Usisahau kuwa kupenda ni HISIA Ila kuhitaji ni UHALISIA.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hili litakusaidia

Usiwadharau uliowaacha na wala usiwaabudu uliowakuta maana hatua zako ziko mikononi mwa Mungu pekee

Kikubwa endelea kunyenyekea katika mkono wa Bwana ulio hodari ili akukweze kwa wakati wake Na usisahau kila hatu Dua

Kumbuka kuwa, kuna watu ambao UNAWAPENDA na kuna wale ambao UNAWAHITAJI.

Usisahau kuwa kupenda ni HISIA Ila kuhitaji ni UHALISIA.

Kwa maneno mengine ni kuwa, usijichanganye kwenye maisha ukawakumbatia unaowapenda peke yao na ukasahau unaowahitaji.

Labda niseme hivi; unapougua ugonjwa na unahitaji matibabu, UNAMUHITAJI Daktari.

Hata Kama atakuwa na rangi, urefu au kabila ambalo haulipendi, Ila kwa wakati huo UNAMUHITAJI.

Watu wengi kwenye maisha yao, huwa wanashindwa kutimiza baadhi ya MALENGO kwa sababu wanatumia muda na nguvu nyingi kwa wanaowapenda na KUWAPUUZA wanaowahitaji.

Kila MAJIRA ya maisha yako kuna watu UNAOWAHITAJI.

Hata kama hauwapendi Ila hakikisha unawapa fursa ya kuchangia HATUA YAKO inayofuata.

Kama umeipenda makala hii…

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment