Nigeria : Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko wa lori la mafuta yafikia 147

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa ajali ya moto ya lori la kubeba mafuta imefikia watu 147.

Ajali za lori za kusafirisha mafuta huripotiwa mara kwa mara nchini Nigeria kutokana na ubovu wa barabara.
Ajali za lori za kusafirisha mafuta huripotiwa mara kwa mara nchini Nigeria kutokana na ubovu wa barabara. REUTERS – ALAMIN MOHAMMED

Wengi wa waliofariki ni raia waliokimbia eneo la ajali kujizolea mafuta, baada ya lori hilo la mafuta kuanguka, kwa mujibu wa taarifa ya polisi, umati mkubwa wa watu ulifika kwenye eneo la mkasa kuyachota mafuta.

Lawal Shiisu Adam, msemaji wa polisi nchini Nigeria amesema watu wengine 100 wapo katika hali mahututi katika hospitali mbalimbali mjini Ringim, kwenye jimbo la Jigawa.

Dereva wa lori hilo hata hivyo hakuathirika na amekamatwa na polisi.

Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria yafikia 147.
Idadi ya watu waliofariki katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria yafikia 147. AP – Sani Maikatanga

Visa vya ajali za moto kutokana na malori ya kubeba mafuta nchini Nigeria vimekuwa vikiongozeka kutoka na kile kinahusishwa na hali mbaya ya barabara na magari mabovu.

Mwezi ulliopita watu wengine 59 walifariki kutokana na mkasa wa moto baada ya lori la kubeba mafuta kugongana na basi la abiria.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment