Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Burkina Faso, mhubiri amepigwa marufuku kuhubiri katika misikiti ya Jumuiya ya Waislamu, mojawapo ya vyama vya Waislamu nchini humo. Ni uamuzi wa Mwenekiti wa Baraza Kuu la Maulamaa, linalohusika na Masuala ya Kiislamu ya jumuiya ya Waislamu. Marufuku haya yanafuatia mahubiri yenye “msimamo mkali” ya imamu huyu kulingana na viongozi wa jumuiya ya Waislamu.

Mwenyekiti wa Baraza la Juu la Maulamaa, linalohusika na masuala ya Kiislamu ya jumuiya ya Waislamu, anamshutumu mhubiri Ousseini Kaboré kwa kutoa mara kwa mara “mahubiri makali na yasiyofaa” misikitini.
Sheikh Mahamoudou Bandé anasisitiza kwamba mahubiri ya mhubiri huyo huenda yakawafanya waumini wa Kiislamu kuwa na msimamo mkali na kuvuruga utulivu wa umma. Kwa hiyo, amepigwa marufuku kuhubiri au kuongoza sala yoyote katika misikiti yoyote ya jumuiya ili kuhifadhi “utaratibu, nidhamu na maelewano mazuri” misikitini.
Mkuu wa masuala ya Kiislamu kwa umma wa Kiislamu anatahadharisha kwamba endapo atatokea kutofuatwa uamuzi huu, atawajibika kwa “matendo yake” na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa “sheria na kanuni zinazotumika”.
Adhabu ambayo inakuja siku ile ile ya kusimikwa kwa kamati yenye jukumu la kufuatilia mahubiri na maoni katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Kamati ambayo dhamira yake ni kutambua matumizi mabaya na kupendekeza vikwazo.
Mnamo tarehe 25 Oktoba, Shirikisho la Jumuiya za Kiislamu lilishutumu mikengeuko hatari katika mijadala ya kidini, na kuwataka wahubiri na maimamu wote kuendeleza mijadala isiyo na vurugu, chuki na madhehebu.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.