Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Nchini Msumbiji tume ya uchaguzi imemtangaza Daniel Chapo, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba tarehe 9.

Chapo, kutoka chama tawala chama cha Frelimo ametangazwa mshindi kwa kupata asilimia 70.67 ya kura huku mpinzani wake wa karibu Venancio Mondlane, akipata asilimia 20.32.
Wakati matokeo hayo yaliposubiriwa, jiji kuu Maputo lilibaki mahame kuanzia mapema siku ya Alhamisi, wakati huu wafuasi wa upinzani wakitarajiwa kuandamana kupinga matokeo hayo.
Mondlane, anayeungwa mkono na vyama vingine vya upinzani, tayari amesema kuwa yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, na matokeo ya mwisho hayatakuwa huru na haki na hivyo kuwataka wafuasi wake kujitokeza na kuandamana.
Soma piaMsumbiji: Wasiwasi wa kutokea vurugu kuhusiana na matokeo ya uchaguzi yaibuka.
Hali ya wasiwasi imekuwa ikiendelea kushuhudiwa nchini Msumbiji kuanzia Jumamosi iliyopita, baada ya kuuawa kwa wakili wa upinzani Elvino Dias, na mwanaharakati Paulo Guambe.
Rais anayemaliza muda wake, Filipe Nyusi, amewashtumu wanasiasa wa upinzani kwa kupanga na kuchochea machafuko nchini humo
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.