Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwa Wanaotaka KUHITIMU CHUO Kwa MAFANIKIO Tu!…
i. Chuo Ni Kiwanda
ii. Kozi unayosoma ni chaguo Lako?
iii. Katika Aina 6 Za UTAJIRI, Masomo Yako Yatakusaidia Kuupata Upi?
Katika Makala Hii Tutazungumzia Jambo La Pili.
– Kozi Unayosoma Ni Chaguo Lako?
Moja ya “stress” inayoendelea kwa sasa kwenye maisha ya watu wengi ni pale ambapo anajikuta amesoma kozi ambayo haipendi.
Na haikuwa chaguo lake na analazimika asome hadi amalize kisha akafanye kazi inayohusiana na hiyo kozi ambayo kiukweli ni kuwa haipendi kabisa.
Utafiti uliowahi kufanywa na “The Students Room” unaonyesha kuwa mwanachuo mmoja kati ya wanachuo watano huwa anahisi kuwa amefanya maamuzi yasiyo sahihi kuhusiana na kozi aliyochagua, yaani wanajutia.
Wengi unakuta walishawishiwa na wazazi, ndugu, marafiki au wengine walijikuta wameangukia katika kozi hizo kwa sababu ufaulu wao au ufadhili ndio uliowalazimisha, ila kutoka moyoni walikuwa hawapendi kabisa.
Utafiti huu ulionyesha kuwa 41% walipoanza kusoma waligundua kuwa wanachofundishwa sio kile walichotarajia kabla hawajaanza kusoma.
Na 19% wanaona kuwa wanachojifunza hakitawasaidia kupata kazi/kufanikisha malengo yao ya maisha watakapohitimu chuo.
Kama umejikuta unasoma kozi ambayo haikuwa chaguo lako wala ndoto yako, basi umefanya vyema kusoma kitabu hiki kwa sababu kitakusaidia sana.
Hakikisha umesoma hadi sura ya mwisho ili kujifunza yale ambayo wengine walijifunza na kuyafanya wakiwa chuoni na wakapata mafanikio.
Kama unataka kujifunza Mbinu Za Kuwa Tofauti Kati Ya Wengi Utakaohitimu Nao, LEO nashauri usome eBook yangu ya “KABLA YA KUHITIMU CHUO, Mbinu Za Kuwa Tofauti Kati Ya Wengi Utakaohitimu Nao”.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.