Uhispania: Zaidi ya tisini waangamia katika mafuriko katika eneo la Valencia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa, usiku wa Jumanne Oktoba 29 kuamkia Jumatano Oktoba 30, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 95 kusini-mashariki mwa Uhispania, ikiwa ni pamoja na 92 ​​katika eneo la Valencia pekee, Waziri wa Sera ya Nchi, Angel Victor Torres amesma. Watu wengine wawili walipoteza maisha katika eneo jirani la Castile-La Mancha na mmoja huko Andalusia, kulingana na ripoti hii ya muda.

Mwanamume akitembea katika mitaa ya Valencia iliyokmbwa na mafuriko, Uhispania, Jumatano Oktoba 30, 2024.
Mwanamume akitembea katika mitaa ya Valencia iliyokmbwa na mafuriko, Uhispania, Jumatano Oktoba 30, 2024. © Alberto Sai / AP

Waokoaji walimaliza kukagua maeneo yenye watu wengi jioni, Jumatano, Oktoba 30. Idadi hiyo, ya juu zaidi tangu mafuriko ambayo yalisababisha vifo vya watu 300 mnamo Oktoba 1973 nchini Uhispania, “itaongezeka kwa sababu tunadhania kwamba kuna wengi waliotoeka”, ameonya Waziri wa Sera ya Nchi Jumatano jioni, Angel Victor Torres. Mvua iliacha kunyesha katika eneo hilo siku ya Jumatano. Lakini kunyesha kwa mvua siku iliyotangulia na usik kulitumbukiza maeneo mengi katika machafuko, ambayo yalikatishwa mbali na ulimwengu huku makumi ya maelfu ya wakaazi wakiwa bado hawana umeme.

Serikali ya Uhispania imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Alhamisi, Oktoba 31, siku ambayo Waziri Mkuu Pedro Sánchez anapanga kuzuru eneo hilo. Mfalme wa Uhispania Felipe VI amesema “amefadhaika” kwenye mtandao wa kijamii wa X, akisema atatoa msaada unaohitajika kwa ndugu wa wahanga.

Kulingana na huduma za dharura katika ujumbe ulioandikwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, mji wa Valencia ndio ulioathirika zaidi huku watu 92 wakifariki dunia katika mji huo pekee.

Miili mingine miwili imepatikana katika eneo jirani la Castilla-La Mancha huku mtu mmoja akifariki katika mji wa kusini wa Malaga.

Dazeni kadhaa za watu bado hawajulikani walipo huku maeneo kadhaa yakiwa hayawezi kufikiwa kutokana na mafuriko hayo.

Waokoaji wamepata wakati mgumu kuyafikia maeneo yaliyokumbwa na mkasa huo kutokana na mafuriko au njia zilizofungwa.

Kutokana na hilo, sehemu kubwa ya usaidizi mjini Valencia unafanywa kwa kutumia ndege aina ya helikopta. Watu wengi wamenasa majumbani mwao, maofisini au madukani na wametoa miito ya kusaidiwa, kupitia mitandao ya kijamii.

Watu wengi pia wanadaiwa kupiga simu katika vyombo vya habari kwa kuwa hawakuweza kuwasiliana na marafiki na wapendwa wao.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa nchini humo limesema mvua zitaendelea hadi siku ya Jumapili. Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez ameahidi msaada wa haraka kwa walioathirika na mkasa huo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment