Israeli: Hezbollah yalenga makaazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Israeli imesema ndege isiyokuwa na rubani ililenga makaazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu mjini Caesarea baada ya wapiganaji wa Hezbollah kurusha makombora kuelekea Israeli yakitokea katika nchi jirani ya Lebanon.

Vikosi vya usalama vya Israel vikiwa karibu na kizuizi kwenye barabara inayoelekea kwenye makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu huko Caesarea Oktoba 19, 2024.
Vikosi vya usalama vya Israel vikiwa karibu na kizuizi kwenye barabara inayoelekea kwenye makazi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu huko Caesarea Oktoba 19, 2024. © Jack Guez/AFP

Haya yanajiri wakati huu Israeli na yenyewe ikiripoti kutekeleza mashambulio kutokea kusini mwa nchi yake kuelekea katika Ukanda wa Gaza.

Watu 33 wameripotiwa kuuawa katika mashambulio hayo ya Israeli na usiku kucha katika mji wa Jabalia, kwenye ukanda wa Gaza kwa mujibu wa idara ya ulinzi ya Gaza.

Ofisi ya Waziri Mkuu Netanyahu imesema kiongozi huyo na mke wake hawakuwa katika nyumba yao mjini Caesarea wakati wa shambulio hilo la ndege isiyokuwa na rubani na kwamba hakuna majeruhi walioripotiwa.

Maafisa wa kitengo cha jeshi la Israel Home Front Command wakiwa mbele ya barabara inayoelekea kwenye makaazi ya Benjamin Netanyahu, ambayo serikali ya Israel inasema ililengwa na ndege isiyo na rubani kutoka Lebanon, huko Caesarea, Israel, Jumamosi, Oktoba 19 2024.
Maafisa wa kitengo cha jeshi la Israel Home Front Command wakiwa mbele ya barabara inayoelekea kwenye makaazi ya Benjamin Netanyahu, ambayo serikali ya Israel inasema ililengwa na ndege isiyo na rubani kutoka Lebanon, huko Caesarea, Israel, Jumamosi, Oktoba 19 2024. © Ariel Schalit / AP

Milio ya vingora vya usalama imesikika mapema leo Jumamosi nchini Israeli, wapiganaji wa Hezbollah kutoka nchini Lebanon wakirusha makombora katika sehemu tofauti.

Wapiganaji hao wanaoungwa mkono na nchi ya Iran wamethibitisha pia kurusha makombora katika kambi ya jeshi katika mji wa Haifa kaskazini mwa Israeli.

Kuelekea mwishoni mwa mwezi uliopita, Israeli iliongezeka kasi ya mashambulio yake nchini Lebanon pamoja na kuwatuma wanajeshi wa ardhini baada ya mashambulio ya karibia mwaka mmoja ya kuvuka mipaka.

Taarifa kutoka kwa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli inasema kiongozi huyo hakuwepo kwenye makazi yao wakati wa shambulio hilo.
Taarifa kutoka kwa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli inasema kiongozi huyo hakuwepo kwenye makazi yao wakati wa shambulio hilo. AP – Ariel Schalit

Katika Ukanda wa Gaza, mapigano yaliongezeka tena kufuatia mauaji ya kiongozi wa wapiganaji wa Hamas Yahya Sinwar, anayetuhumiwa kwa kupanga na kuongoza shambulio la tarehe saba ya mwezi Oktoba dhidi ya Israeli.

Ijumaa ya wiki hii, Hamas ilisisitiza kwamba haitowaachia huru mateka hadi pale ambapo vita vitaisha katika Ukanda wa Gaza.

Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ambaye nchi yake inaunga mkono wapiganaji wa Hamas, amesema kundi hilo halitomalizwa kufuatia kifo cha Sinwar kiongozi wake.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment