Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mapigano yameripotiwa siku ya Jumapili kati ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na jeshi la Kongo linaloungwa mkono na washirika wake. Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi wa Oktoba, FARDC imezuia waasi kusona mbele.

Hii ni siku ya pili mfululizo ya mapigano yanayoripotiwa katika eneo la Walikale. Kwa mujibu wa duru za usalama kwa sharti la kutotajwa majina, wanajeshi wa Kongo na Wazalendo waliingilia kati katika shambulio la Minjenji kujaribu kuwatimua waasi wa M23.
Miilio ya silaha nzito bado ilikuwa ikisikika siku ya Jumapili jioni, kwa mujibu wa vyanzo vya utawala. M23 sasa itakuwa karibu kilomita ishirini kutoka mji wa Pinga, eneo la kimkakati la kijeshi.
Kama Fiston Misona, kongozi wa mashirika ya kiraia katika eneo la Walikale, anaomba majibu ya haraka ya kibinadamu, pia anasisitiza juu ya jibu la kutosha dhidi ya waasi. “Tunaiomba serikali ya Kongo ili iweze kutatua hali hii ya M23 haraka iwezekanavyo. Bado tuna jeshi ambalo tunaliheshimu na ambalo bado tunaliamini. Polisi na vijana wanaojitolea kusaidia kutetea maslahi ya taifa wanapaswa kutoa usaidizi wao kwa jeshi. Tuna helikopta za vita, tuna ndege zisizo na rubani, tunashangaa kwa nini vyombo hivi vyote havitumiki. “
Jeshi la Kongo bado halijatoa taarifa yoyote kufuatia mapigano haya mapya. Mashambulio ya waasi yanaendelea huku usitishaji mapigano uliotolewa na Luanda ukitakiwa kuheshimiwa na pande zote mbili.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.