Jeshi la Chad lashutumiwa kwa kuua ‘dazeni’ za wavuvi nchini Nigeria

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mashambulizi ya Chad dhidi ya Boko-Haram katika eneo la Ziwa Chad, “binafsi” yakiongozwa na Rais Déby, yalilaumiwa Alhamisi na wavuvi wa ndani na wanamgambo wanaopinga wanajihadi kwa kuwaua kimakosa “dazeni” za wavuvi nchini Nigeria, wakitaka kuwalenga wanajihadi. 

Wanajeshi wa Chad waliotumwa katika eneo la Ziwa Chad.
Wanajeshi wa Chad waliotumwa katika eneo la Ziwa Chad. © AP

Afisa mkuu makao makuu ya jeshi la Chad ambaye aliomba jina lake lisitajwe amethibitisha mashambulizi hayo kwa shirika la habari la AFP “yalioendeshwa kwenye visiwa vilivyo kwenye mipaka ya Nigeria na Niger”. “Boko Haram mara nyingi huungana na wavuvi na wakulima kila mara wanapofanya uhalifu wao kwa hiyo ni vigumu kutofautisha kati ya watu na magaidi,” amesema.

Ndege kivita ya jeshi la Chad ilishambulia wavuvi katika kisiwa cha Tilma, na kuua wavuvi wengi,” amesema Babakura Kolo, kiongozi wa wanamgambo wanaopinga wanajihadi nchini Nigeria. “Ndege hiyo “iliwalenga wavuvi kimakosa ikidhani iliwalenga magaidi wa Boko Haram ambao walishambulia kambi ya kijeshi nchini Chad siku ya Jumapili,” ameongeza.

Matokeo ya mashambulizi haya, yaliofanywa usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu na Boko Haram dhidi ya kambi ya kijeshi katika eneo la Ziwa Chad, ni “takriban watu arobaini waliouawa”, kulingana na mamlaka ya Chad. “Ndege ya kivita ‘ilizingira’ eneo la Tilma kabla ya kuanza kurusha mabomu huku watu wakikimbia kila upande kutafuta hifadhi,” amesema Sallau Arzika, mvuvi.

Déby aliongoza mashambulizi haya mwenyewe

Mashambulizi hayo yaliyozinduliwa na jeshi la Chad dhidi ya Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad yaliongozwa “binafsi” na Rais Déby , isara ya mawasiliano katika ofisi ya rais ilitangaza siku ya Alhamisi.

“Rais wa Jamhuri, Mkuu wa Majeshi, Mahamat Idriss Déby Itno bado amepiga kambi kwenye mipaka ya Ziwa Chad ambapo yeye binafsi anaongoza operesheni ya ‘Haskanite'” ofisi ya rais imetangaza kwenye Facebook, huku ikionyesha picha ya mkuu wa nchi akivalia sare ya jeshi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment