PAMBANA SONGA MBELE

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kipimo Kimojawapo Muhimu kujulisha kama utafika mbali ni…

…namna unavyokabiliana na WANAOKUCHUKIA na WANAOKUSEMA Vibaya.

Kuna watu hata ukiwa unafanya mazuri kiasi gani wataona upande wa “Negative” tu.

Kuna watu hata ukiwatendea mema mara ngapi wenyewe watakulipa ubaya tu na kukusema vibaya.

Siku zote kumbuka mtu ambaye hana Kitu kikubwa ndani yake hakuna mtu atajishughulisha kumshambulia.

Mtu ambaye ameganda tu sehemu moja hakuna atakayehangaika kumsema.

Ukiona yote haya yanatokea inamaanisha una KITU ndani YAKO.

Wakati mwingine hata hakijaonekana lakini ni kama kuna kitu kinawaambia “Ua ndoto yake”, “ya kesho yake”. n.k

Wengi wanaokupinga sio kwa sababu ya ULIVYO SASA HIVI bali ni kwa sababu ya VILE UTAKAVYOKUWA…

…ni kwa sababu ya KULE UNAKOELEKEA.

Kumbuka Yusufu alichukiwa na kaka zake kwa sababu ya NDOTO YA KUWA MTU MKUU…

…ingawa bado alikuwa MCHUNGA MBUZI.

Ndoto ndio inayowatisha, usishangae – Ni uthibibitisho kuwa UNA KITU KIKUBWA, Ni UTHIBITISHO kuwa UNAENDA MBALI.

Pambana, Songa Mbele.

Usifanye KOSA la kutumia MUDA MWINGi kushindana na kuwajibu watu wa namna hii.

CHANJA MBUGA.

Tumia Muda kusonga mbele, watakuja kushtuka UMESHABADILISHA VIWANGO.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment