Mkutano wa mataifa ya BRICS unafanyika nchini Urusi kwa siku tatu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Baadhi ya viongozi wa dunia wanakutana katika mji wa Kazan nchini Urusi kwa ufunguzi wa mkutano wa mataifa ya BRICS, muungano wa kiuchumi unaoibuka ambao Kremlin inatarajia kwamba utatoa upinzani kwa mataifa ya Magharibi.

Mataifa ya China, Brazil na Afrika Kusini pamoja na India yanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.
Mataifa ya China, Brazil na Afrika Kusini pamoja na India yanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo. REUTERS – Maxim Shemetov

Kongamano la wiki hii ndilo kubwa zaidi tangu Urusi kutuma wanajeshi wake nchini Ukraine na linakuja pia wakati huu ambapo Rais wa Urusi,  Vladimir Putin akionekana  kutuma ujumbe kwa nchi za Magharibi kwamba juhudi zao za kuitenga nchi yake katika jukwa la kimataifa zimefeli.

Rais wa China Xi Jinping, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wote washirika muhimu wa Urusi wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.

Kongamano hilo linafanyika katika mji wa Kazan nchini Urusi kuanzia tarehe 22 hadi 24 ya mwezi huu wa Oktoba.

Rais Vladimir Putin analenga kutumia muungano huo kama mbadala wa mataifa ya Magharibi.
Rais Vladimir Putin analenga kutumia muungano huo kama mbadala wa mataifa ya Magharibi. AP – Alexander Zemlianichenko

Moscow imeonekana kupanua muungano huo wa BRICS unaojumuisha mataifa ya Brazil, Urusi yenyewe, IndiaChina na Afrika Kusini, ikitaka kuutumia kuendeleza ajenda zake katika nchi za kigeni.

Ajenda kuu ya kongamano hilo ni kutekeleza wazo la Rais Putin na kutaka nchi wanachama kutumia njia mbadala ya malipo kando na ile ya SWIFT, mfumo wa kimataifa wa benki ambao Urusi iliondolewa tangu mwaka wa 2022.

Suala la mzozo wa mashariki ya kati linatarajiwa kupia kujadiliwa kwenye kongamano linaloanza leo Jumanne. Kremlin pia inaona  kwamba muungano wa BRCIS utasaidia kutoa upinzani kwa mataifa ya Magharibi.

Rais wa Putin wa Urusi alikosa kuhudhuria kongamano la awali nchini Afrika Kusini baada ya hati ya kukamatwa kwake kutoka kwa ICC, Afrika kusini ikiwa mwanachama.
Rais wa Putin wa Urusi alikosa kuhudhuria kongamano la awali nchini Afrika Kusini baada ya hati ya kukamatwa kwake kutoka kwa ICC, Afrika kusini ikiwa mwanachama. AFP – IRINA MOTINA

Marekani kwa upande wake imetupilia mbali mawazo kwamba huenda BRICS ikatoa upinzani kwa nchi washirika wa Washington.

Moscow imekuwa ikionekana kupiga hatua katika uwanja wa mapambano mashariki kwa Ukraine mwaka huu wakati pia ikielezwa kuimarisha uhusiano wake na mataifa ya ChinaKorea Kaskazini pamoja na Iran, mataifa ambao hayapo katika uhusiano mwema na Marekani.

Mahakama ya ICC mwaka wa 2023 ilitoa hati ya kukamatwa kwa Rais Putin hatua ambayo ilimzuia kusafiri kwenda nchini Afrika Kusini mwanachama wa ICC kuhudhuria kongamano la awali.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment