Afya: Kisa cha kwanza cha lahaja mpya ya Mpox chagunduliwa nchini Uingereza

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Shirika la Usalama wa Afya la Uingereza limetangaza siku ya Jumatano Oktoba 30 kwamba limegundua kisa cha kwanza cha maambukizo ya aina mpya ya virusi vya Mpox, ambavyo chimbuko lake kubwa ni kutoka barani Afrika. “Shirika la Usalama la Afya la Uingereza (UKHSA) limegundua kisa kimoja cha binadamu kilichothibitishwa cha clade 1b Mpox,” shirika hilo limendika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, likibainisha kuwa “hatari kwa raia  bado ni ndogo”.

Chanjo ya Mpox.
Chanjo ya Mpox. Getty Images – MicroStockHub

Shirika hilo limebaini kwamba “kisa kimoja cha binadamu kilichothibitishwa cha clade 1b mpox” kimegunduliwa London na kinamhusu mtu “ambaye alikuwa amesafiri hivi majuzi katika nchi za Afrika” zilizoathiriwa na lahaja hii.

Mamlaka za afya zinabainisha katika taarifa kwa vyombo vya habari kwamba “hatari kwa raia bado ni ndogo”.

Mgonjwa aliyeambukizwa lahaja hii mpya aligunduliwa nchini Ujerumani zaidi ya wiki moja iliyopita. Wagonjwa wengine waliripotiwa nchini Sweden na nchi kadhaa za Asia.

“Watu wote waliotangamana na mgonjwa huyu watatakiwa kufanya vipimo na chanjo ikiwa ni lazima na watashauriwa juu ya huduma ya ziada inayotolewa ikiwa wana dalili au ikiwa vipimo vitaonyesha dadili yoyote ya ugonjwa huo,” llimeongeza shirika la usalama, British Health Authority ( UKHSA).

Shirika hili limesema linafanya kazi “kwa ushirikiano wa karibu” na Huduma ya Afya ya Umma ya Uingereza (NHS) “na washirika wa kitaaluma kuamua dalili za ugonjwa huu na kutathmini zaidi hatari kwa afya ya binadamu”.

Mpox ambayo hapo awali iliitwa monkeypox, ni ugonjwa wa virusi ambao huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu lakini pia hupitishwa kati ya binadamu, na kusababisha homa, maumivu ya misuli na vidonda vya ngozi.

Kwa miezi kadhaa,mlipuko mpya umeathiri Afrika, na takwimu za juu zaidi za maambukizi zinapatikana nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi na Nigeria.

Magonjwa mawili ya mlipuko yanayotokea kwa wakati mmoja yanatokea, moja yakisababishwa na kundi la 1 katika Afrika ya Kati, yakiathiri zaidi watoto, na jingine la aina mpya ya clade 1b, ambayo huathiri watu wazima katika eneo lingine, mashariki mwa DRC, na katika nchi jirani.

Kampeni ya chanjo ilizinduliwa mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba nchini DRC, nchi iliyoathiriwa zaidi na virusi hivi duniani.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment