Botswana: Rais anayemaliza muda wake apingwa na mtangulizi wake katikati ya uchaguzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Raia wa Botswana wanapiga kura leo Jumatano Oktoba 30, 2024 kumchaguwa rais wao  na wabunge. Wagombea wanne, akiwemo rais anayemaliza muda wake, wanachuana  katika uchaguzi huu. Lakini wakati wa kampeni, rais anayemaliza muda wake, Mokgweetsi Masisi, hasa alilazimika kukabiliana na mtangulizi wake Ian Khama, ambaye alirejea kutoka uhamishoni, lakini hawezi tena kugombea katika uchaguzi huu.

Mwanamke na mtoto wakipita mbele ya bango la uchaguzi la Rais wa Chama cha Kidemokrasia cha Botswana Mokgweetsi Masisi huko Gaborone, Botswana, Jumanne, Oktoba 29, 2024.
Mwanamke na mtoto wakipita mbele ya bango la uchaguzi la Rais wa Chama cha Kidemokrasia cha Botswana Mokgweetsi Masisi huko Gaborone, Botswana, Jumanne, Oktoba 29, 2024. © Themba Hadebe / AP

Wawili hao ambao ni washirika wa muda mrefu sasa ni wapinzani. Aliporejea kutoka uhamishoni wiki sita zilizopita, rais wa zamani, Ian Khama, aliongoza kampeni ya kumkashifu Mokgweetsi Masisi, yule aliyempenda zaidi na kumchaguwa kumrithi mwaka wa 2018.

Licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo, mkuu wa Chama cha Kidemokrasia cha Botswana, chama kilicho madarakani tangu uhuru mnamo mwaka 1966, rais mwenye ufasaha hata hivyo anawasilisha tathmini tofauti: ukuaji wa polepole, kupungua kwa mahitaji ya almasi, rasilimali ya msingi ya nchi, Ukosefu wa ajira ni zaidi ya 25% mwaka huu.

Shutuma kali kutoka kwa mtangulizi wake

Ian Khama, ambaye hawezi kugombea katika uchaguzi wa urais kwa sababu tayari amehudumu kwa mihula miwili kati ya 2008 na 2018, pia alimshutumu mkuu wa nchi kwa “kudhoofisha demokrasia, kuingilia kati mfumo wa mahakama . “

Mgawanyiko ndani ya upinzani, pamoja na vyama vitatu kuteuwa wagombea, hata hivyo unaweza kumpa nafasi kubwa Mokgweetsi Masisi kushinda uchaguzi. Mokgweetsi Masisi alichaguliwa kwa asilimia 52 ya kura mwaka 2018 na alitangaza wakati wa mdahalo uliopita “tutaendelea na sera zetu ambazo zinalenga kuweka fedha zaidi mikononi mwa raia wa nchi hii.”

Botswana ni nchi isiyo na bahari katikati mwa Afrika kusini, lakini hata hivyo imestawi, na inasifika kwa uzalishaji wake wa almasi na wakati huo huo mojawapo ya mataifa yasiyo na usawa duniani katika ugawaji upya wa mali.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment