Watu kumi na moja wafariki katika maandamano ya baada ya uchaguzi nchini Msumbiji

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Polisi nchini Msumbiji wamewauwa takriban watu 11 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 50 wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi, shirika la kimataifa la Human Rights Watch (HRW) imesema siku ya Jumanne Oktoba 28, 2024.

Wapiga kura nchini Msumbiji wakipiga kura.
Wapiga kura nchini Msumbiji wakipiga kura. PATRICK MEINHARDT / AFP

Maandamano yameitikisa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika tangu chama cha FRELIMO, kilichoko madarakani tangu mwaka 1975, kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Oktoba 9. Mamia ya wafuasi wa upinzani waliingia mitaani wiki jana, na kusababisha makabiliano na polisi wa kutuliza ghasia.

“Vikosi vya usalama vya Msumbiji viliua watu wasiopungua 11,” HRW imesema katika taarifa, na kuongeza kuwa “zaidi ya watu 50 walijeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi” Oktoba 24 na 25. Maafisa wanane wa polisi pia walijeruhiwa, kulingana na HRW ambayo inasema hivyo imehoji watu 22, wakiwemo waathiriwa na mashahidi, madaktari, waandishi wa habari, viongozi wa serikali na mashirika ya kiraia.

“Watu wengi, ikiwa ni pamoja na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, walivuta gesi ya kutoa machozi ambayo polisi walitumia kiholela katika maeneo ya makazi,” shirika la haki za binadamu linaandika.

Daktari ameiiambia HRW kwamba amewatibu makumi ya watu waliojeruhiwa, akiwemo mtu mmoja ambaye alikuwa na “risasi kwenye uti wa mgongo”. Allan Ngari, HUman Right Watch katika kada ya Afrika, anabaini kwamba uchunguzi katika matukio haya unapaswa kufanywa na mamlaka ya Msumbiji.

Shirika lisilo la kiserikali la Msumbiji, Kituo cha Demokrasia na Haki za Kibinadamu (CDD), pia limehesabu takriban watu 11 waliouawa katika ghasia za siku ya Jumapili, wakiwemo sita katika jimbo la Nampula (kaskazini). Zaidi ya watu 450, wakiwemo 370 huko Maputo, walikamatwa kando ya maandamano haya, CDD iilibainisha siku ya Jumapili, ikisema kuwa angalau waandamanaji 85 waliachiliwa.

Polisi wa Msumbiji hawakutoa maoni yoyote kuhusu ripoti za CDD na HRW. Siku ya Ijumaa, msemaji wa polisi nchini Msumbiji aliripoti kwa vyombo vya habari majeruhi 20 lakini hakuna vifo. Siku ya Alhamisi iliyopita, Tume ya uchaguzi (CNE) ilitangaza ushindi wa wazi kwa chama tawala, FRELIMO, kwa karibu asilimia 71 ya kura za mgombea wake wa urais, Daniel Chapo, na viti 195 vya wabunge.

Chama cha Podemos, ambacho kilikuja kuwa chama kikuu cha upinzani nchini Msumbiji kufuatia uchaguzi wa Oktoba 9, kiliwasilisha rufaa mbele ya mahakama ya juu zaidi ya nchi hiyo kuomba kuhesabiwa upya kwa kura, kulingana na duru za kuaminika. Podemos, ikiongozwa na kiongozi mpya wa upinzani, Venancio Mondlane, ambaye alishika nafasi ya pili katika uchaguzi wa urais kwa asilimia 20 ya kura, inataka hesabu hiyo ifanyike upya, ikisema imeona dosari nyingi wakati wa uchaguzi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment