Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Kaskazini Choe Son Hui amewasili nchini Urusi kwa ziara ya kikazi, ziara inayokuja baada ya Korea Kusini na Marekani kudai kwamba Pyongyang imetuma maelfu ya wanajeshi wake kufanya mafunzo nchini Urusi.

Vyombo vya habari vya Urusi vimethibitisha kwamba Coe atakuwa na mazungumzo na maofisa nchini Urusi bila ya kuweka wazi na akina nani atakaokutana nao.
Washington imesema kwamba Korea Kaskazini imewatuma wanajeshi Elfu 10 kwenda kufanya mafunzo nchini Urusi, maofisa hao wakitarajia kupigana nchini Ukraine. Korea Kusini kwa upande imetaja hatua ya Korea Kaskazini na Urusi kama tishio kwa usalama.

Rais wa Urusi Vladimir Putin hajakana kuwepo kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini mwake.
Urusi na Korea Kaskazini zimeimarisha uhusiano wao katika siku za hivi karibuni, kiongozi wa Pyongyang Kim Jong Un akifanya ziara nchini Urusi kukutana na rais Putin mashariki mwa Urusi mwezi Septemba.

Putin alitia saini makubaliano ya kijeshi na Kim mjini Pyongyang mwezi Juni wakati wa ziara yake ya kwanza kwenye taifa hilo katika kipindi cha miaka 24. Choe tayari amefanya ziara nchini Urusi kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka huu.
Ubalozi wa Urusi mjini Pyongyang umesema ziara ya sasa ya Choe imekuja baada ya viongozi wa mataifa hayo kukubaliana kuwa na mazungumzo ya kimkakati wakati wa mkutano wao wa mwezi Juni.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.