Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Eugène Rwamucyo, daktari wa zamani wa Rwanda, amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela. Uamuzi huo umetolewa hivi punde siku ya Jumatano Oktoba 30 jioni katika Mahakama ya Paris. Amepatikana na hatia, miongoni mwa mambo mengine, ya kula njama katika mauaji ya kimbari ya Watutsi mwaka 1994. Hata hivyo, amefutiwa mashtaka ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Eugène Rwamucyo alianza kutumikia kifungo chake jela usiku wa Oktoba 30, 2024 kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Paris. Alipata wakati wa kuzungumza na familia yake na wafuasi wake wengi waliokusanyika nyuma yake kwenye chumba cha Vedel, anaripoti mwandishi wetu wa habari Nadia Ben Mahfoudh. Huu ndio mwisho wa kesi iliyoanza Oktoba 1.
Amepatikana na hatia ya kula njama katika mauaji ya halaiki na kushiriki katika makubaliano ya kuandaa mauaji ya kimbari, kushiriki katika uhalifu dhidi ya ubinadamu na hatimaye kushiriki katika makubaliano ya kujiandaa kwa uhalifu huu. Daktari huyu wa zamani na mwalimu, ambaye sasa ana umri wa miaka 65, alishutumiwa kwa kushiriki katika mauaji ya waliojeruhiwa, lakini pia kwa kuwachochea watu hadharani kushambulia Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994.
Alain Gauthier, rais wa muungano wa vyama vya kiraia nchini Rwanda ambaye aliwasilisha malalamiko katika kesi hii, anasema anakubali uamuzi huu wa kimahakama hata hivyo hajaridhishwa na uamuzi huo: “Ninaona familia ikitokwa na machozi, ni jambo la kawaida kuwa hivyo. lakini pia naona kufuatia hatua zetu na malalamiko tuliyowasilisha, mauaji yote ya halaiki tuliyoshtaki yamehukumiwa,” ameeleza.
Hukumu hiyo inaashiria mwisho wa vita vya muda mrefu vya Gasana Ndoba, rais wa zamani wa tume ya haki za binadamu ya Rwanda na chama cha kiraia katika kesi dhidi ya Eugène Rwamucyo. “Ni afueni kujua kwamba hatimaye amepatikana na hatia. Sasa, wengine ambao walifanya vitendo kama hivyo watajiambia kuwa itakuwa zamu yao kesho, au katika miaka miwili au mitatu. Inatia moyo, na ninaweza tu kutumaini kwamba mchakato unaendelea na kwamba unazidi nchini Ufaransa ambako kuna ucheleweshaji mkubwa wa kusughulikia kesi hii ya mauaji ya halaiki,” anasema kwenye kipaza sauti cha mwandishi wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud.
Eugène Rwamucyo hata hivyo alifutiwa mashtaka mawili: ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambayo inaelezea miaka 27 jela badala ya miaka 30 inayotakiwa na upande wa mashtaka. Hukumu hiyo “haikubaliki (…) haifai kwa kesi ya kihistoria ambayo ingelipaswa kuwa” imejibu moja kwa moja wakili wake, ambaye alitangaza kwamba atakata rufaa.
Faili iliyojaa ushahidi
Daktari na mwalimu amekuwa akisema kuwa hana hatia. Asubuhi ya Oktoba 30, Eugène Rwamucyo alikaa kimya kwa sekunde chache kabla ya kusema. Kwa sauti isiyoeleweka kabisa, aliishia kunong’ona kwamba hajawahi kuamuru au kuruhusu watutsi wauawe: “Ninaelewa mateso ya wale ambao bado wanatafuta wapendwa wao (…) lakini sina cha kuwasaidia, sijui lolote,” alisema kabla ya mahakama kuchukuwa uamuzi.
Hata hivyo, jalada lililoletwa na mwendesha mashtaka na mawakili wa vyama vya kiraia 530 lilikuwa na mambo mengi dhidi yake, hususan kumbukumbu ya hotuba aliyoitoa chuoni kwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Jean Kambada. Ilikuwa Mei 14, 1994 huko Butaré, mji wa kusini ambapo mauaji ya halaiki yalianza baadaye kuliko katika maeneo mengine. Katika hotuba hii iliyorushwa kwenye Radio Des Mille Collines, Eugène Rwamucyo anawahamasisha watu kuwashambulia Watutsi. Anaonekana kama mtu mwenye mamlaka katika eneo hilo, anashutumiwa kuwa mdhamini wa kiakili wa mauaji ya kimbari.
Miaka kumi na minne ilipita kati ya kukamatwa kwa mshtakiwa na hukumu iliyotolewa Jumatano hii. Miaka thelathini baada ya mauaji ya kimbari, takriban kesi arobaini za washukiwa wanaoishi nchini Ufaransa bado zinachunguzwa. Philibert Gakwenzire, rais wa chama cha walionusurika mauaji ya kimbari, Ibuka, anamwambia mwanahabari wetu Lucie Mouillaud: “Kwa kweli tunapaswa kwenda mbali zaidi, kwa sababu faili zilizosalia bado ni nyingi sana, na kesi hizi si mfano mdogo kuliko ile ya Rwamucyo. “
Eugène Rwamucyo ni Mnyarwanda wa tisa kuhukumiwa nchini Ufaransa kwa uhalifu unaohusishwa na mauaji ya kimbari ya Watutsi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.