Lebanon: Mamia ya raia watoroka mji wa Beirut kutokana na mashambulio ya Israeli

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mamia ya wakazi kwenye mji wa Beirut nchini Lebanon, wamelazimika kukimbia maeneo yao baada ya mfululizo wa mashambulio ya Israel, wakati huu Tel Aviv ikianza pia kushambulia kile imesema ofisi za wafadhili wa kundi la Hezbollah.

Shambulio la Israeli kusini mwa mji wa Beirut, Lebanon, Jumapili, Oct. 20, 2024. (AP Photo/Hussein Malla)
Shambulio la Israeli kusini mwa mji wa Beirut, Lebanon, Jumapili, Oct. 20, 2024. (AP Photo/Hussein Malla) © Hussein Malla / AP

Wakati raia na mashirika ya kibinadamu yakiripoti milipuko mikubwa mjini Beiruti, jeshi la Israel pia lilianza kushambulia matawi ya taasisi zinazotuhumiwa kutoa fedha kwa kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.

Vyombo vya habari vya Lebanon, vimerekodi milipuko zaidi ya 11 kusini mwa mji mkuu Beirut, ambako ofisi za Al-Qard Al Hassan zililengwa sawia na matawi mengine kwenye eneo la bonde la Bekaa.

Moshi ukionekana karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut-Rafic Al Hariri baada ya shambulio la Israeli, huku kukiwa na uhasama unaoendelea kati ya Hezbollah na wanajeshi wa Israel, Oktoba 20, 2024. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Moshi ukionekana karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beirut-Rafic Al Hariri baada ya shambulio la Israeli, huku kukiwa na uhasama unaoendelea kati ya Hezbollah na wanajeshi wa Israel, Oktoba 20, 2024. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany © Mohamed Abd El Ghany / Reuters

Aidha baadhi ya mabomu yaliangushwa jirani na uwanja mkuu wa ndege mjini Beirut, njia kuu ya kupitisha misaada ya kibinadamu na unaotumika pia kuwaondoa raia wa kigeni waliokwama nchini humo.

Mashambulio haya yamejiri saa chache tangu Israel iagize raia kuondoka kwenye baadhi ya maeneo, wakati huu pia kundi la Hezbollah nalo likirusha mamia ya roketi kulenga kambi za kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika hatua nyingine tume ya walinda amani wa umoja wa mataifa walioko kusini mwa nchi hiyo, imesema Israel imeshambulia kwa makusudi baadhi ya maeneo yake muhimu.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment