Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Siku moja mfalme wa Babeli aliamua kumpandisha cheo Daniel na kumuheshimisha sana.
Cha ajabu, kwa haraka sana Daniel akaomba pia rafiki zake wa karibu (Shedrack, Meshack na Abednego) nao wapatiwe nafasi.
Kwa sababu Mfalme alimuheshimu na kumuamini sana Daniel…
…akafanya sawa sawa na ombi lake.
Hii ilimsaidia sana Daniel, kwa sababu kuna wakati alipata TISHIO la KUUWAWA…
…na wakati mwingine alisingiziwa KESI, hawa marafiki watatu ndio WALISIMAMA NAYE.
Wengine wote WALIMTENGA.
Nadhani moja ya mtihani MKUBWA sana kwenye maisha ni pale…
…UNAPOWAACHA wanaokupenda na kujizungushia na waliofuata MALI/UMAARUFU au CHEO Chako.
Kila unapopanda HATUA ya JUU, ni muhimu sana kuwakumbuka akina Shedrack wako.
Hawa ni watu ambao wanakujua, unawajua na mnashare MAONO na IMANI.
Daniel alijua, akipanda PEKE YAKE ni hatari kwa HATIMA YAKE.
Ukiinuliwa ofisini, kwenye Biashara, Kipaji, Uongozi n.k…
…Usisahau kuwainua na akina Shedrack pia.
NB: USIWASAHAU uliotoka nao CHINI kwa sababu ya ULIOKUTANA nao JUU.
Kama umejifunza kitu comment maneno “NIMEJIFUNZA KITU”
Muda wowote ukiwa tayari nikusaidie kutimiza malengo yako hizi ndio namna 4 ninazoweza kukusaidia.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.