Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Karibu katika Matangazo yetu ya jioni moja kwa moja kutoka Communication Center. Tumekuandalia mengi ikiwa ni pamoja
Muhtasari
- Setilaiti iliyotengenezwa na Boeing yavunjika angani
- Trump akishutumu Chama cha Labour cha Uingereza kwa ‘uingiliaji kati wa kigeni’
- Polisi Ujerumani wavamia duka la pizza linalouza kokeini pembeni
- Israel yasema ilimuua aliyetarajiwa kumrithi Nasrallah
Naam,Natumai U buheri wa afya popote pale ulipo duniani kwa mwoyo mkunjufu na mikono miwili Hujambo na karibu katika matangazo yetu Afrika Leo Asubui ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 23/10/2024 Jina langu ni Cantona Joseph,karibu.
Setilaiti iliyotengenezwa na Boeing yavunjika angani

Setilaiti ya mawasiliano iliyotengenezwa na kampuni kubwa ya vyombo vya angani ya Boeing imevunjika kwenye uzingo.
Mwendeshaji satelaiti, Intelsat, amethibitisha “hasara ya jumla” ya iS-33e, ambayo imeathiri wateja katika maeneo ya Ulaya, Afrika na sehemu za eneo la Asia-Pasifiki.
Intelsat pia inasema imechukua hatua kukamilisha “uchunguzi wa kina” wa tukio hilo.
Boeing imekuwa ikikabiliwa na migogoro katika nyanja nyingi, changamoto upande wa ndege za kibiashara na chombo chake cha Starliner.
“Tunashirikiana na mtengenezaji wa satelaiti, Boeing, na mashirika ya serikali kuchanganua data na kufanya uchunguzi,” Intelsat ilisema.
Boeing haikutoa maoni yake moja kwa moja kuhusu tukio hilo, ikirejelea BBC News kwenye taarifa za Intelsat.
Tovuti ya Idara ya Ulinzi ya Marekani ya kufuatilia vyombo vya kwenye anga, SpaceTrack, pia ilithibitisha tukio hilo.
Tahadhari kwenye jukwaa ilisema Jeshi la Anga za Juu la Marekani pia “kwa sasa inafuatilia vipande 20 vinavyohusika” na satelaiti hiyo.
Ikumbukwe kwamba wanaanga wawili wamekwama katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) baada ya chombo cha Boeing Starliner walichowasili nacho mnamo mwezi Juni kuonekana kutofaa katika safari ya kurudi.
Trump akishutumu Chama cha Labour cha Uingereza kwa ‘uingiliaji kati wa kigeni’

Kambi ya Kampeni ya Donald Trump imewasilisha malalamiko kwa Tume ya Shirikisho la Uchaguzi (FEC) dhidi ya Chama cha Labour cha Uingereza, ikikishutumu kwa “uingiliaji kati wa kigeni” katika uchaguzi wa Marekani ili kusaidia kampeni ya Harris-Walz.
Malalamiko hayo yanataja ripoti za vyombo vya habari kuhusu mawasiliano kati ya chama cha Labour na kambi ya kampeni ya Harris pamoja na juhudi za kujitolea, zikisema kuwa hii ni sawa na “michango” isiyo halali.
BBC inaelewa kuwa wanaharakati wa chama cha Labour wanaofanya kampeni katika uchaguzi wa rais wa Marekani wanafanya hivyo katika nafasi zao binafsi.
Chama cha Labour hakijatoa jibu rasmi.
Hasa, malalamiko hayo yanataja gazeti linaloripoti kuwa watu wanaohusishwa na chama cha Labour wamesafiri hadi Marekani kumfanyia kampeni Harris.
Malalamiko hayo yanadai “uingiliaji wa wazi wa Chama cha Labour, na kambi ya kampeni ya Harris imekubali michango isiyo halali ya kitaifa kutoka nje ya nchi.”
Polisi Ujerumani wavamia duka la pizza linalouza kokeini pembeni

Polisi wamevamia duka la pizza magharibi mwa Ujerumani ambalo wanadaiwa kuwahudumia wateja wa dawa ya kulevya ya kokeini pembeni wanapoagiza bidhaa nambari 40 kwenye menyu.
Mamlaka zilidokezwa kuhusu hilo mnamo mwezi Machi na wakaguzi wa chakula, na maafisa wa kikosi cha madawa ya kulevya walianza kufuatilia mgahawa huo, mkurugenzi wa uhalifu Michael Graf von Moltke alisema Jumatatu.
Wakati polisi walipokwenda kumkamata meneja wa mgahawa huo wa pizza nyumbani kwake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 aliripotiwa kurusha begi la dawa za kulevya nje ya dirisha, ambalo “lilianguka mikononi mwa maafisa wa polisi”, polisi wa Düsseldorf walisema.
Polisi walipata kilo 1.6 (lb 3.5) za dawa ya kokeini, 400g (14.1oz) za bangi na €268,000 (£223,120) pesa taslimu katika nyumba hiyo.
Israel yasema ilimuua aliyetarajiwa kumrithi Nasrallah

Jeshi la Israel linasema kuwa lilimuua kiongozi wa kidini aliyekuwa anadokezwa kumrithi aliyekuwa kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, katika shambulio la anga karibu wiki tatu zilizopita.
Hashem Safieddine alifariki katika mashambulizi ya anga kwenye viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kulingana na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).
Hezbollah, shirika lenye nguvu la Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon linalopigana na Israel, halijathibitisha kifo cha Safieddine.
Kiongozi wake wa awali, Nasrallah, aliuawa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Beirut tarehe 27 Septemba.
Baada ya mashambulio ya anga karibu na uwanja wa ndege wa mji huo tarehe 4 Oktoba, maafisa wa Hezbollah walisema wamepoteza mawasiliano na Safieddine, huku vyombo vya habari vya Marekani vikiwataja maafisa wa Israel wakisema mhubiri huyo ndiye aliyekuwa mlengwa wa shambulio hilo.
Milipuko mikubwa ilitikisa jiji usiku huo, ikiacha moshi mwingi ambao ungeweza kuonekana hadi asubuhi.
Siku ya Jumanne, IDF ilitoa taarifa ikisema Safieddine aliuawa pamoja na Ali Hussein Hazima, aliyeelezwa kama kamanda wa Makao Makuu ya Ujasusi ya Hezbollah, katika shambulizi la makao makuu ya kijasusi ya shirika hilo mjini Beirut.
Ilimshutumu Safieddine kwa kuelekeza “mashambulio ya kigaidi dhidi ya taifa la Israel” kwa miaka mingi, pamoja na kushiriki katika “michakato ya maamuzi makubwa” ya Hezbollah.
Hezbollah ni shirika la kijeshi, kisiasa na kijamii ambalo lina nguvu kubwa nchini Lebanon. Imetajwa kama shirika la kigaidi na Israel pamoja na Marekani, Uingereza na nchi nyinginezo.
Siasa za usaliti na ‘njama za mauaji’ zarejea kwa kishindo Kenya

Naibu Rais aliyebanduliwa Rigathi Gachagua. Picha|Maktaba
SIASA za madai ya usaliti na njama za watu kuuawa zimeanza kujitokeza tena baada ya naibu rais aliyetimuliwa mamlakani kudai alijaribiwa kulishwa sumu mara mbili.
Akihutubu Jumapili baada ya kuondoka Hospitali ya Karen, Nairobi, Naibu Rais aliyetimuliwa mamlakani alidai kuwa kulikuwa na majaribio mawili ya kuumua mnamo Agosti 30 kupitia kuwekewa sumu kwenye mlo.
Jaribio la kwanza, alidai, lilitokea kwenye hoteli ya Acacia, Kisumu akiwa kwenye ziara ya kisiasa eneo la Nyanza. Alidai kuwa kulikuwa na jaribio jingine mnamo Septemba 3 wakati ambapo chakula alichostahili kula kwenye mkutano na Baraza la Wazee wa Agikuyu pia kilitiwa sumu.
Bw Gachagua ambaye anapambana mahakamani kuhakikisha kuwa habanduliwi kabisa mamlakani, pia alimwendea Rais akimtaka akome kuhangaishwa familia yake wala asiwaue watoto wake.
“Inasikitisha kuwa Rais ameamuru nipokonywe walinzi wakati ambapo nipo hospitalini. Sina afisa yeyote wa polisi hapa na ameamrisha hata wale ambao walikuwa nyumbani kwangu Nyeri na hapa Karen waondolewe,” akasema Bw Gachagua.
“Sikujua Rais angekuwa katili hivi dhidi yangu. Nimepigwa na mshangao mwanaume ambaye nilimsaidia kupata mamlaka amenigeuka na ananifanyia haya wakati ambapo napigania uhai wangu hospitalini,” akaongeza Bw Gachagua.
Hii si mara ya kwanza ambapo maadai ya mauaji na kuhangaishwa kwa familia ya mwanasiasa zimeanza kuchipuka. Bw Gachagua alikuwa anaonekana kufuata mkondo wa bosi wake ambaye alitoa madai kama hayo wakati ambapo uhusiano wake na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta uliingia mdudu, wawili hao wakiwa mamlakani.
Mnamo Julai 2022, Rais Ruto wakati huo akiwa naibu rais alimwaambia Bw Kenyatta akome kutumia vitisho dhidi yake baada ya kumuidhinisha Kinara wa Azimio Raila Odinga kama mgombeaji wa urais aliyekuwa akiunga kwenye kura ya mnamo Agosti 2022.
Rais Ruto wakati huo alidai kulikuwa na njama ya kumuua pamoja na wanafamilia wake na wandani wake wa kisiasa. Alidai kuwa Bw Kenyatta aliandaa mkutano wa kibinafsi ambapo alimtishia pamoja na wandani wake na akamtaka asielekeze hasira zake kwa watoto wake.
“Namwambia Rais akome kuwatishia watu kwa sababu kazi yake ni kuhakikisha kuna amani nchi. Akome kutuambia kuwa tutajua wewe ndiye rais na kutuhangaisha kwa sababu hatuwezi kutishika,” akasema Ruto wakati huo.
“Mradi tu usiwaue watoto wangu, mimi nitakukabili lakini tuheshimiane,” akaongeza.
Rais Ruto alitoa madai hayo baada ya Bw Kenyatta kumrejelea kama mwanasiasa mwongo ambaye hakuwa amekomaa kisiasa na akawataka wapigakura wamuunge Raila.
“Bw Rais koma kuzungumza kunihusu na uzungumzie mwaniaji wako. Nilikuunga mkono wakati ulihitaji mtu wa kukusaidia kama hutaki kuniunga mkono, niache,
“Nataka nimwambie Rais kuwa licha ya kunifanyia haya yote, sitalipiza kisasi kwa sababu mimi ni Mkiristo. Nitahakikisha umestaafu kwa amani na uniache niongoze nchi kwa sababu najua kile nafanya,” akasema Rais Ruto wakati huo.
Bw Kenyatta hata hivyo alimjibu akisema kuwa Ruto alikuwa amemhangaisha na kumtusi kwa miaka mitatu wala angekuwa na nia ya kumuumiza angekuwa ashafanya hivyo.
“Miaka hiyo mitatu si nimekuwa nikishikilia afisi hii na nilikuwa na mamlaka yote. Wakati huu ambapo nastaafu na sina mamlaka ndiyo unafikiria nina muda wa kukutafuta?” akasema Bw Kenyatta.
Mwaka moja baadaye, Bw Kenyatta naye baada ya kustaafu alidai Rais Ruto alikuwa akimhangaisha na kulenga familia yake. Akizungumza bomani mwa mwanawe mkubwa Jomo Muigai mtaa wa Karen, Bw Kenyatta aliitaka serikali ikome kulenga familia yake na imkabili moja kwa moja.
“Wanafaa waniambie wanataka nini kwa watoto wangu kwa sababu wamewapokonya walinzi na sasa wanataka kuchukua silaha ambazo wanazo kihalali. Ni kwa sababu wanapanga kitu?
“Kama wanapanga jambo basi wasilenge watoto wangu au mamangu. Wapange dhidi yangu na waache familia yangu kabisa,” akasema Bw Kenyatta.
Alilaumu serikali ya Rais Ruto kwa kushiriki njama ya kumhangaisha na familia yake baada ya kuwapokonya walinzi. Alisema serikali inastahili kumwendea na kulipiza kisasi cha kisiasa naye badala ya kulenga familia yake.
Wafanyakazi wa Gachagua wafungiwa nje jumba la Harambee Annex, wakuta kufuli mpya

Jumba la Harambee Annex ambalo lina afisi za naibu rais. Wafanyakazi wa Gachagua wamezuiwa kuingia humo. Picha|Maktaba
WAFANYAKAZI wakuu na wa ngazi za chini wanaofanya kazi katika afisi ya Naibu Rais aliyetimuliwa Rigathi Gachagua, walirudishwa nyumbani Jumanne asubuhi waliporipoti kazini katika Harambee House Annex, Nairobi.
Waliozungumza na Radio Fortune Africa walisema walifika na kukuta maafisa mbalimbali wa usalama wakisimamia jengo hilo. Maafisa hao walitoka Kitengo cha Kukabiliana na dharura (RDU).
Maafisa hao hawakuruhusu mtu yeyote kuchukua video au picha. Waandishi wa habari pia hawakuruhusiwa kufanya mahojiano.
“Walituambia tuende nyumbani hadi tutakapofahamishwa,” alisema mmoja wa wakurugenzi wakuu wanaofanya kazi katika afisi ya Bw Gachagua.
Wale wachache waliobahatika kuingia ndani saa za asubuhi walipata kufuli mpya kwenye milango ya ofisi zao na wakalazimika kuondoka.
Haya yalijiri siku chache tu baada ya wafanyakazi 108 wa naibu rais aliyeondolewa madarakani kutumwa kwa likizo ya lazima.
Katika taarifa iliyotolewa na Katibu wa Usimamizi Patrick Mwangi na kunakiliwa kwa Mkuu wa Wafanyakazi na Utumishi wa Umma Felix Koskei, maafisa wote wa daraja la T na U walitumwa kwa likizo.
Taifa Leo iliwasiliana na Bi Njeri Rugene, mkuu wa mawasiliano wa Bw Gachagua, lakini hakujibu simu wala jumbe zetu.
Bw Gachagua amemlaumu Rais William Ruto kwa masaibu yake.
Jana Rais Ruto aliomba Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi kadhaa za kupinga kuondolewa kwa Rigathi Gachagua kama Naibu Rais, akidai kuwa masuala yaliyoibuliwa katika kesi hizo yametengewa Mahakama ya Juu pekee.
Dkt Ruto alisema katika majibu yake kwamba kesi zilizowasilishwa zinakiuka Kifungu 140 kama kinavyosomwa pamoja na vifungu vya 148 na 149 vya katiba, ambavyo vinatwika Mahakama ya Juu, mamlaka ya kuamua mizozo inayotokana na mchakato wa uchaguzi wa urais.
“Kwa mujibu wa Kifungu cha 165 (5) (a) cha Katiba, Mahakama hii haiwezi kuamua kesi na kutoa maagizo iliyoombwa, kwa kuwa ni suala ambalo limetengewa Mahakama ya Juu,” Dkt Ruto alisema kupitia wakili Adrian Kamotho.
Bw Gachagua na walalamishi wengine kadhaa walipinga mchakato wa kuondolewa kwake madarakani, kutokana na kutoshirikishwa ipasavyo kwa umma na kushindwa kuthibitishwa kwa madai dhidi yake.
Jaji Chacha Mwita na Richard Mwongo, wa Mahakama Kuu ya Milimani na Mahakama Kuu ya Kerugoya, mtawalia waliidhinisha kesi hizo kuwa za dharura na kusimamisha mchakato wa kujaza nafasi ya Bw Gachagua kama Naibu Rais.
Israeli yadai kumuua Hashem Safieddine, kiongozi mwingine wa Hezbollah
Israel imethibitisha kumuua Hashem Safieddine, kiongozi mwingine wa juu wa kundi la Hezbollah, aliyekuwa akitajwa kuwa mrithi wa aliyekuwa kiongozi mkuu wa kundi hilo Hassan Nasrallah ambaye aliuawa katika shambulio la anga mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa jeshi la Israel, Safieddine huenda aliuawa katika shambulio la anga lililotekelezwa wiki tatu zilizopita kusini mwa mjini wa Beirut, huu ukiwa ni uthibitisho wa kwanza tangu Israel iliposema kuwa huenda kiongozi huyo ameuawa.
Hata hivyo licha ya uthibitisho huu wa Israel, kundi la Hezbollah bado halijatoa taarifa yoyote kukanusha au kuthibitisha mauaji ya Safieddine.

Tangu kuuawa kwa Nasrallah, Safieddine ambaye ni ndugu wa kiongozi huyo, amekuwa akiongoza kundi hilo kwa kushirikiana na katibu mkuu wake Naim Qassem, wakisimamia operesheni za kiutawala, kijeshi na kifedha.
Safieddine alianza kuwa mkosoaji mkubwa wa Israel mwaka uliopita ambapo alikuwa akihudhuria mikutano ya hadhara na shughuli za mazishi ambazo Nasrallah alikuwa haudhurii kwa sababu za kiusalama.
Uchaguzi wa Marekani 2024: Elon Musk anawapa baadhi ya wapiga kura dola milioni 1. Je, ni halali?

Maswali yameibuka kuhusu uhalali wa pesa za bilionea wa teknolojia Elon Musk kwa wapiga kura wa majimbo mbalimbali wanaotia saini ombi lake, kabla ya uchaguzi wa Marekani tarehe 5 Novemba.
Ombi hilo liliundwa na kundi la kampeni la Musk la America PAC, ambalo lilianzishwa ili kumuunga mkono Donald Trump katika kinyang’anyiro cha urais.
Lakini wataalam wa sheria wanasema huenda hilo linavunja sheria ya Marekani – kutoa pesa kwa mtu aliyesajiliwa kama mpiga kura.
Musk anatoa nini?
Ombi lililoundwa na Amerika PAC linawahimiza wapiga kura katika majimbo sita – Georgia, Nevada, Arizona, Michigan, Wisconsin na North Carolina – kutia saini ya “kuunga mkono uhuru wa kujieleza na haki ya kubeba silaha.”
Wale wanaoleta mpiga kura mwingine atakayetia saini hupewa kiasi cha dola za kimarekani 47. Kiasi cha juu cha dola 100 kwa kusaini au kumleta mtu wa kusaini hutolewa huko Pennsylvania, jimbo ambalo ni uwanja wa vita kati ya Trump na Harris na kura zao huko zinaaminiwa zinaweza kuamua mshindi wa mwisho.
Amerika PAC inasema wale wanaotia saini ombi hilo wanaashiria kuunga mkono kifungu cha kwanza na cha pili cha katiba ya Marekani.
Kila siku hadi siku ya kupiga kura tarehe 5 Novemba, zawadi ya dola milioni 1 itatolewa katika mfumo wa bahati nasibu kwa mtu yeyote aliyetia saini katika mojawapo ya majimbo saba.
Je, ni halali?

“Naamini pesa ya [Elon] Musk inaweza kuwa ni kinyume cha sheria,” anasema Paul Schiff Berman, profesa wa sheria wa Chuo Kikuu cha George Washington.
Kanuni za Marekani kuhusu sheria ya uchaguzi, inasema mtu yeyote “anayelipa au kujitolea kulipa au kukubali malipo – kwa ajili ya kujiandikisha kupiga kura au kupiga kura” anaweza kutozwa faini ya dola 10,000 au kifungo cha miaka mitano jela.
“Pesa zake ziko kwa ajili ya wapiga kura waliojiandikisha tu, kwa hivyo nadhani anakwenda kinyume na sheria hii,” anasema Berman.
Idara ya Sheria ya Marekani ilikataa kutoa maoni. Tume ya Shirikisho ya Uchaguzi (FEC) imefuatwa ili kutoa kauli.
“Hoja ya kuvunja kanuni inaweza kuwa dhaifu, kwa sababu hakuna anayelipwa moja kwa moja ili kujiandikisha au kupiga kura,” anasema mwenyekiti wa zamani wa FEC, Brad Smith.
“Hawalipi watu kujiandikisha kupiga kura. Anawalipa ili kutia saini ombi lake – na anataka watu waliojiandikisha tu kupiga kura kutia saini ombi hilo. Kwa hiyo nadhani yuko sawa hapa,” anasema.
Lakini profesa wa sheria za uchaguzi katika Chuo Kikuu cha Northwestern aliambia BBC lengo la pesa hiyo kutolewa ni muhimu.
“Naelewa kwa baadhi ya wachambuzi kuwa sio kinyume cha sheria, lakini lengo moja liko wazi, kushawishi watu kujiandikisha kupiga kura kwa njia ambayo ina shida kisheria,” anasema Michael Kang.
Adav Noti kutoka kituo cha Campaign Legal Center, anasema mpango wa Musk “unakiuka sheria ya shirikisho na uko chini ya kosa la kiraia au jinai kwa mujibu wa Idara ya Haki.”
“Ni kinyume cha sheria kutoa pesa kwa masharti kwamba wapokeaji wawe wamejisajili kama wapiga kura,” anasema Noti.
Profesa wa sheria za katiba Jeremy Paul, kutoka Chuo Kikuu cha Northeastern anasema katika barua pepe kwa BBC kwamba Musk anatumia mwanya wa kisheria.
Ingawa kuna hoja kwamba pesa hizo zinaweza kuwa kinyume cha sheria, “lakini zinatolewa kwa mtindo wa kuizunguka sheria” na anaamini kesi hiyo itakuwa ngumu mahakamani.
Hoja za Kisheria
Gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro, anasema jambo hilo, linatia mashaka na kutoa wito kwa vyombo cha sheria kuchunguza.
Mwekezaji bilionea Mark Cuban, ambaye amefanya kampeni katika wiki za hivi karibuni kwa Kamala Harris, anasema:
“Ikiwa mpango huo utafanya kazi au la ni jambo jingine. Na mpango huo unaweza hata kukupa matokeo tofauti na uyatakayo,” aliiambia CNBC.
Musk amejibu ukosoaji huo, akisema Democratic na wafadhili wao wamefadhili mipango kama hiyo hapo awali.
Kwenye X, aliweka chapisho linalosema bosi wa Meta, Mark Zuckerburg “alifanya vivyo hivyo mwaka 2020.”
Zuckerburg alichangia dola milioni 400 katika uchaguzi wa 2020 – lakini pesa hiyo ilitolewa kwa mashirika mawili yasiyoegemea upande wowote ili kusaidia vifaa katika upigaji kura kwa njia ya posta. Haikutolewa moja kwa moja kwa wapiga kura.
Huko nyuma Chama cha Democratic, kiliwahi kuwekeza katika mipango ya kuongeza wafuasi, kwa kampeni ya usajili wa wapiga kura ya dola milioni 25 katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani wa 2022.
Lakini pesa hizi hazikutolewa moja kwa moja kwa wapiga kura. Pesa hizo zilikuwa ni za mipango ya kuwahimiza wapiga kura kujiandikisha, na zilitolewa kwa wale walioajiriwa kubisha hodi nyumba hadi nyumba, na kwa matangazo ya televisheni na mtandaoni.
“Ni halali kuwalipa watu kwenda kusajili wapiga kura, lakini huwezi kuwalipa watu moja kwa moja kujiandikisha,” anasema Prof Kang.
Musk na siasa za Marekani

Tajiri huyo mkubwa zaidi duniani alikuwa na uhusiano mbaya na Trump wakati Trump alipokuwa rais, lakini Musk ameelezea kutofurahishwa kwake na Democratic katika miaka ya hivi karibuni.
Kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022, alitangaza amekihama chama hicho na kuwahimiza wafuasi wake kupiga kura Republican.
Mwaka huu, amejihusisha na siasa za Marekani, akitoa michango na machapisho ya mitandaoni kwa niaba ya Warepublican kadhaa.
Katika maoni yake wiki iliyopita, alieleza kuwa sehemu kubwa ya mpaka wa Marekani na Mexico ni kama filamu ya World War Z.
Musk alizindua America PAC, Julai kwa lengo la kuunga mkono kampeni za Trump za kuwa rais. Hadi sasa amechangia takribani dola milioni 75 katika kikundi hicho.
Tovuti ya Amerika PAC inasema inataka “udhibiti wa mipaka”, “miji salama”, “uhuru wa kujieleza”, “matumizi mazuri ya pesa”, “mfumo sawa wa haki” na “kujilinda”.
Katika wiki za hivi karibuni, Musk ameonekana kwenye kampeni kwa mara ya kwanza, akiwa na Trump na katika ukumbi mwingine akiwa mwenyewe
Mwanamke anaswa kichwa chini miguu juu akijaribu kuokota simu yake iliyoanguka

Mwanamke aliyetajwa kama Matilda Campbell – alikuwa akitembea katika eneo la Mabonde la Hunter huko New South Wales mapema mwezi huu alipoanguka kwenye mwanya wa mita tatu.
Ilikuwa ni mwanzo wa kunaswa kwa saa kadhaa na ilibidi huduma za dharura kuja kukabiliana na kibarua “kigumu” cha uokoaji – ikiwa ni pamoja na kuhamisha miamba kadhaa.
Na hata baada ya kufanikiwa kuondoa mwamba wa kilo 500 (1,100lb) njiani, bado ilibidi wapange jinsi ya kumtoa mwanamke huyo kwa jinsi alivyokuwa amenaswa.
“Katika kipindi cha miaka 10 ya kazi yangu kama mhudumu wa uokoaji sijawahi kukutana na kazi kama hii, ilikuwa kibarua kigumu lakini iliyofanikiwa,” Peter Watts, mhudumu wa huduma ya Ambulance ya New South Wales, alisema.
Tayari alikuwa amenaswa kwa zaidi ya saa moja kabla ya waokoaji kufika, marafiki walijaribu kumuokoa lakini wakashindwa.
Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani aionya Israel kuhusu msaada wa Gaza

Antony Blinken amewaambia viongozi wa Israel kwamba “mengi zaidi yanahitajika kufanywa” ili msaada wa kibinadamu kwa raia upatikane katika eneo la kaskazini mwa Gaza lililozingirwa, na kuibua maswali kuhusu athari zinazoweza kutokea katika sheria za Marekani ikiwa hatua hazitachukuliwa, afisa mwandamizi katika utawala wa Biden anasema.
Siku ya Jumanne, waziri wa mambo ya nje wa Marekani alikutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant, Waziri wa Masuala ya Mikakati Ron Dermer na maafisa wakuu wa kijeshi katika mfululizo wa mikutano mjini Jerusalem na Tel Aviv.
Mikutano hiyo ni sehemu ya ziara ya kikanda ambayo Washington inaiona kama fursa ya kufufua diplomasia baada ya Israel kumuua kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar huko Gaza wiki iliyopita.
Ujumbe katika akaunti ya Blinken kwa Waisrael umetolewa licha ya ukosoaji unaoongezeka kwamba Marekani imeshindwa kuzuia kiwango ambacho raia wameuawa huko Gaza kwa sababu haijakuwa tayari kutumia usambazaji wake wa silaha kwa Israel kama njia ya kudhibiti hilo.
Hata hivyo, Marekani imekuwa ikipinga ukosoaji huo kila wakati.
Afisa huyo alisema Blinken pia aliushinikiza uongozi wa Israel juu ya ripoti kwamba jeshi lake limekuwa likitekeleza kile kinachoitwa “mpango wa majenerali” kaskazini mwa Gaza – mbinu inayoelezewa kama raia wengi kulazimishwa kuhama na kujisalimisha au yenye kusababisha njaa dhidi ya watu wote waliobaki.
Israel imesema mashambulizi yake kaskazini mwa Gaza ni kukomesha kufufuka tena kwa kundi la Hamas.
Setilaiti iliyotengenezwa na Boeing yavunjika angani

Setilaiti ya mawasiliano iliyotengenezwa na kampuni kubwa ya vyombo vya angani ya Boeing imevunjika kwenye uzingo.
Mwendeshaji satelaiti, Intelsat, amethibitisha “hasara ya jumla” ya iS-33e, ambayo imeathiri wateja katika maeneo ya Ulaya, Afrika na sehemu za eneo la Asia-Pasifiki.
Intelsat pia inasema imechukua hatua kukamilisha “uchunguzi wa kina” wa tukio hilo.
Boeing imekuwa ikikabiliwa na migogoro katika nyanja nyingi, changamoto upande wa ndege za kibiashara na chombo chake cha Starliner.
“Tunashirikiana na mtengenezaji wa satelaiti, Boeing, na mashirika ya serikali kuchanganua data na kufanya uchunguzi,” Intelsat ilisema.
Boeing haikutoa maoni yake moja kwa moja kuhusu tukio hilo, ikirejelea BBC News kwenye taarifa za Intelsat.
Tovuti ya Idara ya Ulinzi ya Marekani ya kufuatilia vyombo vya kwenye anga, SpaceTrack, pia ilithibitisha tukio hilo.
Tahadhari kwenye jukwaa ilisema Jeshi la Anga za Juu la Marekani pia “kwa sasa inafuatilia vipande 20 vinavyohusika” na satelaiti hiyo.
Ikumbukwe kwamba wanaanga wawili wamekwama katika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) baada ya chombo cha Boeing Starliner walichowasili nacho mnamo mwezi Juni kuonekana kutofaa katika safari ya kurudi.
Trump akishutumu Chama cha Labour cha Uingereza kwa ‘Kuingilia uchaguzi’ wa Marekani

Kambi ya Kampeni ya Donald Trump imewasilisha malalamiko kwa Tume ya Shirikisho la Uchaguzi (FEC) dhidi ya Chama cha Labour cha Uingereza, ikikishutumu kwa “muingilio” katika uchaguzi wa Marekani ili kusaidia kampeni ya Harris-Walz.
Malalamiko hayo yanataja ripoti za vyombo vya habari kuhusu mawasiliano kati ya chama cha Labour na kambi ya kampeni ya Harris pamoja na juhudi za kujitolea, zikisema kuwa hii ni sawa na “michango” isiyo halali.
BBC inaelewa kuwa wanaharakati wa chama cha Labour wanaofanya kampeni katika uchaguzi wa rais wa Marekani wanafanya hivyo katika nafasi zao binafsi.
Chama cha Labour hakijatoa jibu rasmi.
Hasa, malalamiko hayo yanataja gazeti linaloripoti kuwa watu wanaohusishwa na chama cha Labour wamesafiri hadi Marekani kumfanyia kampeni Harris.
Malalamiko hayo yanadai “uingiliaji wa wazi wa Chama cha Labour, na kambi ya kampeni ya Harris imekubali michango isiyo halali ya kitaifa kutoka nje ya nchi.”
Polisi Ujerumani wavamia duka la pizza linalouza kokeini kisiri

Polisi wamevamia duka la pizza magharibi mwa Ujerumani ambalo wanadaiwa kuwahudumia wateja wa dawa ya kulevya ya kokeini pembeni wanapoagiza bidhaa nambari 40 kwenye menyu.
Mamlaka zilidokezwa kuhusu hilo mnamo mwezi Machi na wakaguzi wa chakula, na maafisa wa kikosi cha madawa ya kulevya walianza kufuatilia mgahawa huo, mkurugenzi wa uhalifu Michael Graf von Moltke alisema Jumatatu.
Wakati polisi walipokwenda kumkamata meneja wa mgahawa huo wa pizza nyumbani kwake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 aliripotiwa kurusha begi la dawa za kulevya nje ya dirisha, ambalo “lilianguka mikononi mwa maafisa wa polisi”, polisi wa Düsseldorf walisema.
Polisi walipata kilo 1.6 (lb 3.5) za dawa ya kokeini, 400g (14.1oz) za bangi na €268,000 (£223,120) pesa taslimu katika nyumba hiyo.
Israel yasema ilimuua aliyetarajiwa kumrithi Nasrallah

Jeshi la Israel linasema kuwa lilimuua kiongozi wa kidini aliyekuwa anadokezwa kumrithi aliyekuwa kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, katika shambulio la anga karibu wiki tatu zilizopita.
Hashem Safieddine alifariki katika mashambulizi ya anga kwenye viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kulingana na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).
Hezbollah, shirika lenye nguvu la Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon linalopigana na Israel, halijathibitisha kifo cha Safieddine.
Kiongozi wake wa awali, Nasrallah, aliuawa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Beirut tarehe 27 Septemba.
Baada ya mashambulio ya anga karibu na uwanja wa ndege wa mji huo tarehe 4 Oktoba, maafisa wa Hezbollah walisema wamepoteza mawasiliano na Safieddine, huku vyombo vya habari vya Marekani vikiwataja maafisa wa Israel wakisema mhubiri huyo ndiye aliyekuwa mlengwa wa shambulio hilo.
Milipuko mikubwa ilitikisa jiji usiku huo, ikiacha moshi mwingi ambao ungeweza kuonekana hadi asubuhi.
Siku ya Jumanne, IDF ilitoa taarifa ikisema Safieddine aliuawa pamoja na Ali Hussein Hazima, aliyeelezwa kama kamanda wa Makao Makuu ya Ujasusi ya Hezbollah, katika shambulizi la makao makuu ya kijasusi ya shirika hilo mjini Beirut.
Ilimshutumu Safieddine kwa kuelekeza “mashambulio ya kigaidi dhidi ya taifa la Israel” kwa miaka mingi, pamoja na kushiriki katika “michakato ya maamuzi makubwa” ya Hezbollah.
Hezbollah ni shirika la kijeshi, kisiasa na kijamii ambalo lina nguvu kubwa nchini Lebanon. Imetajwa kama shirika la kigaidi na Israel pamoja na Marekani, Uingereza na nchi nyinginezo.
Jeshi la DRC, limethibitisha kuchukuwa tena udhibiti wa mji wa #Kalembe, siku moja baada ya waasi wa #M23 kudai kuchukuwa usimamizi wa mji huo.
Msemaji wa Keshi la DRC ,Sylvain Ekenge, amesema jeshi la DRC, lilifanikiwa kukomboa Kalembe, ila bado kuna mapigano makali yanayoendelea katika maeneo ambayo hayana udhibiti wa jeshi la serikali.
Maktaba

Kocha wa Tunisia Faouzi Benzarti ‘atupiwa virago’
Timu ya Tunisia imevuna alama 7 tu baada ya michezo minne ya kufuzu michuano ya AFCON 2025.Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Tunisia Faouzi Benzarti./Picha: Wengine
Tunisia imemtimua kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Faouzi Benzarti baada ya kupoteza mchezo wao na visiwa vya Comoro, Shirikisho la Soka la nchi hiyo limesema siku ya Jumanne.
Benzarti, mwenye umri wa miaka 74, aliiongoza Tunisia kushika usukani wa kundi A kwenye michezo ya kufuzu AFCON 2025, licha ya kupoteza na baadaye kutoka suluhu ya 1-1 na timu ya taifa ya Comoro.
Benzarti alipewa mikoba ya timu ya taifa ya Tunisia mwezi Septemba, wakati wa michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2025), ambapo aliiongoza timu hiyo kushinda michezo miwili dhidi ya Madagascar na Gambia.
Kabla ya hapo, Benzarti aliwahi pia kuwa mkufunzi wa Tunisia kwa vipindi vitatu, yaani kwa mwaka 1994, 2010 na 2018 mtawalia.
Fainali za AFCON 2025, zitafanyika nchini Morocco kuanzia Disemba 2, 2025 hadi Januari 18, 2026.
Lori lililokuwa limesheheni mafuta lilipoteza muelekeo katika mji wa Kigogwa, kupinduka na kisha kulipuka na kuua watu takribani 10, kulingana na AFP.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la njia ya panda, lililo katika mji wa Kigogwa, kilomita 25 kutoka mji mkuu wa Uganda, Kampala siku ya Jumanne 22 Oktoba.
“Idadi ya watu walipoteza maisha hadi sasa ni 10, lakini kuna taarifa za majeruhi zaidi,“alisema Charles Lwanga, Mkuu wa Wilaya wa eneo hilo.
Kulingana na Lwanga, lori hilo lilipata hitilafu ya breki kabla ya kutokea kwa ajali hiyo.
KIPENGA CHA MICHEZO
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 23.10.2024

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi afanya mazungumzo na Manchester United, Sevilla wanataka kumsajili beki wa Tottenham Archie Gray kwa mkopo, Chelsea imemwambia Josh Acheampong hatacheza tena hadi asaini mkataba mpya.
Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi amefanya mazungumzo na Manchester United kuhusu uwezekano wa kuchukua nafasi ya Erik ten Hag. (Mail)
Sevilla wana nia ya kumsajili beki wa Tottenham mwenye umri wa miaka 18, Archie Gray kwa mkopo. (Mucho Deporte – kwa Kihispania)
Chelsea imemwambia mlinzi wa umri wa miaka 18 wa England Josh Acheampong kwamba hataichezea klabu hiyo kwa kiwango chochote tena hadi asaini mkataba mpya. (Athletic – Usajili unahitajika)

Beki wa Tottenham Archie Gray
Tottenham wameweka bei ya pauni milioni 80 kwa beki wa Uhispania Pedro Porro, 25, ambaye anawindwa na Manchester City. (Football Insider)
Brighton na Arsenal wanavutiwa na kipa wa Aston Villa wa Aston Villa mwenye umri wa miaka 21 raia wa Poland Oliwier Zych. (Telegraph – usajili unahitajika)
Kocha wa Arsenal wa timu ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18 Jack Wilshere, 32, atajiunga na Norwich kama mkufunzi wa kikosi cha kwanza wiki hii baada ya klabu hizo mbili kukubaliana ada ya fidia kwa kiungo huyo wa zamani wa Gunners. (Standard)
Graham Potter, David Moyes na Gareth Southgate wanatarajiwa kurithi mikoba ya Oliver Glasner iwapo atatimuliwa na Crystal Palace. (Guardian)
Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund Edin Terzic atawania kazi katika klabu ya West Ham iwapo The Hammers watamfukuza Julen Lopetegui. (Florian Plettenberg)
Dortmund wanataka kumsajili beki mwezi Januari huku mchezaji wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 Ben Chilwell na mchezaji wa kimataifa wa Hungary na Bournemouth Milos Kerkez, 20, wakijumuishwa kwenye orodha yao fupi. (Team Talk)
Wachezaji wakuu barani Ulaya henda wakakataa kutangaza Kombe la Dunia la Vilabu lililopanuliwa hivi karibuni kama sehemu ya mzozo kati ya vyama vya wachezaji na Fifa kuhusu kalenda ya soka iliyosongamana. (Times- usajili unahitajika)
Mpango wa Freidkin Group wa kuinunua klabu ya Everton unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba, lakini wamiliki hao wapya hawataidhinisha matumizi makubwa ya Januari kwa sababu ya vikwazo vya PSR. (The i – Usajili unahitajika)
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.