Kenya : Bunge la Seneti kuamua kuhusu mswada wa kutimuliwa kwa Naibu Rais

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Bunge la seneti nchini Kenya, baadaye leo jioni linatarajiwa kupiga kura ya ndio au la, ya kumuondoa afisini naibu rais Rigathi Gachagua, baada ya kuskiza hoja ya matumizi mabaya ya afisi ambayo tayari imeidhinishwa na bunge la kitaifa.

Rigathi Gachagua atakuwa naibu rais wa kwnzaa kuondolewa afisini iwapo hilo litafanyika tangu Kenya kujipatia katiba yake ya mwaka 2010.
Rigathi Gachagua atakuwa naibu rais wa kwnzaa kuondolewa afisini iwapo hilo litafanyika tangu Kenya kujipatia katiba yake ya mwaka 2010. © Monicah Mwangi – REUTERS

Gachagua anakabiliwa na mashtaka 11 ya matumizi mabaya ya afisi ikiwemo rushwa, kueneza siasa za kikabila na kuhujumu serikali.

Baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao hapo jana katika kikao kilichojawa majibizano makali kutoka kwa mawakili, hii leo itakuwa zamu ya Naibu Rais Rigathi Gachagua maarufu kama “Riggy G” kujitetea mbele ya maseneta.

Naibu Rais  Rigathi Gachagua amekanusha mashtaka yote 11 dhidi yake.
Naibu Rais Rigathi Gachagua amekanusha mashtaka yote 11 dhidi yake. © Andrew Kasuku / AP

Gachagua amekanusha mashtaka yote dhidi yake, akisema yamechochewa kisiasa baada ya uhusiano kati yake na rais William Ruto kudaiwa kuingia doa, hata hivyo huenda akaondolewa afisini iwapo bunge la Seneti litaidhinisha mashtaka dhidi yake.

Aidha naibu huyo wa rais  atakuwa na fursa  ya kujieteta mahakamani iwapo ataondolewa afisini na bunge.

Rigathi Gachagua atakuwa naibu rais wa kwanza kuondolewa afisini iwapo hilo litafanyika tangu Kenya kujipatia katiba yake ya mwaka 2010.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment