Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Unataka Kupona MAUMIVU ya MOYO?…

i. Maumivu yanayotokana na kupoteza
iii. Kukataliwa
iv. Kufeli
v. Upweke
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina Tatu
– Kukataliwa
Watu wengi sana wamejikataa baada ya kukataliwa na watu waliodhania walitakiwa kuwathamini.
Kuna watu ambao tangu walipokataliwa na baba yao wakati mama yao alipopata ujauzito, hawajawahi kufurahia maisha tena.
Kuna wengine walijaribu kumtafuta baba yao ila baada ya kukutana naye aliwakataa, hawajaweza kupona tena.
Wapo ambao walikataliwa na watu waliowapenda sana, tangu hilo liwatokee limeiba furaha yao.
Wale walioachwa wakati wenyewe bado wanapenda, wameishia kila wakati kujiuliza wamepungukiwa na nini katika maisha yao.
Changamoto kubwa ya maumivu ya kukataliwa ni kuwa, yanaweza kukupelekea na wewe uanze kujikataa pia.
Unaweza kuanza kuacha kujithamini na ujione kuwa haufai tena.
Kuna watu ambao waliamini kuwa wana kipaji kizuri, ila walipoenda kutafuta fursa walikataliwa na tangu wakati huo kisaikolojia hawajaweza kuwa sawa.
Wengine waliamini wana wazo zuri au hata uwezo mzuri wa kufanya kazi fulani, ila tangu wakataliwe hawajawahi kurudi kuwa kawaida tena.
Usisahau kuwa, wale ambao wameendelea kung’ang’ania mahali ambapo walitakiwa wapaachie, ndio hasa hupata maumivu zaidi ndani ya mioyo yao.
Maumivu ya kukataliwa yamewafanya watu wengi wajione hawafai tena waone kuwa dunia haiwahitaji kabisa.
Usiwe mmoja wapo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.