AFRIKA LEO MCHANA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari

  • Kithure aapa kuwahudumia Wakenya kwa moyo wake wote
  • Profesa Kithure Kindiki aapishwa rasmi kuwa naibu rais mpya wa kenya
  • Ndege 31 zisizo na rubani zadunguliwa Ijumaa usiku, Jeshi la anga la Ukraine lasema
  • Chama tawala cha Botswana chakataliwa baada ya miaka 58 madarakani
  • Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150
  • Saba wauawa Israel katika shambulio baya zaidi la roketi la Hezbollah kuwahi kushuhudiwa katika miezi kadhaa

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Mchana.

Kithure aapa kuwahudumia Wakenya kwa moyo wake wote

Naibu Rais mpya wa Kenya Kithure Kindiki amemshkuru rais William Ruto kwa kumteua kuwa naibu wake.

Akihutubia umati mkubwa wa watu muda mfupi baada ya kuapishwa , bwana Kindiki amesema kwamba atakuwa mtiifu kwa rais Willima Ruto.

Alisema kwamba atahudumu chini ya rais na kumsaidia kuongoza taifa la Kenya .

Bwana Kindiki hususan aliwashukuru wale wote waliochangia mafanikio yake.

Alisema: ”Ninakuahidi Mheshimiwa Rais kuwa nitahudumu chini yako na kukuunga mkono kuiongoza nchi hii.”

“Ninawaahidi katika mkutano huu mbele ya Mungu kwamba sitakuangusha,” akasema.

Bwana Kindiki ameahidi kuwa hatamuangusha Rais Ruto katika majukumu yake.

”Naomba Mungu anisaidie kutekeleza majukumu haya”, anasema.

Aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani nchini kenya Profesa Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa naibu rais mpya wa Kenya.

Kithure Kindiki anachukua mahala pake Rigathi Gachagua aliyeondolewa madarakani.

Kindiki anachukuwa wadhfa huo baada ya siku kadhaa za makabiliano ya mahakamani kati ya mawakili wa aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua na wale wa serikali.

Gachagua alikwenda mahakamani kuzuia kuapishwa kwa Kindiki baada ya kudai kwamba aliondolewa madarakani kinyume na sheria.

Hafla ya kuapishwa inafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.

Taarifa ya gazeti la serikali kuhusu hafla hiyo ilitolewa saa chache tu baada ya Mahakama kuu kuondoa agizo la kuzuiwa kwa Prof. Kindiki kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.

“Inaarifiwa katika taarifa ya umma kwamba hafla ya kuapishwa kwa Naibu Rais mteule itafanyika Ijumaa, Novemba 1, 2024, katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kenyatta (KICC) katika kaunti ya Nairobi, kuanzia saa 10 asubuhi. ,” ilisema taarifa ya gazeti la serikali iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau.

Hii inakuja baada ya Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua kupata pigo baada ya Mahakama ya rufaa ya Kenya kukataa kutoa maagizo ya kuizuia Mahakama kuu kuendelea na kesi ya kuondolewa madarakani.

Vita vya Ukraine: Ndege 31 zisizo na rubani zimedunguliwa Ukraine, Jeshi la anga la Ukraine lasema

f

Usiku wa tarehe 1 Novemba, jeshi la Urusi limeishambulia Ukraine kwa makombora matatu ya ndege ya X-59/69, droni 48 za aina ya Shahed, pamoja na droni za “aina isiyojulikana,” kulingana na ripoti ya kila siku ya Ukraine kuhusu ya jeshi la anga la Ukraine.

Pia inabainisha kuwa mfumo wa ulinzi wa anga, ulidungua droni 31 kwa risasi na droni nyingine 14 “zilipotea ndani,” na tatu zaidi ziliruka kuelekea Belarus.

“Pia, ulinzi wa anga ulifanikiwa kuangusha kombora moja la ndege iliyokuwa ikiongozwa na droni ya X-59/69. Malengo ya mashambulizi ya Urusi hayakufikiwa,” ripoti hiyo inasema.

Jeshi la anga lilibaini kuwa, hakukuwa na majeruhi.

Haya yanakijiri Urusi inaripoti kuwa jana usiku, mifumo ya ulinzi wa anga ilidungua ndege zisizo na rubani 83 za Ukraine katika maeneo ya Kursk, Voronezh, Bryansk, Oryol na Belgorod, pamoja na eneo lililotwaliwa na Urusi, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.

“Mifumo ya ulinzi wa anga iliangusha na kuharibu ndege 83 zisizokuwa na rubani za Ukrain. UAV 36 zilipigwa risasi juu ya eneo la mkoa wa Kursk, 20 juu ya eneo la mkoa wa Bryansk, 12 juu ya eneo la Jamhuri ya Crimea, nane juu ya eneo la mkoa wa Voronezh, nne juu ya eneo la Oryol na tatu katika eneo la Belgorod,” ujumbe huo unasema.

Chama tawala cha Botswana chakataliwa baada ya miaka 58 madarakani

g
Maelezo ya picha,Maafisa walihesabu kura Alhamisi nzima

Wapiga kura nchini Botswana wamekikataa chama tawala cha muda mrefu cha nchi hiyo katika matokeo ambayo yanaashiria mtikisiko wa kisiasa katika taifa hilo lenye utajiri wa almasi kusini mwa Afrika.

Chama cha Kidemokrasia cha Botswana (BDP) kilichokuwa madarakani tangu uhuru mwaka 1966 kilikuwa kimeshinda kiti kimoja tu cha ubunge kufikia mapema Ijumaa asubuhi, matokeo ya awali ya uchaguzi yanaonyesha.

Chama cha Umbrella for Democratic Change (UDC), kinachoongozwa na wakili wa haki za binadamu Duma Boko, kilishinda viti 20, kulingana na hesabu za awali.

UDC kinaonekana kitaunda serikali huku kikitarajiwa kupitisha kizingiti cha viti 31 kwa wingi wa wabunge.

Wabunge wanapomchagua rais nchini Botswana, Duma Boko yuko mbioni kuwa mkuu wa nchi mara tu bunge litakapokutana kwa mara ya kwanza.

Boko, ambaye anagombea kwa mara ya tatu, amewataka wafuasi wake “kudumisha umakini na nidhamu”.

Licha ya kusimamia mabadiliko makubwa nchini Botswana, ukuaji duni wa uchumi wa hivi karibuni na ukosefu mkubwa wa ajira ulidhoofisha umaarufu wa BDP.

Atachukua nafasi ya Mokgweetsi Masisi ambaye aliingia madarakani tangu 2018 na kuongoza kampeni ya BDP iliyoshindwa kupata matokeo mazuri ya kura.

Katika kampeni yake Rais alinadi ujumbe kwamba chama chake kinaweza kuleta “mabadiliko”, lakini hakuna wapiga kura wa kutosha waliokuwa na imani kwamba BDP knaweza kufanya kile ambacho nchi inakihitaji.

Uhispania yaomboleza huku idadi ya vifo vya watu waliofariki kutokana na mafuriko ikizidi 150

g
Maelezo ya picha,Mafuriko yalisomba mamia ya magari mjini Valencia

Takriban watu 158 wamefariki katika maafa makubwa zaidi ya mafuriko nchini Uhispania katika vizazi huku waokoaji wakipambana kutafuta manusura.

Siku ya Alhamisi zaidi ya wafanyakazi 1,200, wakisaidiwa na ndege zisizo na rubani, walitumwa kufanya kazi ya uokoaji huku mvua ikiendelea kusababisha tisho la maafa zaidi maeneo mbali mbali ya nchi hiyo.

“Kwa sasa jambo la muhimu zaidi ni kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo,” Waziri Mkuu Pedro Sánchez aliwaambia waathiriwa katika ziara ya kutembelea jamii zilizoathirika.

Lakini katika baadhi ya miji iliyoathiriwa zaidi na mafuriko ya Jumanne usiku, watu walikumbwa na kazi ya kuopoa miili kutoka kwenye matope na vifusi vya majengo yaliyoporomoka kufuatia mafuriko.

Vifo visivyopungua 155 vilirekodiwa katika mji wa Valencia, huku vingine viwili vikirekodiwa katika eneo la Castilla-La Mancha magharibi mwa jimbo hilo, na raia Muingereza, alitangazwa kufariki Andalusia.

Saba wauawa Israel katika shambulio baya zaidi la roketi la Hezbollah kuwahi kushuhudiwa katika miezi kadhaa

g
Maelezo ya picha,Moshi ulionekana ukifuka katika mji wa Israel wa Metula kufuatia shambulio la roketi la Hezbollah siku ya Alhamisi

Mashambulizi mawili tofauti ya roketi ya Hezbollah yamewauwa watu saba kaskazini mwa Israel, mamlaka yanasema ni siku mbaya zaidi ya mashambulizi hayo katika kipindi cha miezi.

Mkulima wa Israel na wafanyakazi wanne wa kigeni wa kilimo waliuawa wakati roketi zilipotua karibu na Metula, mji ulio kwenye mpaka na Lebanon, Waziri wa Mambo ya Nje Israel Katz amesema.

Baadaye, mwanamke wa Kiisraeli na mwanaye waliuawa katika shamba la mizeituni karibu na Kibbutz Afek, nje kidogo ya mji wa pwani wa Haifa.

Hezbollah ilisema imerusha makombora kuelekea eneo la Krayot kaskazini mwa Haifa na kwenye ngome ya vikosi vya Israel iliyopo kusini mwa mji wa Lebanon wa Khiam, uliopo nje ya mpaka kutoka Metula.

Jeshi lilisema jumla ya makombora 55 yalirushwa kuelekea eneo la Magharibi mwa Galilaya, iliko miji ya kibbutz , Galilaya ya Kati na Galilaya ya Juu mapema alasiri.

Baadhi ya makombora yalidunguliwa na mifumo ya ulinzi wa makombora ya ang awa Israel huku mengine yakaanguka katika maeneo ya wazi, liliongeza jeshi la Israel.

Kithure Kindiki AMEApishwa kuwa Naibu Rais wa Kenya leo

h
Maelezo ya picha,Profesa Kindiki Kithure

Profesa Kithure Kindiki ameapishwa leo rasmi kuwa Naibu Rais mpya leo tarehe 1, Novemba 2024.

Hafla ya kuapishwa itafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta (KICC) jijini Nairobi.

Taarifa ya gazeti la serikali kuhusu ilitolewa saa chache tu baada ya Mahakama kuu kuondoa agizo kuzuiwa kwa Prof. Kindiki kuchukua wadhifa wa Naibu Rais.

“Inaarifiwa katika taarifa ya umma kwamba hafla ya kuapishwa kwa Naibu Rais mteule itafanyika Ijumaa, Novemba 1, 2024, katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Kenyatta (KICC) katika kaunti ya Jiji la Nairobi, kuanzia saa 10 asubuhi. ,” ilisema taarifa ya gazeti la serikali iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau.

Hii inakuja Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua alipata pigo baada ya Mahakama ya rufaa ya Kenya kukataa kutoa maagizo ya kuizuia Mahakama kuu kuendelea na kesi ya kuondolewa madarakani.

g
Maelezo ya picha,Prof. Kindiki Kithure akiwa na Rais William Ruto

Gachagua alikwenda katika mahakama ya rufaa akisema kuwa hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa wiki iliyopita na mahakama ya majaji watatu uliyoidhinisha uamuzi wa Naibu jaji mkuu iliyoundwa na Naibu jaji mkuu Philomena Mwilu. Hata hivyo malalamiko yake yalitupiliwa mbali na Mahakama.

Tarehe 17 Oktoba Naibu Rais aliyetimuliwa aliondolewa madarakani na siku iliyofuata Rais Ruto akamteua Profesa Kindiki kuchukua wadhifa huo siku inayofuata.

Hoja ya kumtimua madarakani Bw Gachagua ulianzishwa na mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse katika Bunge la taifa.

Ndani ya mwezi mmoja Gachagua alijipata akitumuliwa na mabunge yote mawili, Bunge la kitaifa na Baraza la Seneti.

Uchaguzi wa Marekani 2024: Je, upigaji kura kwa barua za posta hufanyikaje?

df
Maelezo ya picha,Wamarekani wanaweza kupiga kura katika uchaguzi huu kupitia kura za barua za posta

Wamarekani wanaweza kuchagua rais wa nchi hiyo yenye ushawishi mkubwa zaidi duniani kwa njia ya posta, licha ya upigaji kura huo kutiliwa shaka na rais wa zamani na mgombea wa sasa Donald Trump hapo mwanzoni.

Zaidi ya mwezi mmoja kabla ya uchaguzi, wapiga kura wa Marekani walianza kupiga kura ya mapema. Septemba 20, kura ya mapema ilianza katika majimbo kadhaa kati ya 47 ambayo hutoa fursa za kupiga kura ya mapema.

Upigaji kura wa mapema unajumuisha upigaji kura wa ana kwa ana au kura za barua za posta. Kila jimbo la Marekani linaweza kuweka kanuni ya namna wakazi wake wanavyopiga kura zao.

Wengine watapiga kura kupitia masanduku ya mtaani ya kupigia kura, wengine kwenye vituo vya kupigia kura. Na wengine watapiga kura wakiwa mbali, wiki kabla ya tarehe ya kupiga kura.

Aina ya kura za barua ya posta

trfg
Maelezo ya picha,Baadhi ya majimbo yanawataka wapiga kura kutoa sababu ya kuomba kura ya aina hiyo

Shirika la Habari la Associated Press linasema hakuna tofauti kubwa kati ya upigaji kura kituoni na kutuma kwa barua, kwa kuwa zote zinahusisha kura mbayo mwisho hutiwa katika masanduku ya vituoni au mahali pengine palipoteuliwa.

Baadhi ya majimbo yanahitaji wapiga kura kutoa sababu ya kuomba kura ya posta au sahihi ya shahidi au hati nyingine kabla ya kutoa kura, na kisha ofisi ya uchaguzi hushughulikia ombi hilo na kutuma kura kwa mpiga kura.

Majimbo ya Marekani huruhusu wapiga kura kufuatilia kura zao kwa njia ya mtandao. Majimbo 31 huruhusu mtu mwingine asiyekuwa mpiga kura kurudisha karatasi ya kupigia kura baada ya kuijaza kwa niaba ya mpiga kura, na majimbo mengi hutaka mwanafamilia tu ndio anaweza kurudisha kura hiyo, jambo ambalo linakosolewa na Republican.

Majimbo 28 huruhusu upigaji kura wa aina hiyo hata bila udhuru, na majimbo manane hutuma barua ya posta kwa wapigakura wote waliosajiliwa.

Kwa jumla, majimbo 47 yanatoa fursa za upigaji kura wa mapema. Alabama, Mississippi na New Hampshire hazitoi fursa ya upigaji kura wa ana kwa ana wa mapema wala hakuna sababu kwa kura ya posta.

Kura zote katika kinyang’anyiro cha urais wa Marekani huhesabiwa, na baadhi ya majimbo huzihesabu punde tu zinapoingia, huku nyingine, kama vile Michigan na Pennsylvania, huzuia kuhesabiwa kwa kura za posta kabla ya siku ya schaguzi.

Historia ya Kura hiyo

erdf
Maelezo ya picha,Rais Calvin Coolidge akipiga kura kwa njia ya barua ya posta mwaka 1924

Paul Groenke, profesa wa sayansi ya siasa katika chuo cha Reed nchini Marekani, anasema upigaji kura kwa njia ya posta umetumika kwa zaidi ya karne moja nchini humo, na ulitumiwa kwa mara ya kwanza na wanajeshi wakati wa Marekani wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

“Katika Vita vya wenyewe kwa wenyewe, Marekani ilijaribu kwa mara ya kwanza upigaji kura wa watu wengi wasioweza kufika kituoni wakati wa uchaguzi wa urais wa 1864 ambapo Abraham Lincoln alimshinda George McClellan – walipiga kura katika kambi na hospitali chini ya usimamizi wa makarani au maafisa wa serikali,” kulingana na gazeti la Time. .

Sheria zilizotungwa na Congress wakati wa Vita vya Pili vya Dunia kusaidia kupiga kura kwa wanajeshi walio ng’ambo bado zinatumika.

Hadi mwishoni mwa miaka ya 1970, upigaji kura kwa njia ya posta ulihitaji udhuru na ulitumiwa hasa na wanajeshi, Wamerika walio ng’ambo na wanafunzi waliokuwa mbali na nyumbani, kulingana na Groenke.

Groenke anasema majimbo kadhaa yalibadilisha sheria zao ili kuruhusu upigaji kura hata bila udhuru mwishoni mwa miaka ya 1970, na kuzindua enzi ya sasa ya upigaji kura wa barua ya posta.

Mwaka 1974, Washington lilikuwa jimbo la kwanza kuruhusu mpiga kura yeyote kuomba kura ya barua ya posta kwa sababu yoyote.

Katika miaka ya 1980, California iliruhusu wapiga kura kuomba kura wa barua ya psota kwa sababu tu walipendelea kupiga kura kwa njia hiyo.

Mwaka 2000, Oregon likawa jimbo la kwanza kufanya upigaji kura wote uwe kwa njia barua ya posta, kulingana na Groenke.

Katika uchaguzi wa 1972, takriban 95% ya wapiga kura walikwenda kwenye vituo vya kupigia kura na kupiga kura wenyewe, kulingana na Associated Press. Na 90% ya wapiga kura katika uchaguzi wa 1996 walipiga katika vituo.

Idadi ya watu waliopiga kura kabla ya siiku ya uchaguzi ilipanda karibu 70% katika uchaguzi wa 2020, ambapo idadi ya kura za posta ilizidi zile zilizopigwa siku ya uchaguzi, kwa mara ya kwanza.

Uskosoaji wa Trump

efdxc
Maelezo ya picha,Kisanduku cha kutia kura huko Leavenworth, Kansas

Trump kwa muda mrefu amekosoa aina zote za upigaji kura isipokuwa ile ya siku ya uchaguzi, na amesema kushindwa kwake katika uchaguzi dhidi ya Biden 2020 ni kwa sababu ya kura ya posta.

Bila ushahidi alidai kuwa aina hiyo ya upigaji kura inaweza kuathiri matokeo, kulingana na shirika la habari la Associated Press.

Alizungumzia kuhusu “udanganyifu na kughushi,” na mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka sabini na nane, alisema mara kwa mara bila ushahidi kwamba chama cha Democratic kiitumia upigaji kura wa posta ili kujaza masanduku ya kura wakati wa uchaguzi uliopita.

Mwaka 2022, Trump alisema, “Marekani ni kituko cha dunia linapokuja suala la uchaguzi.”

Uchunguzi katika jimbo la Georgia kuhusu madai ya ulaghai katika kura haukupata ushahidi wa kuunga mkono madai ya Trump.

Groenke anasema posta ni mfumo wa haki na usawa wa kutoa fursa kwa mtu yeyote ambaye ana shida kufikia masanduku ya kura katika siku ya uchaguzi, anasisitiza kuwa ni mfumo wa wazi kama vile kupiga kura ana kwa ana kituoni.

Licha ya kukosoa mfumo huo mara kwa mara, Trump mwenyewe alipiga kura yake huko Florida kwa barua ya posta wakati wa mchujo wa 2020 wa Republican.

Trump aliachana na kampeni yake dhidi ya upigaji kura kwa njia ya barua ya posta, baada ya kugundua kuwa kupinga kunaweza kumgharimu katika harakati zake za kurejea Ikulu ya White House, na akatangaza kuzindua mpango wa kuhimiza upigaji kura kwa njia ya posta, bila kutaja ukosoaji wake wa zamani.

Katika uchaguzi wa 2020, ambao ulifanyika huku kukiwa virusi vya Corona, wapiga kura walipendelea kupiga kura kwa njia ya posta, na mfumo huo ulipata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa Democratic, kulingana na Taasisi ya Utafiti ya Pew. Na 32% ya Warepublican pia walipiga kura kwa mfumo huo.

Groenke anasema “kihistoria, wapiga kura wengi ambao walipiga kura zao kwa njia ya posta walikuwa ni wafuasi wa Republican kwa sababu wapiga kura hawa walikuwa na umri mkubwa, elimu bora, na mapato ya juu, na watu wa aina hiyo mara nyingi huwa ni wa-Republican.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment