Ukiwa na moyo mzuri lazima pia uwe na mipaka.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Gharama mojawapo utakayoipata kwa kuwa mtu ambaye unajali sana watu ni kubeba Mizigo Yao kila wakati.

Kuna watu kwa sababu ya wema wao kwenye familia, wamejikuta hawapumziki katika majukumu ya kusaidia watu.

Kuna wengine wako ofisini na kwa sababu ya roho Yao nzuri, kila siku wanatumia rasilimali zao kusaidia watu.

Au haujawahi kuona mtu amezungukwa na watu ambao hawampi nafasi ya kupumzika, kila siku Rafiki zake wanamuomba yeye na kumpa mzigo tu.

Ndio maisha yalivyo: Ukiwa na moyo mzuri lazima pia uwe na mipaka.

Kuna wakati usipojiwekea mipaka utafanya vitu kwa kiwango cha kupitiliza.

Na baadaye itadhoofisha uwezo wako wa kufanya kabisa.

Usisahau, hakuna mtu atakuambia upumzike na uanze kujijali, ni wajibu wako.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment