DRC: Karibu mtu mmoja kati ya wanne wako katika njaa kali, ripoti ya Umoja wa Mataifa yaonya

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Takriban robo ya wakaazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mamilioni ya watu wameyakimbia makazi yao, wako katika hali ya njaa kali, Umoja wa Mataifa unaonya katika ripoti iliyochapishwa siku ya Jumatatu.

Wakongo waliokimbia makazi yao wanatafuta na kuandaa chakula katika kambi ya wakimbizi huko Kanyaruchinya, DRC, Desemba 2022.
Wakongo waliokimbia makazi yao wanatafuta na kuandaa chakula katika kambi ya wakimbizi huko Kanyaruchinya, DRC, Desemba 2022. © GUERCHOM NDEBO / AFP

Hii inahusu baadhi ya watu milioni 25.6 ambao maisha au njia zao za maisha “zinatishiwa kwa muda mfupi kutokana na ukosefu wa chakula cha kutosha”. Hii ndiyo maana ya “uhaba mkubwa wa chakula” kwa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwao, zaidi ya watu milioni tatu wako katika hali inayochukuliwa kuwa “hatari”, kulingana na ripoti ya Mfumo wa Uainishaji wa Usalama wa Chakula (IPC), unaotolewa na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

“Uhaba mkubwa wa chakula unatokana na mambo kadhaa ya pamoja, ikiwa ni pamoja na migogoro, kupanda kwa bei ya chakula na gharama za usafiri, na athari za muda mrefu za magonjwa mbalimbali ya milipuko kama vile Surua, KipindupinduMalaria au ugojwa wa hivi karibuni wa Mpox,” ripoti hiyo inasema.

Hali inayoathiri nchi nzima

Mikoa yote ya DRC inakabiliwa na hali hii, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Kinshasa. Lakini takwimu zinatisha zaidi katika maeneo yenye migogoro. Kivu Kaskazini, Ituri, Kivu Kusini… Mikoa ambayo mgogoro wa kibinadamu umekuwa karibu kudumu kwa miaka thelathini, lakini ulizidi kuwa mbaya zaidi tangu mzozo unaoendelea kwa kuibuka tena kwa waasi wa M23.

Idadi ya watu kuyahama makazi yao ni kubwa. Kwa mujibu wa FAO, katika mikoa hiyo, asilimia 25 ya wafugaji walipoteza mifugo na asilimia 35 ya kaya hazikuwa na uwezo wa kulima zehemu zao za ardhi.

Sababu za kimuundo

Kinachoongezwa kwa hili ni sababu za kimuundo: ukosefu wa miundombinu, ukosefu wa maji na “ukosefu wa wazi wa barabara bora”, ambayo inakatisha tamaa uzalishaji wa kilimo, ambao ni vigumu sana kuuza kwenye masoko. Kwa hiyo, kutokana na matatizo haya ya muda mrefu – ugonjwa, mafuriko au mavuno duni – sehemu ya raia hujikuta haraka katika mgogoro au kaika hali ya dharura.

Makadirio ya IPC yanaonyesha kuwa uhaba wa chakula katika ngazi ya kitaifa unatarajiwa kuendelea katika mwaka 2025 katika kiwango sawa na mwaka 2024, sawa na kile cha mwaka 2023. Hata hivyo, FAO ina wasiwasi juu ya kuzorota kwa hali ya usalama kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) huko Kivu Kusini mnamo Juni 30.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment