaacha wengine na majeraha usiku wa kuamkia Jumanne wa mashambulio mazito dhidi ya Hamas.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Israeli limesema, vikosi vyake vimeendeleza mashambulio ya angaa na ardhini Kaskazini mwa Gaza ambako mamia ya watu wameuawa tangu tarehe 6 mwezi Oktoba mwaka uliopita.
Nalo Shirika la afya duniani, WHO limesema, wagonjwa zaidi ya 100 wakiwemo watoto wanaosumbuliwa na magonjwa sugu na matatizo ya akili watahamishwa kutoka kwenye ukanda wa Gaza kwenda katika nchi ya Falme ya Kiarabu na Romania kupata matibabu zaidi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.