Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Misri imependekeza mpango wa usitishwaji wa vita kwenye ukanda wa Gaza kati ya jeshi la Israeli na kundi la Hamas, ili kujaribu kupata mkataba wa kudumu, baada ya mapigano ya zaidi ya mwaka mmoja sasa.
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesema mapendekezo hayo, yatawezesha kuachiwa huru kwa mateka wanne wa Israeli wanaoshikiliwa Gaza lakini pia kuachiwa huru kwa wafungwa wa Kipalestina wanaozuiwa kwenye magereza ya Israeli.
Aidha, kiongozi huyo wa Misri ameongeza kuwa baada siku hizi mbili, kutakuwa na mazungumzo ya siku 10 kupata mkataba wa kusitusha vita.

Hata hivyo, rais al-Sisi hajaeleza iwapo mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Israel na Hamas na yamekubaliwa wakati huu mazungmzo yakirejelewa jijini Doha nchini Qatar kati ya wawakilishi wa pande hizo mbili.
Wakati hayo yakijiri, wanajeshi wa Israeli wameendelea kutekeleza mashambulio kwenye ukanda wa Gaza ambapo watu 53 wameuawa huku wengine wakipoteza maisha nchini Lebanon.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.