Msumbiji: Mamlaka yawaonya wanaopanga maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Msumbiji anayemaliza muda wake, Felipe Nyusi, ameonya kuwa vurugu zozote za kisiasa zitachukuliwa kama vitendo vya kihalifu, wakati huu upinzani ukijiandaa kwa maandamano zaidi kupinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 9 yanayotarajiwa kutangazwa rasmi Ijumaa ya wiki hii.

Polisi wakipiga doria mjini Maputo baada ya mgombea wa upinzani kutoa wito kwa wafuasi wake kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, Oktoba 22, 2024. REUTERS/Siphiwe Sibeko     TPX IMAGES OF THE DAY
Polisi wakipiga doria mjini Maputo baada ya mgombea wa upinzani kutoa wito kwa wafuasi wake kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, Oktoba 22, 2024. REUTERS/Siphiwe Sibeko TPX IMAGES OF THE DAY © Siphiwe Sibeko / Reuters

Onyo la rais linakuja wakati mgombea mkuu wa upinzani Venancio Mondlane, akitoa wito wa siku 25 za kuiasi serikali kutokana na mauaji ya wakili wake.

Akizungumza Jumatano ya wiki hii,  Rais Nyusi alisema kuwahimiza wananchi kuiasi serikali, kutoa taarifa zisizo sahihi na kuleta machafuko kwa madhumuni ya kisiasa kunaweza kuchukuliwa kuwa ni uhalifu.

Filipe Nyusi - Rais wa Msumbiji anayeondoka.
Filipe Nyusi – Rais wa Msumbiji anayeondoka. © LUSA – LUÍSA NHANTUMBO

Katiba inawapa wananchi wa Msumbiji haki ya kuandamana, lakini kwa kuheshimu utaratibu wa kisheria, alisema Nyusi, huku akimtaka kila anayepinga matokeo ya uchaguzi kutumia njia za kikatiba.

Siku ya Alhamis maelfu ya raia walikusanyika nje ya mji mkuu maputo, kumzika wakili Elvino Dias aliyeuawa pamoja na mshirika mwingine wa upinzani, Paulo Guambe, wawili hao, walikuwa wakitayarisha kesi ya kupinga kura kwa niaba ya Mondlane na chama cha Podemos kinachomuunga mkono.

Wakili wa mwanasiasa Mkuu wa upinzani azikwa

Maelfu ya watu wamehudhuria mazishi ya wakili wa mwanasiasa mkuu wa upinzani Venancio Mondlane, aliyeuawa wakati huu, matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 9 mwezi huu yanapotarajiwa.

Mazishi ya wakili Elvino Dias yamefanyika, wakati mgombea mkuu wa upinzani Mondlane akiitisha maandamano ya siku 25.

Mazishi ya wakili wa chama cha Podemos, Elvino Dias yamefanyika Jumatano ya wiki hii  nchini Msumbiji.
Mazishi ya wakili wa chama cha Podemos, Elvino Dias yamefanyika Jumatano ya wiki hii nchini Msumbiji. REUTERS – Siphiwe Sibeko

Wakili huyo aliuawa na watu wanaominiwa kuwa maafisa wa serikali akiwa na wakili mwenzake Elvino Dias, wakati wakijiandaa kuwasilisha kesi Mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais.

Kwenye ujumbe wake wa Facebook, Mondlane, amewashtumu maafisa wa usalama kwa kuwalenga na kuwapiga risasi 25 mawakili hao wawili wakati huu polisi wakiahidi uchunguzi wa mauaji hayo.

Upinzani unaituhumu serikali kwa kumuua wakili wa chama cha  Podemos Elvino Dias.
Upinzani unaituhumu serikali kwa kumuua wakili wa chama cha Podemos Elvino Dias. REUTERS – Siphiwe Sibeko

Tayari waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Umoja wa Ulaya, wametoa taarifa ya kuonesha mashaka yao kuhusu uhalali wa matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo wa urais, ambao mgombea mkuu wa chama tawala cha FRELIMO, Daniel Chapo, anatarajiwa kutangazwa mshindi.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment