Uingereza kutumia mbinu mpya ya ushirikiano na bara Afrika: David Lammy

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Lammy, amesema nchi yake itatumia mbinu mpya ya ushirikiano na nchi za Afrika, ambapo itakuwa inasikiliza zaidi kuliko kuelekeza, wakati huu akitarajiwa kuanza ziara kwenye nchi za Nigeria na Afrika Kusini.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, David Lammy.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, David Lammy. REUTERS – Isabel Infantes

Lammy amesema mbinu mpya itachangia ushirikiano wenye heshima na bara la Afrika, lengo kuu likiwa kukuza uhusiano na kuleta ukuaji wa muda mrefu badala ya ufumbuzi wa muda mfupi.

Akiwa nchini Nigeria, waziri huyo anatarajiwa kutia saini ushirikiano wa kimkakati ambao utashughulikia ukuaji, usalama wa kitaifa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mataifa ya mbalimbali ya Magharibi yamekuwa yakiimarisha uhusiano wake na nchi za bara Afrika.
Mataifa ya mbalimbali ya Magharibi yamekuwa yakiimarisha uhusiano wake na nchi za bara Afrika. REUTERS – Maja Smiejkowska

Kisha ataelekea Afrika Kusini ambapo pia atatia saini makubaliano ya kuunda Mpango mpya wa Ukuaji wa Uingereza na Afrika Kusini, kulingana na Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza.

Pia atahudhuria mkutano mjini Cape Town, ambapo atazungumza na wabunifu kuhusiana na jinsi Uingereza inaweza kusaidia kuelekeza fedha kwenye suluhu za mazingira.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment