Mapigano mapya yazuka Mashariki mwa DRC, wakati rais wa Angola akiongeza juhudi za kidiplomasia

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mapigano mapya yameripotiwa kati ya waasi wa M23 na wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku rais wa Angola, msuluhishi katika mgogoro wa DRC akiongeza juhudi za kidiplomasia ili kuhakikisha mazungumzo kati ya Rwanda na DRC yanazaa matunda.

Tangu M23 ilipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameteka maeneo makubwa ya eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye  utajiri wa madini.
Tangu M23 ilipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameteka maeneo makubwa ya eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye utajiri wa madini. AP – Moses Sawasawa

Duru kutoka mashariki mwa DRC zinabaini kwamba alfajiri ya siku ya Jumapili Oktoba 20, 2024, waasi wa M23 walikabiliana na wanamgambo wa Wazalendo na kuwajeruhi raia 14 wakiwemo vijana wawili.

Mapigano hayo mapya yanaoneakana kuvunja makubaliano ya usitishwaji mapigano ambayo yalikuwa yamedumu kwa wiki kadhaa. 

Wakati huo huo rais wa Angola João Lourenço ameongeza juhudi zake za kidiplomasia ili kupunguza mvutano kati ya DRC na Rwanda. Siku ya Jumamosi asubuhi, alikuwa na mazungumzo ya simu na Marais Félix Tshisekedi na Paul Kagame, majadiliano yaliyolenga hali ya usalama mashariki mwa DRC. Mazungumzoo haya mapya yanafanyika katika hali ambayo mahusiano kati ya Kinshasa na Kigali yanasalia kuwa ya wasiwasi, licha ya mchakato wa Luanda unaonuiwa kuleta amani katika eneo hili lenye vurugu.

Mazungumzo ya amani kati ya Kinshasa na Kigali yalikwama, lakini duru mpya ya mazungumzo imepangwa kufanyika mjini Luanda mwishoni mwa wiki ijayo.

Siku ya Alhamisi Oktoba 17 Waziri Mkuu wa Kongo, Judith Suminwa, alitangaza mjini Brussels, kwamba “kwa mara ya kwanza, Rwanda imekubali kuwasilisha mpango wa kuondoa zaidi ya wanajeshi 4,000”. Lakini Kigali inakanusha. Olivier Nduhungirihe, mkuu wa diplomasia ya Rwanda, alijibu vikali, na kuthibitisha kwamba Rwanda haijawahi kukubali kuondoa wanajeshi wake, iwe Luanda wala kwingineko.

Kauli zisizo na msingi wowote

Alikashifu matamshi haya kuwa hayana msingi wowote, akisisitiza kuwa ahadi hiyo haionekani popote katika majadiliano yaliyofanyika wakati wa mkutano wa tano wa mawaziri huko Luanda. Kutokana na mkanganyiko huu, macho yote sasa yanageukia timu ya usuluhishi.

Kufikia Oktoba 26, Angola inahitajika kuwasilisha dhana ya operesheni (Conops). Huu ni waraka wa kimkakati ambao lazima uzingatie maswala ya pande zote mbili. Nakala hii itawasilishwa kwa uchunguzi na wataalam wa Kongo na Rwanda wakati wa mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 30 huko Luanda.

Rwanda inadai kuwa kuwepo kwa kundi la Wahutu wenye msimamo mkali wa FDLR eneo hilo, ni tishio kwa usalama wake. Tangu M23 ilipoanzisha tena mashambulizi mwishoni mwa mwaka 2021, wameteka maeneo makubwa ya eneo hilo la mashariki mwa Kongo lenye  utajiri wa madini.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment