Uhalifu dhidi ya waandishi wa habari: Kesi kadhaa zarekodiwa nchini Mali na Burkina Faso

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Tarehe 2 Novemba ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Uhalifu dhidi ya Wanahabari, tarehe iliyochaguliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwakumbuka wenzetu, Ghislaine Dupont na Claude Verlon, waliouawa Novemba 2, 2013 nchini Mali. Katika nchi kama Burkina Faso, visa vya mashambulizi, utekaji nyara na kutoweka kwa waandishi wa habari bado vinarekodiwa.

Katika duka la magazeti mjini Bamako.
Katika duka la magazeti mjini Bamako. AFP/ISSOUF SANOGO

Kukimbilia uhamishoni pengine ni njia iliyokoa maisha ya mwanahabari Malick Konate. Mnamo mwaka 2022 huko Bamako, watu wawili waliojifunika nyuso zao walivunja madirisha ya gari lake. Hakuwa ndani ya gari, lakini ujumbe ulikuwa wazi.

Mwenzake Birama Touré kutoka Gazeti la kila wiki la Le Sphinx hakubahatika kuondoka kwa wakati. Ni miaka minane sasa, “ametoweka”. Mahakam ya Mali imefungua uchunguzi, lakini hakuna maendeleo yoyote.

Karibu na Mali, nchini Burkina Faso, hatima ya waandishi wa habari wanne nchini humo inatia wasiwasi. Shirika la Waandishi wa habari Wasio na Mipaka linasema kwa uwezekano wote, “wanashukiwa kuwa wako mikononi mwa wanajeshi”.

Mwandishi wa habari mmoja alitekwa nyara, mwingine kutoweka

Mmoja wao anaitwa Serge Oulon, ni mkurugenzi wa idara ya uchapishaji wa Gazeti la L’Événement. Rafiki wa karibu wa utawala wa kijeshi aliwasilisha malalamiko dhidi yake kwa “kashifa na matusi ya umma”. Juni 24, siku ya kesi, hakufika mahakamani.

Kisha ilifahamika kwamba wakati huo alikuwa ametekwa nyara, kulingana na vyanzo kadhaa, na watu wanaodhaniwa kuwa maafisa wa Idara ya ujasusi (ANR). Kulingana na jamaa zake wawili, alikuwa na majeraha mwilini, hali inayoonyesha kuwa alifanyiwa kipigo.

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Burkina faso, Kapteni Ibrahim Traoré, wiki chache baadaye, alithibitisha kuandikishwa kwa mwandishi wa habari katia jeshi, bila kumtaja mwandishi huyo.

Mwezi wa Julai mwaka huu, mwandishi mwingine wa Burkina Faso, Alain Traoré, alitoweka. Watu wenye silaha waliojifunika nyuso zao wanaodai kutoka Idara ya ujasusi wanadaiwa kumteka nyara kutoka nyumbani kwake. Tangu wakati huo, hakuna habari kutoka kwake. Habari za kutisha ambazo haziwezi kuthibitishwa kwa sasa zimewafikia wapendwa wake.

Orodha ya wanahabari ambao wametoweka nchini Burkina Faso pia inajumuisha waandishi wawili wa safu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment