EU yaongeza muda wa vikwazo dhidi ya Burundi hadi mwaka wa 2025

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Umoja wa Ulaya, umeamua kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025.

Mji wa Bujumbura.
Mji wa Bujumbura. © Wikimedia

Ripoti zinasema, Baraza la Umoja wa Ulaya, limetangaza kuongeza muda wa vikwazo hivyo hadi tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2025.

Vikwazo hivyo, viliwekewa serikali ya Burundi, wakati huo ikiongozwa na Marehemu Pierre Nkurunziza, kutokana na rekodi mbaya ya haki za binadamu na kuwahangaisha wanasiasa wa upinzani na wanaharakati.

Hayati rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, aliyeaga dunia Juni 8, 2020.
Hayati rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, aliyeaga dunia Juni 8, 2020. REUTERS/Jean Pierre Aime Harerimana

Wakati wa uongozi wa Nkurunzinza, aliifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo na kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu, na kuzua sintofahamu ya kisiasa nchini humo.

Kutoka na thathmini ya Umoja huo wa Ulaya, imebainika kuwa hali ya haki za binadamu imeendelea kuwa mbaya na hakuna mageuzi makubwa ya kisiasa yaliyofanywa na uongozi wa kisasa ili kuondoa vikwazo hivyo.

Rais wa sasa wa Burundi Évariste Ndayishimiye na serikali yake hawajazungumzia hatua hiyo ya EU.
Rais wa sasa wa Burundi Évariste Ndayishimiye na serikali yake hawajazungumzia hatua hiyo ya EU. © AFP

Aidha, Baraza la EU limesema, serikali ya Burundi inapaswa kuanzisha mazungumzo ya ndani ili kurejesha demokrasia thabiti nchini humo.

Miongoni mwa vikwazo ilivyowekewa ni pamoja na kuwazuia kusafiri maafisa wa serikali wanaodaiwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu, mali zao zimezuiwa na Umoja wa Ulaya, Umoja huo pia umezuia misaada kwa serikali ya Burundi ambayo haijajibu kuongezwa muda kwa vikwazo hivyo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment