Kwa WANANDOA Wanaotaka Mafanikio Ya KIFEDHA…
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Watumiaji Hovyo
iii. Makini na Mtumiaji
iv. Kila Mtu na Lake
v. Wanandoa Tegemezi
vi. Wanandoa Wafanyabiashara
vii Wanandoa Marafiki
Katika Makala Hii Tutazungumzia Aina ya Tatu ya Wanandoa.
– Makini na Mtumiaji
Kwenye kundi hili kunakuwa na mwanandoa mmoja ni mtumiaji wa hovyo na mwingine ni makini sana katika matumizi ya pesa.
Mwingine anataka kila siku mpange bajeti na muifuate, mwingine hajali mambo ya bajeti na hata kama mkipanga huwa haifuati.
Yaani hapa, kuna mmoja anaweza kuwa anajibana sana hadi katika mambo muhimu, lakini mwingine ananunua vitu hovyo hovyo bila kujali.
Kinachouma zaidi yule anayetumia hovyo hovyo ndio unakuta wa kwanza kuanza kuuliza mambo ya kujenga, kulipa ada, n.k.
Ila akiba mliyoweka au pesa alizopata yeye alizitumia hovyo hovyo na alizimaliza.
Wanandoa wa namna hii huwa ugomvi wa mambo ya pesa hauishi kila siku.
Na huweza kupelekea yule mtumiaji makini kuwa na hofu ya kutoa taarifa za pesa kwani anajua zikijulikana zipo zitatumiwa haraka.
Ili wanandoa hawa wawe na mafanikio, ni lazima yule mtumiaji hovyo aamue kubadilisha falsafa yake ya maisha kuhusu fedha.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.