Afrika Leo Afrika-30-10-2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja

Muhtasari

  • Afrika Kusini kumnyang’anya Malkia wa urembo utambulisho wake
  • Trump amjibu Biden bila kupoteza muda kwa neno alilotumia ‘takataka’
  • Biden afafanua matumizi ya neno ‘takataka’ huku wafuasi wa Republican wakimkosoa
  • Biden: Ikiwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wataingia Ukraine, Ukraine inapaswa kuwashambulia
  • RSF, washirika wake, walifanya unyanyasaji wa kingono Sudan, ujumbe wa Umoja wa Mataifa unasema
  • Mshindi wa taji la Urembo nchini Rwanda akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa
  • Ufaransa yaiunga mkono Morocco katika mzozo kuhusu Sahara Magharibi
  • Wanaharakati kufika mahakama za juu kupinga Tamisemi kusimamia uchaguzi
  • Marekani yasema shambulizi la anga la Israel ‘ni la kutisha’

Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Jioni ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 30/10/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.

Marekani yaionya Israel kuhusu msaada wa Gaza huku muda wa makataa ukiyoyoma

.

Israel inapaswa kushughulikia mara moja “hali mbaya ya kibinadamu” huko Gaza, mjumbe wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ameonya, wakati tarehe ya mwisho inakaribia ya kuongeza upatikanaji wa misaada au ikabiliane na kupunguzwa kwa usaidizi wa kijeshi wa Marekani.

“Maneno ya Israel lazima yalinganishwe na hatua zinazochukuliwa,” Linda Thomas-Greenfield alisema. “Kwa sasa, hilo halifanyiki.”

Marekani imempa mshirika wake hadi Novemba 12 “kuongeza” msaada wote, na angalau malori 350 yawe yanaingia Gaza kila siku.

Lakini Umoja wa Mataifa unasema ni 10% tu kwa wastani ya idadi hiyo imevuka mpaka kila siku tangu wakati huo.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Danny Danon, alisema inafanya “kila iwezalo na zaidi ya majukumu yake ya kibinadamu” na akailaumu Hamas.

Bw Danon pia alikataa ukosoaji wa kimataifa wa uamuzi wa bunge la Israel kupiga marufuku shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi wa Kipalestina (Unrwa) kufanya kazi nchini Israel.

Washirika wa Israel wameonya kwamba Unrwa ina jukumu muhimu katika kupeleka misaada ya kibinadamu huko Gaza, ambako ni shirika kubwa zaidi la kibinadamu duniani.

Afrika Kusini kumnyang’anya Malkia wa urembo utambulisho wake

.

Malkia wa urembo Chidimma Adetshina, ambaye amekuwa katikati ya mzozo tatanishi wa utaifa, atanyang’anywa utambulisho wake wa Afrika Kusini na hati za kusafiria.

Idara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ilianza kuchunguza kesi yake baada ya kufika fainali katika shindano la ‘Miss South Africa’, lakini alikosolewa huku watu wakihoji ikiwa anastahili kushiriki kwa sababu mama yake ana asili ya Msumbiji na baba yake ni Mnigeria.

Alijiondoa katika shindano hilo mwezi Agosti baada ya idara hiyo kutangaza kuwa mamake huenda alifanya “wizi wa utambulisho” ili kuwa raia wa Afrika Kusini.

Bi Adetshina, mwanafunzi wa sheria, alishinda Miss Universe Nigeria baada ya kualikwa kushiriki na waandaaji.

Trump amjibu Biden bila kupoteza muda kwa neno alilotumia ‘takataka’

.

Trump amejua kuhusu neno alilotumia Joe Biden ‘takataka’ alipokuwa jukwaani huko Allentown, Pennsylvania, na Seneta Marco Rubio mara moja akarejelea matamshi ya Hillary Clinton ya 2016 akiwaita baadhi ya wafuasi wa Trump “wenye kusikitisha”.

“Takataka nadhani ni baya zaidi?” Trump alisema, kabla ya kuongeza, “Lakini tafadhali msameheni, kwani hajui alichosema”.

Biden amekanusha kwamba aliwataja wafuasi wa Trump kwa pamoja, na kusema alikuwa anazungumza kuhusu mcheshi Tony Hinchcliffe, ambaye alitumia mkutano wa Trump kutaja Puerto Rico kama “kisiwa kinachoelea cha taka”.

Trump baadaye aliandika tena kwenye tovuti yake ya Truth Social, akimshutumu Harris kwa “kuendesha kampeni ya chuki”.

Biden afafanua matumizi ya neno ‘takataka’ huku wafuasi wa Republican wakimkosoa

.

Nianze kwa kukujuza taarifa zinazoendelea Marekani. Rais Joe Biden amezua ghadhabu kwa wafuasi wa Republican katika saa za hivi karibuni.

Ilianza muda mfupi baada ya Kamala Harris kumaliza kutoa hotuba yake kubwa ya kampeni huko Washington DC.

Akiongea kwenye hafla kupitia Zoom na wapiga kura hapo awali, Biden alizungumza juu ya watu wa Puerto Rico: “Ni watu wazuri na wenye heshima.”

Kisha alionekana kusema: “Takataka pekee ninayoiona ikielea huko nje ni wafuasi wake … Walatino anaowatumia vibaya, haikubaliki.”

Warepublican wanasema Biden aliwataja wafuasi wote wa Trump kama “takataka” – huku Biden na Ikulu ya White House wakisema alikuwa akimrejelea haswa mcheshi aliyeshambulia Puerto Rico kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump, na “maneno ya chuki” dhidi ya kisiwa hicho.

Wakati Ikulu ya White House ilipotoa nakala ya maoni ya Biden, walijumuisha neno “msaidizi” likiwa kwenye apostrofi – ambayo ingeashiria rais alikuwa anazungumza juu ya mtu maalum badala ya kundi kwa jumla.

Ukraine kusajili wanajeshi wengine 160,000, Urusi yasonga mbele eneo la mashariki

Kifaru

Ukraine inapanga kusajili wanajeshi wengine 160,000 katika jeshi lake huku Urusi ikipata mafanikio katika eneo la mashariki.

Urusi imekuwa ikisonga mbele katika eneo la mashariki la Donetsk na Jumanne ilisema kuwa imeuteka kikamilifu mji wa wenye shughuli za uchimbaji madini wa Selydove.

Pia hatua hii inakuja huku kukiwa na ripoti kwamba idadi kadhaa ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wametumwa Urusi.

Jeshi la Ukraine limekuwa chini ya shinikizo kubwa siku za hivi karibuni, kwa sehemu kutokana na nguvu kazi kubwa ya Urusi na rasilimali nyingi zaidi.

“Kuna mipango ya kuwaita zaidi ya watu 160,000,” katibu wa Baraza la Usalama la Taifa la Ukraine, Oleksandr Lytvynenko, aliliambia bunge siku ya Jumanne.

Shirika la habari la AFP linaripoti kuwa usajili huo utafanyika kwa muda wa miezi mitatu.

Pentagon inakadiria kuwa takribani wanajeshi 10,000 wa Korea Kaskazini wametumwa kutoa mafunzo mashariki mwa Urusi.

Marekani ilisema Jumanne “idadi ndogo” ya wanajeshi wa Korea Kaskazini wametumwa Kursk.

Maelfu kadhaa zaidi wanaelekea huko, ilisema. Korea Kusini imedai kuwa wanajeshi hao wanapewa mafunzo katika maeneo mbalimbali, huku wengi wao wakiwa wamevalia sare za Kirusi ili kujificha.

Afisa wa ngazi ya juu wa serikali alisema wanaamini hadi wanajeshi 11,000 tayari wametumwa Urusi, na takribani 3,000 magharibi mwa nchi hiyo.

Wiki iliyopita Rais Vladmir Putin alikana taarifa kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wamewasili nchini Urusi kufuatia ripoti kwamba Pyongyang inajiandaa kutuma maelfu ya wanajeshi wake kusaidia mshirika wake.

China yatangaza mafanikio wakati wanaanga wake wakifikia anga za juu

Chombo

Chombo cha anga za juu cha China kikiwa na wafanyakazi watatu akiwemo mhandisi wa anga wa kwanza mwanamke nchini humo kimetia nanga baada ya safari ya zaidi ya saa sita.

Wafanyakazi watatumia kituo cha anga za juu kwa muda wa miezi sita kufanya majaribio na kufanya matembezi ya anga wakati Beijing inakusanya uzoefu kwa ajili ya dhamira yake ya kumweka mtu kwenye Mwezi ifikapo 2030.

Beijing ilitangaza urushaji wa Shenzhou 19 kuwa “mafanikio”, ni moja ya matukio 100 ambayo China imepanga katika mwaka wa rekodi wa uchunguzi wa anga inapojaribu kumshinda mpinzani wake, Marekani.

BBC ilipewa nafasi ya kufika kwenye kituo cha kurushia Satellite cha Jiuquan huko Gansu na tulikuwa umbali wa zaidi ya kilomita moja wakati chombo hicho kilipolipuka.

Miale ya moto ilitoka kwenye kirusha roketi ilipopaa angani, ikimulika Jangwa la Gobi kwa kishindo.

Mamia ya watu walijipanga barabarani, wakipunga mkono na kuwashangilia wanaanga hao.

Katika kituo cha anga za juu cha Tiangong, wafanyakazi wa Shenzhou 19 walikutana na wanaanga wengine watatu ambao wanasimamia Shenzhou 18 na watarejea duniani tarehe 4 Novemba.

Miaka miwili tu iliyopita, Rais Xi Jinping alitangaza kwamba “kuchunguza anga kubwa, kuendeleza sekta ya anga na kujenga China katika nguvu ya anga ni ndoto yetu ya milele”.

Lakini wengine huko Washington wanaona matarajio ya nchi na maendeleo ya haraka kama tishio.

Mapema mwaka huu, mkuu wa Nasa, Bill Nelson alisema Marekani na China “ziko katika mbio” za kurejea Mwezini.

Aliwaambia wabunge kwamba anaamini mpango wa China wa anga za juu wa kiraia pia ulikuwa mpango wa kijeshi.

Biden: Ikiwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wataingia Ukraine, Ukraine inapaswa kuwashambulia

Jeshi la Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa maoni yake kuhusu ripoti za wanajeshi wa Korea Kaskazini kuwasili katika eneo la Kursk nchini Urusi.

Alisema ana wasiwasi na ripoti hizo. Alipoulizwa ikiwa Ukraine inapaswa kujibu, Biden alijibu: “Ikiwa watavuka mpaka na kuingia Ukraine, basi ndio washambuliwe.”

Vikosi vya RSF, washirika wake, walifanya unyanyasaji wa kingono Sudan, ujumbe wa Umoja wa Mataifa unasema

Mzozo unaoongezeka katika jimbo la Gezira nchini Sudan umewalazimu raia kukimbia

Vikosi vya wanamgambo wa Sudan (RSF) na washirika wake wamefanya viwango vya “kushangaza” vya unyanyasaji wa kingono, kuwabaka raia huku wanajeshi wakisonga mbele na kuwateka nyara baadhi ya wanawake kama watumwa wa ngono wakati wa vita vilivyodumu zaidi ya miezi 18, ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne, Reuters imeripoti.

Waathirika wameanzia kati ya miaka minane hadi 75, ilisema ripoti ya ujumbe wa uchunguzi wa Umoja wa Mataifa, huku unyanyasaji mwingi wa kingono ukifanywa na RSF na wanamgambo washirika wa Kiarabu katika jaribio la kuwatisha na kuwaadhibu watu kwa kudhaniwa kuwa na uhusiano na maadui.

“Kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia ambao tumeandika nchini Sudan ni cha kushangaza,” mwenyekiti wa misheni Mohamed Chande Othman alisema katika taarifa iliyoambatana na ripoti ya kurasa 80 iliyojikita katika mahojiano na waathiriwa, familia na mashahidi.

Ripoti hiyo ilirejea uchunguzi wa Reuters na makundi ya haki za binadamu kuhusu unyanyasaji mkubwa wa kingono katika mzozo huo. RSF, ambayo inapambana na jeshi la Sudan, haikujibu mara moja ombi la kutoa maoni. Hapo awali imesema itachunguza tuhuma na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

Mshindi wa taji la Urembo nchini Rwanda akamatwa kwa kuendesha gari akiwa amelewa

Divine Muheto

Polisi nchini Rwanda wamemkamata mshindi wa taji la taifa la urembo kwa “kurudia” “kuendesha gari akiwa amekunywa pombe kupita kiasi” na kusababisha uharibifu wa miundombinu.

Divine Muheto hana leseni ya kuendesha gari na alitoroka eneo la ajali baada ya kugonga miundombinu, polisi walisema katika taarifa.

Bi Muheto hajajibu hadharani madai hayo. Bi Muheto, 21, alipata umaarufu aliposhinda shindano la urembo la Miss Rwanda mnamo 2022, kabla ya serikali kusitisha shindano hilo baada ya tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya waandaaji.

Polisi wametangaza kukamatwa kwake leo, siku chache baada ya tetesi kuwa mrembo huyo alihusika katika ajali ya barabarani na baadaye kukamatwa.

Adhabu ya kuendesha ukiwa umekunywa ni faini ya faranga 150,000 za Rwanda (dola 110), na siku tano rumande.

Katika miaka ya hivi karibuni maelfu ya watu walikamatwa kwa kosa hili huku polisi wakitekeleza sheria hii. Mnamo 2022 mbunge alijiuzulu na kuomba msamaha kwa kuendesha gari akiwa amelewa.

Utekelezaji mkali wa sheria za trafiki umepunguza kwa kiasi kikubwa ajali mbaya za barabarani nchini Rwanda, serikali imesema.

Katika taarifa yake, polisi walisema kuwa kesi ya Bi Muheto ilifikishwa katika ofisi ya mashtaka.

Ufaransa yaiunga mkono Morocco katika mzozo kuhusu Sahara Magharibi

Maelfu ya watu wa Sahrawi wanaishi katika kambi za wakimbizi nchini Algeria

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameliambia bunge la Morocco kwamba anaamini Sahara Magharibi inapaswa kuwa chini ya mamlaka ya Morocco, na ameahidi kuwekeza fedha za Ufaransa huko.

Sahara Magharibi ni eneo la pwani ya kaskazini-magharibi mwa Afrika ambalo limekuwa na mzozo wa miongo kadhaa.

Wakati fulani lilikuwa koloni la Uhispania, na sasa linadhibitiwa zaidi na Morocco na kwa kiasi fulani na Polisario Front inayoungwa mkono na Algeria, ambayo inasema inawakilisha watu asilia wa Sahrawi na inataka taifa huru.

Ufaransa ilikuwa nchi yenye nguvu ya kikoloni katika Morocco na Algeria. Inaungana na mataifa mengine ikiwemo Uhispania, Marekani na Israel kuunga mkono mpango wa Morocco.

Wabunge walisimama na kumpongeza Macron Jumanne aliposema, “kwa Ufaransa, eneo hili la sasa na la siku zijazo liko chini ya mamlaka ya Morocco”.

Maoni yake siku ya Jumanne huko Rabat yanalingana na matamshi ya mshangao aliyotoa kwa mara ya kwanza mnamo Julai. Akiashiria mabadiliko katika msimamo wa muda mrefu wa Ufaransa kuhusu mpango wa Morocco wa kuipa Sahara Magharibi uhuru wa kujitawala chini ya mamlaka ya Morocco, rais wa Ufaransa alisema huo ndio “msingi pekee” wa suluhu la haki na la kudumu la kisiasa.

Uungaji mkono wa Ufaransa kwa madai ya eneo la Morocco uliikasirisha Algeria, ambayo ilijibu habari hiyo kwa kumuondoa balozi wake huko Paris. Algiers inachukulia uwepo wa Morocco huko kama uvamizi haramu.

Wachambuzi wanasema uamuzi wa Ufaransa kuunga mkono madai ya Morocco ni jaribio la kurekebisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, ambao ulikuwa umedorora baada ya Rabat kushutumiwa kwa kujaribu kufanya ujasusi dhidi ya Rais Macron na Ufaransa ikaimarisha vikwazo vya visa kwa raia wa Morocco wanaozuru nchni humo.

Uhusiano kati ya Morocco na Algeria umekuwa wa wasiwasi hasa katika miaka ya hivi karibuni, na Algiers ilitangaza mwaka 2021 kwamba ilikuwa imekata uhusiano wa kidiplomasia na jirani yake wa magharibi.

Wanaharakati kufika mahakama za juu kupinga Tamisemi kusimamia uchaguzi

Wapiga kura

Wakili na wanaharakati nchini Tanzania waliokuwa wakipinga Waziri kutunga kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa na kuusimamia uchaguzi huo wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama uliotolewa jana na kuhalalisha kanuni za uchaguzi zilizotungwa na Waziri na kuruhusu Tamisemi kuendelea kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Wakili Jebra Kambole akiwa na wanaharakati Bob Wangwe, Dr Ananilea Nkya na Bubelwa Kaiza walifungua shauri mahakamani wakihoji mamlaka ya Waziri wa Tamisemi kutunga kanuni za uchaguzi huo na pia kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa serikali za mitaa. Walitaka majukumu hayo yapewe Tume Huru ya Uchaguzi.

“Tutakwenda mahakama ya riufaa ambayo ndiyo ya mwisho. Na yenyewe ikiwa itafanya maamuzi ya ndivyo sivyo, tutaifikia mahakama ya Afrika ya watu na binnadamu au tume ya haki za binadamu ya Afrika tunaamini huko tutapata haki kama tulivyoppata haki ya kesi ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi, mgombea binafsi ya mtikila, au kesi ya kupingwa kwa matokeo ya urais” amesema Kambole

Kamboleanasema msingi wa moja ya hoja zao ulikuwa ni haki ya asili juu ya nafasi ya Waziri wa Tamisemi na wajibu wake katika kusimamia uchaguzi

“Mtu anapokuwa anafanya maamuzi au anasimamia jambo hapaswi kuwa na maslahi na jambo hilo, lakini pia, huyo mtu huyo anayesimamia uchaguzi pamoja na kutokuwa na maslahi hawezikuwa na maamuzi kwenye kesi ambayo inamuhusu” amesema Kambole

Mwanaharakati wa haki za binadamu Dr Ananilea Nkya ameyataja maamuzi ya mahakama kubariki nnafasi ya Tamisemi katika uchaguzi huo kama kupuuzwa kwa sauti za wananchi

“Kile kilio cha wananchi, kile kilio cha raia, kwamba sisi raia tunataka chaguzi ziwe huru ina maana hakikusikilizwa, ina maana kimepokwa” amesema Nkya

Chama cha upinzani ACT wazalendo wamesema hawakupendezwa na uamuzi huo wa mahakama ambao unapunguza imani juu ya mchakazo mzima wa uchaguzi.

“Hatuuamini kwasababu upo chini ya Tamisemi, ambayo ipo chini ya CCM. Na hatuwezi kusema hatushiriki kwasababu itakuwa tunawaachia CCM ushindi bila kupingwa. Kwahivyo, manyago yatakuwepo kwasababu ndio siasa za CCM lakini na sisi tutaenda nazo hivyo hivyo,” amesema Ruqayya Nassir ni Naibu Katibu Mkuu Ngome ya Vijana ACT Wazalendo

Pamoja na uamuzi wa mahakama kuthibitishwa mamlaka ya Tamisemi katika kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa Dr Nkya anasema bado atakwenda kupiga kura

“Mimi ni mpiga kura, na mimi huwa siamini katika kuacha kupiga kura, nitakwenda kwenye sanduku la kupiga kura, nitapiga kura yangu. Kwasbabu unapokuwa hauna uongozi bora kwanzia ngazi ya mtaa, unapoteza si tu mabilioni ya fedha unaweza wananchi katika hali ya hofu, kwasababu hawana viongozi waliowachagua wao kupitia sanduku huru la kura” amesema Nkya

Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi wa serikali za mtaa tarehe 27 Novemba huku wapiga kura wakitarajiwa kuchagua Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Wilaya.

Nafasi zingine zinazotarajiwa kugombaniwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo, Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji.

Marekani yasema shambulizi la anga la Israel ‘ni la kutisha’

Athari za mashambulizi

Takribani watu 93 wameuawa au hawajulikani walipo baada ya mashambulizi ya anga ya Israel katika mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas imesema, katika shambulio ambalo Marekani imelitaja kuwa la “kuogofya”.

Waokoaji walisema jengo la makazi la ghorofa tano lilipigwa, na video kwenye mitandao ya kijamii zilionesha miili iliyofunikwa kwa blanketi sakafuni.

Jeshi la Israel lilisema “linafahamu ripoti kwamba raia walijeruhiwa leo [Jumanne] katika eneo la Beit Lahia”. Imeongeza kuwa taarifa za tukio hilo zinaangaliwa.

Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vimekuwa vikifanya kazi kaskazini mwa Gaza katika muda wa wiki mbili zilizopita, hasa katika maeneo ya Jabalia, Beit Lahia na Beit Hanoun.

Mkurugenzi wa hospitali ya karibu ya Kamal Adwan huko Jabalia, Hussam Abu Safia, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watoto walikuwa wakitibiwa katika hospitali hiyo ambayo inatatizika kuwatibu wagonjwa kutokana na ukosefu wa wafanyakazi na dawa.

“Hakuna kilichosalia katika Hospitali ya Kamal Adwan isipokuwa vifaa vya huduma ya kwanza baada ya jeshi kukamata timu yetu ya matibabu na wafanyikazi,” Abu Safia alisema.

IDF ilivamia hospitali hiyo wiki jana, ikisema ilikuwa ikitumiwa na wapiganaji wa Hamas.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller alisema Marekani “imesikitishwa sana na kupoteza maisha ya raia katika tukio hili.

Hili lilikuwa tukio la kuogofya na matokeo ya kuogofya”.

Israel inasema operesheni zake kaskazini mwa Gaza zimefanyika ili kuzuia Hamas kujipanga upya na inawatuhumu kwa kujiingiza miongoni mwa raia, jambo ambalo Hamas inakanusha.

KITIMTIM CHA SIASA NCHINI MAREKANI

Je, uchaguzi wa Marekani unaweza kubadilisha dunia kwa jinsi gani?

h

Maelezo kuhusu taarifa

Wakati Rais wa Marekani Joe Biden alipoitembea Kyiv mnamo Februari 2023 katika ziara ya kushtukiza kuonyesha mshikamano na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, za ving’ora zilikuwa zinasikika . “Nilihisi kitu chenye nguvu zaidi ambayo sijawahi kuwa nayo,” baadaye nilikumbuka. “Marekani ni nguzo ya ulimwengu.”

Sasa dunia inasubiri kuona nani ataongoza “nguzo” hii baada ya Wamarekani kufanya uchaguzi wao katika uchaguzi wa rais wiki ijayo. Je, itakuwa Kamala Harris, kwa imani yake kwamba “Marekani haiwezi kumudu kurudi nyuma katika nyakati hizi za misukosuko,” kuendelea kuongoza kwa Biden? Au itakuwa Donald Trump, na matumaini yake kwamba “Umarekani, sio utandawazi” utakaoongoza?

Tunaishi katika ulimwengu ambao thamani ya ushawishi wa Marekani ulimwenguni unatiliwa shaka.

Mataifa yenye nguvu ya kikanda yanakwenda kwa njia yao wenyewe, tawala za kiimla zinaunda ushirikiano wao wenyewe, na vita vya kutisha huko Gaza, Ukraine, na kwingineko vinaibua maswali yasiyo na wasiwasi juu ya thamani ya jukumu la Washington.

Lakini Marekani ni muhimu kwa sababu ya nguvu zake za kiuchumi na kijeshi, na jukumu lake kuu katika ushirikiano mwingi. Nilizungumza na waangalizi wenye ufahamu mzuri na wanaotazamwa kwa karibu kwa mawazo na tafakari zao kuhusu athari za ulimwengu za uchaguzi huu muhimu.

Nguvu ya kijeshi

Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa NATO, Rose Gottemoeller, alisema: “Siwezi kupunguza maonyo haya ya Donald Trump ni jinamizi kwa Ulaya, haswa kutokana na tishio lake la kujiondoa kutoka kwa NATO linalosikika kama mwangwi masikioni mwa kila mtu.”

Matumizi ya ulinzi ya Washington ni sawa na theluthi mbili ya bajeti ya kijeshi ya nchi 31 wanachama wa NATO. Nje ya NATO, Marekani hutumia zaidi jeshi lake kuliko mataifa 10 makubwa zaidi kwa pamoja, ikiwa ni pamoja na China na Urusi.

Trump anajivunia kuwa ana jukumu kubwa katika kuzilazimisha nchi nyingine za NATO kufikia malengo yao ya matumizi ya kijeshi ya asilimia 2 ya pato la taifa – ni nchi 23 tu wanachama ambazo zimefikia lengo hilo kufikia mwaka 2024. Lakini kauli zake za uongo bado zinatia wasiwasi.

Ikiwa Kamala Harris atashinda, Bi Gottemoeller anaamini, “NATO bila shaka itakuwa katika mikono mizuri huko Washington.” Wakati huo huo, pia anaonya kwamba Kamala “atakuwa tayari kuendelea kufanya kazi na NATO na EU ili kupata ushindi nchini Ukraine, lakini hataacha kuishinikiza Ulaya kuhusu matumizi ya kijeshi.”

g
Maelezo ya picha,Harris aliahidi kuwa mshirika mkubwa wa Ukraine.

Lakini timu ya Kamala ya White House italazimika kushindana na Seneti au Baraza la wawakilishi ambalo hivi karibuni linaweza kuwa mikononi mwa Republican na halitakuwa na mwelekeo wa kuunga mkono vita vya kigeni kuliko wenzao wa Democratic.

Kuna hisia inayoongezeka kwamba yeyote atakayekuwa rais, shinikizo litaongezeka mjini Kiev kutafuta njia za kuondokana na vita hivi wakati wabunge wa Marekani wakizidi kuhangaika kupitisha vifurushi vikubwa vya misaada.

‘‘Mtafutaji amani’’

Rais mpya wa Marekani atalazimika kufanya kazi katika ulimwengu unaokabiliwa na mapambano makubwa zaidi tangu zama za Vita Baridi, kati ya mataifa makubwa.

“Marekani bado ni mhusika muhimu zaidi wa kimataifa katika masuala ya amani na usalama,” anasema Comfort Ero, rais na mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utatuzi wa migogoro ya kimataifa , International Crisis Group. “Lakini uwezo wake wa kusaidia kutatua migogoro umepungua,” anaonya.

Vita vinaendelea kuwa vigumu zaidi kumalizika. “Mgogoro wa muda mrefu unazidi kuwa mgumu, huku ushindani mkubwa wa nguvu ukiongezeka na nguvu za kati zikiongezeka,” Bi Ero anaelezea mazingira. Vita kama vile vya Ukraine huhusisha nguvu nyingi, na migogoro kama Sudan inawapa wahusika wa kikanda maslahi ya kushindana dhidi ya kila mmoja, wengine zaidi wamewekeza katika vita kuliko amani.

Marekani inapoteza msingi wake wa maadili, Bi Comfort anasema. “Wahusika wa vita wa kimataifa wanatambua kwamba inahusika kwa kiwango kimoja kwa vitendo vya Urusi nchini Ukraine na kwa vitendo vya Israeli huko Gaza,” anasema. “Vita nchini Sudan vimekuwa na ukatili wa kutisha lakini vinachukuliwa kama suala la daraja la pili.”

Ushindi wa Harris , anasema, “atamaanisha mwendelezo na utawala wa sasa,” wakati ikiwa Trump atashinda, anaweza “kuipa Israeli uhuru mkubwa zaidi huko Gaza na kwingineko, na amedokeza kwamba anaweza kujaribu kupunguza makubaliano na Moscow juu ya Ukraine kwa gharama ya Kiev.”

Kuhusu Mashariki ya Kati, mgombea huyo wa chama cha Democratic alirudia mara kwa mara kuunga mkono vikali hatua ya Biden ya “haki ya Israel kujilinda,” lakini pia alisisitiza kuwa “mauaji ya Wapalestina wasio na hatia lazima yakome.”

Trump pia alitangaza kwamba ni wakati wa “kurejea kwenye amani na kuacha kuua watu,” lakini aliripotiwa kumwambia kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu: “Fanya kile unachotakiwa kufanya.”

g

Mgombea wa Republican anajivunia kuwa yeye ni “mtafutaji amani.” Aliahidi katika mahojiano na Al Arabiya Jumapili jioni: “Nitafikia amani katika Mashariki ya Kati hivi karibuni.”

Ameahidi kupanua mkataba wa mwaka 2020 unaofahamika kama Abraham Accords, ambao ulirejesha uhusiano kati ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiarabu lakini unaonekana kuwa umewatenga Wapalestina na kuchangia katika mgogoro wa sasa ambao haujawahi kutokea.

Kuhusu Ukraine, Trump hajawahi kuficha sifa zake kwa “watu wenye nguvu” kama kiongozi wa Urusi Vladimir Putin. Mgombea huyo wa Republican ameweka wazi kwamba anataka kumaliza vita nchini Ukraine, na kwa msaada mkubwa wa kijeshi na kifedha wa Marekani. “Ninaondoka,” alisisitiza katika mkutano wa hivi karibuni. “Tunapaswa kuondoka katika vita hivi.”

Kwa upande wake, Bi Harris alisema: “Nimekuwa na fahari kusimama na Ukraine. Nitaendelea kushirikiana na Ukraine. Na nitajitahidi kuhakikisha kuwa Ukraine inashinda vita hivi.”

Lakini Comfort Ero, rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kikundi International Crisis Group ana wasiwasi kwamba bila kujali nani anachaguliwa, mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi duniani.

Mahusiano ya kibiashara na Beijing

Kwa mtazamo wa msomi wa China Profesa Rana Mitter, pendekezo la Trump la ushuru wa asilimia 60 kwa bidhaa zote za China zinazoingizwa nchini humo ni “mshtuko mkubwa kwa uchumi wa dunia katika miongo kadhaa.”

Kuonesha gharama kubwa kwa China na washirika wengine wengi wa kibiashara imekuwa moja ya vitisho vya Trump vinavyoendelea kama sehemu ya mbinu yake ya “Marekani Kwanza”.

Lakini Trump pia anachukulia kile anachokiona kama uhusiano wake wa kibinafsi na Rais Xi Jinping. Aliiambia bodi ya wahariri ya Wall Street Journal kwamba hatalazimika kutumia nguvu za kijeshi ikiwa Beijing itaamua kuizuia Taiwan kwasababu kiongozi huyo wa China “ananiheshimu na anajua nina wazimu.”

Lakini viongozi wote wa Republican na Democrats ni wachuuzi, na wote wanaiona Beijing kuwa na nia ya kujaribu kuipiku Marekani kama taifa lenye nguvu zaidi duniani.

Lakini mwanahistoria wa Uingereza anayesomea uhusiano wa Marekani na Asian katika shule ya Kennedy ya Harvard, Profesa Mitter, anaona tofauti kadhaa. Pamoja na Bi Harris, anasema, “uhusiano huo unaweza kubadilika kwa kiwango sawa na ilivyo sasa.” Ikiwa Trump atashinda, itakuwa “hali mbaya zaidi.”

Bwana Mitter anaangazia viwango viwili vya Trump kuhusu iwapo atatetea kisiwa kilicho mbali na Marekani – Taiwan.

Viongozi wa China wanaamini kuwa Harris na Trump watakuwa na msimamo mkali. “Kikundi kidogo cha watu wanaoanza biashara kinampendelea Harris, kwa kuzingatia msemo wa zamani ‘Ni bora adui unayemjua kuliko rafiki usiyemjua,'” anasema Profesa Mitter.

Watu wachache wanamuona Trump kama mtu asiyetabirika ambaye anaweza kufanya biashara kubwa na China, hata hivyo hakuna uwezekano wa hilo kuonekana.

Mgogoro wa hali ya hewa

“Uchaguzi wa Marekani una madhara makubwa sio tu kwa raia wake bali kwa dunia nzima kwa sababu ya dharura ya mgogoro wa hali ya hewa na mazingira,” anasema Mary Robinson, rais wa zamani wa Ireland na kamishna mkuu wa zamani wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, ambaye sasa ni mwenyekiti wa The Elders, kundi la viongozi wa dunia lililoanzishwa na Nelson Mandela.

h
Maelezo ya picha,Onyo la joto kali katika Death Valley, California, USA

Lakini wakati kimbunga Milton na Helene vikiendelea, Trump alidharau mipango na sera za mazingira kushughulikia dharura ya hali ya hewa kama “moja ya kashfa kubwa zaidi kuwahi kutokea.” Wengi wanatarajia Trump kujiondoa katika mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi wa mwaka 2015, kama alivyofanya katika muhula wake wa kwanza.

Hata hivyo, Robinson anaamini kuwa Trump hawezi kuzuia kasi ambayo hali ya hewa ya sasaya Marekani: “Hawezi kuzuia mabadiliko ya nishati nchini Marekani na kuondoa mabilioni ya dola katika ruzuku ya kijani.”

Harris, ambaye bado hajatoa msimamo wake juu ya hali ya hewa, alihimiza kila mtu kuongeza juhudi za “kuongoza katika kulinda mazingira .”

Uongozi katika masuala ya kibinadamu

“Matokeo ya uchaguzi wa Marekani ni muhimu sana, kutokana na ushawishi usio wa kawaida ambao Marekani inautumia, sio tu kupitia nguvu zake za kijeshi na kiuchumi, bali kupitia uwezo wake wa kuongoza kwa mamlaka ya kimaadili katika jukwaa la dunia,” anasema Martin Griffiths, mpatanishi mkongwe wa migogoro ambaye hadi hivi karibuni alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na mratibu wa misaada ya dharura.

Griffith anaona mwanga mkubwa wa matumaini ikiwa Harris atashinda. Kwa upande mwingine, anasema, “kurejea kwa urais wa Trump, wa upande mmoja kunazidisha tu ukosefu wa utulivu duniani na kukata tamaa.”

g
Maelezo ya picha,Bango mjini Tehran linamuonyesha rais wa Iran na mkuu wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi akikabiliana na Biden na Netanyahu.

Marekani pia ni mfadhili mkubwa zaidi linapokuja suala la mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikitoa rekodi ya dola bilioni 18.1 mnamo 2022.

Lakini katika muhula wa kwanza wa Trump, alisitisha ufadhili kwa mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na kujiondoa katika Shirika la Afya Duniani. Wafadhili wengine walikimbilia kujaza mapengo – kitu ambacho Trump alitaka kuona kikitokea.

Lakini Bwana Griffiths anaangazia kuongezeka kwa kukata tamaa katika jamii ya kibinadamu hata zaidi, na kukosoa “uamuzi” wa utawala wa Biden juu ya hali mbaya katika Mashariki ya Kati. Viongozi wa mashirika ya misaada wamelaani mara kwa mara mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7 dhidi ya Waisraeli. Lakini mara kwa mara wameitaka Marekani kuchukua hatua zaidi kukomesha mateso makubwa ya raia katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.

Licha ya Biden na maafisa wake wa ngazi ya juu kutoa wito wa mara kwa mara wa kutaka msaada zaidi kwa Gaza, wakosoaji wanasema misaada na shinikizo hilo havijatosha.

“Uongozi wa kweli unatokana na kushughulikia migogoro ya kibinadamu kwa uwazi usioyumba wa kimaadili, na kutekeleza ulinzi wa maisha ya binadamu kuwa msingi wa diplomasia ya Marekani ,” Griffiths alisema.

Lakini bado anaamini kuwa Marekani ni taifa lenye nguvu kubwa. “Katika wakati wa migogoro ya kimataifa na kwa kutokuwa na uhakika, dunia inatamani Marekani iinuke kwenye changamoto ya uongozi wa uwajibikaji, wa kanuni,” alisema. “Tunahitaji zaidi. Tunastahili zaidi. Na tuna ujasiri wa kutumaini zaidi.”

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment