Naim Qassem ateuliwa kuongoza Hezbollah baada ya kifo cha Nasrallah

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wapiganaji wa Hezbollah wa nchini Lebanon wamemteua naibu kiongozi wao Naim Qassem kuchukua nafasi ya Hasan Nasrallah aliyeuwa katika shambulio la Israeli kusini mwa mji wa Beirut mwezi uliopita.

Naim qassem ameteuliwa kuchukua nafasi yake Nasrallah aliyeuawa katika shambulio la Israeli.
Naim qassem ameteuliwa kuchukua nafasi yake Nasrallah aliyeuawa katika shambulio la Israeli. via REUTERS – AL MANAR TV

Hashem Safieddine, kiongozi wa baraza kuu la Hezbollah, alikuwa ametajwa kama ambaye angechukua wadhifa wa Nasrallah.

Safieddine aliuawa pia katika shambulio la Israeli kusini mwa mji wa Beirut muda mfupi baada ya kuuawa kwa Nasrallah.

Soma piaIsraeli yadai kumuua Hashem Safieddine, kiongozi mwingine wa Hezbollah

Qassem, 71, alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa kundi la Hezbollah mwaka wa  1982 na amekuwa akihudumu katika wadhifa wa katibu mkuu tangu mwaka wa  1991, kabala ya Nasrallah kuchukua uongozi wa kundi hilo.

Alizaliwa mjini Beirut mwaka wa 1953 katika kijiji cha Kfar Fila kwenye mpaka wa Israeli.

Naïm Qassem, Kiongozi mpya wa Hezbollah.
Naïm Qassem, Kiongozi mpya wa Hezbollah. © Reuters/Al Manar TV

Tangu kuuawa kwa Nasrallah katika shambulio la Israeli la tarehe 27 ya mwezi Septemba, Qassem amekuwa na hotuba tatu za televisheni akizungumza katika lugha ya Kirabu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment