Afrika Leo Mchana

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari

  • Korea Kaskazini yalipua barabara kuu na leri inayoiunganisha na Korea Kusini ili “kutenganisha kabisa” nchi zote mbili
  • Israel yaushambulia mji mkuu wa Lebanon kwa mara ya kwanza baada ya siku tano
  • Tuchel akubali kuwa meneja ajaye wa England
  • Mahakama yakataa kuzuia kushtakiwa kwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua
  • Tazama: Shambulio la Israel lilivyopiga kambi ya mahema ya wakimbizi katika hospitali ya Gaza
  • Walioshuhudia shambulio la Israel kwenye hospitali ya Gaza waliona ‘watu wengi wakiungua’
  • Bunge la Seneti Kenya kuanza kusikiliza hoja ya kumuondoa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua
  • Marekani yaipa Israel siku 30 kuongeza msaada wa Gaza la sivyo itakuwa katika hatari ya kukatwa kwa msaada. 

Kesi ya kumuondoa Gachagwa yaanza kusikilizwa Seneti

Naibu Rais Rigathi Gachagua anakabiliwa na wakati mgumu wa kihistoria huku Bunge la Seneti lenye wanachama 67 likianza kusikiliza pendekezo la kuondolewa mamlakani.

Gachagua alifika katika bunge la Seneti Jumatano akiandamana na mawakili wake.

Nderitu Gachagua alinusurika Seneti 2016, hivyo Rigathi pia aombea nyota ishuke kumuokoa

Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye kakake, Gavana Nderitu alinusurika kutimuliwa 2016

FAMILIA ya Naibu Rais Geoffrey Rigathi Gachagua si geni kwa hoja ya kutimuliwa mamlakani katika Seneti kwa kuwa marehemu kakake James Nderitu alikabiliana nayo miaka minane iliyopita alipokuwa Gavana wa Nyeri.

Marehemu Gavana Nderitu, ambaye aliaga dunia kutokana na saratani ya kongosho mnamo Februari 24, 2017, alikuwa ameondolewa na madiwani 35 kati ya 47 wa Bunge la Kaunti ya Nyeri mnamo Septemba 2, 2016—na hivyo kufika Seneti kujitetea mnamo Septemba 15.

Miaka minane baadaye, kakake mdogo, Rigathi, anajitetea dhidi ya kuondolewa mamlakani kama Naibu Rais wa Kenya.

Bw Nderitu alipokuwa akijitetea Seneti, alikuwa na umri wa miaka 62, Rigathi amefika katika Bunge hilo kujitetea akiwa na umri wa miaka 59.

Japo Bw Nderitu alitakaswa makosa yoyote na Seneti, hatima ya Bw Rigathi haijulikani, huku wafuasi wake wakisubiri matokeo baada ya maseneta kupiga kura Alhamisi.

Ndugu hao wawili walizaliwa katika kijiji cha Hiriga Kaunti ya Nyeri wakiwa watoto wa Bw Gachagua Reriani na Martha Kirigo—wapiganiaji wa uhuru wa Mau Mau katika msitu wa Mlima Kenya.

Baba yao alipokuwa akiwahudumia askari wa Mau Mau, mama yao alisaidia kuwalisha kwa siri, pamoja na kuwapelekea silaha.

Kulingana na Gavana wa Nyeri Mutahi Kahiga, “hii ni familia ambayo ilibarikiwa kuwa na talanta za uongozi lakini inavyotarajiwa, maadui wa baraka hiyo wamekuwa wakijaribu kuiangamiza”.

Bw Kahiga mnamo Oktoba 16, 2024 aliambia Taifa Leo kuwa “kama baba wa sasa wa Kaunti ya Nyeri, naweza kuapa kwamba hakuna ubaya katika familia ya Gachagua, ni kwamba nyota yake ya uongozi inatatizwa na wale wanaofurahia kuangusha talanta.”

Nderitu alitimuliwa na bunge la kaunti yake, kufuatia hoja iliyowasilishwa na diwani wa Mathari Baragu Mutahi.

Kuhusu kuondolewa kwa mashtaka ya Rigathi, Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse aliwasilisha Oktoba 1, 2024 akiibua mashtaka 11, na wabunge 291, wakiwemo takriban wabunge wote kutoka eneo la Mlima Kenya, waliungana dhidi yake.

Kabla ya kuondolewa mamlakani, Bw Nderitu aliomba msamaha wakazi wa Nyeri kwa kuruhusu suala hilo kuzidi hadi kuwa mjadala wa kitaifa.

Kadhalika, Bw Rigathi, ameomba msamaha kwa Rais William Ruto, Bunge na wananchi wa Kenya kwa mchakato wa kumuondoa mamlakani.

Hata hivyo, maombi yote mawili ya msamaha, hayakufanya kazi na michakato ya kuwashtaki ilifikia Seneti.

Mnamo Septemba 15, 2016, Bw Nderitu alikabiliana na Seneti ambapo iliamuliwa kuwa mashtaka dhidi yake hayajatimiza kiwango cha kuondolewa mamlakani.

Alikuwa ameshutumiwa kwa kumteua Alice Wachira kama kaimu Katibu wa Kaunti licha ya, kulingana na  madiwani, hakutimiza mahitaji ya majukumu ya kazi hiyo.

Bunge lilikuwa limependekeza kutimuliwa kwake ofisini mnamo Julai 2016 kwa misingi kwamba hakuwa ametimiza sifa zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na kukosa uzoefu wa miaka 10 katika nafasi ya usimamizi.

Vile vile, madiwani walikuwa wamedai kwamba Bw Nderitu alikuwa amefuja Sh1.7 bilioni.

Wawakilishi hao wa wadi pia walikuwa wamemlaumu gavana huyo kwa kukiuka Katiba kwa kuendesha kaunti bila Baraza la Mawaziri, huku wakidai kuwa serikali yake ilitenga Sh740 milioni kutoka kwa maendeleo hadi shughuli za kawaida bila kufuata utaratibu uliowekwa.

Seneti ilipata madai hayo kuwa hayakuthibitishwa.

Huku Rigathi akikabiliana na Seneti, na kusubiri uamuzi wake Alhamisi, atakuwa na matumaini ya kuwa na bahati ya marehemu kaka yake itamuokoa.

Miongoni mwa madai ya Mutuse ni kwamba Bw Rigathi alihujumu wosia wa Nderitu wa kuwanyima warithi halali wa mali ya marehemu, jambo ambalo limeshuhudia wosia wa kibinafsi ‘kufichuliwa’ na kuwa hati ya umma.

“Kimsingi, Wosia wa marehemu ni miongoni mwa sababu zilizowasilishwa kushinikiza kuondolewa kwa naibu rais…hivyo aombe kwa bidii ili roho ya kaka yake ishuke na kusimama naye kwenye dhoruba inayomkumba,” anasema Wakili wa Mahakama Kuu Timothy Kariuki.

Uhusika wa Orengo katika kikosi cha mawakili wa Bunge wapingwa na Gachagua

Seneta James Orengo (kulia) aongoza upande wa mashtaka dhidi ya Rigathi Gachagua katika Seneti. Picha|Hisani

MAWAKILI wawili wandani wa Raila ambao ni viongozi waliochaguliwa, wamejiunga na kesi ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua wakiwakilisha Bunge la Kitaifa katika kikao cha Seneti.

Wakili James Orengo ambaye ni Seneta wa Siaya na mbunge wa Rarieda Otiende Omollo wameungana na, Paul Nyamodi, Erick Gumbo, Muthomi Thiankolu, Moses Kipkogei, Peter Wanyama, Ken Melly, Mwangi Kang’u, George Murugara, Samwel Chepkonga, John Makali na  Zamzam Mohamed kuwakilisha Bunge la Taifa.

Bw Murugara, Bw Chepkonga, Bw Makali na Bi Mohammed pia ni wabunge.

Upande wa Bw Gachagua unaongozwa na Wakili Paul Muite, Elisha Ongoya, Tom Macharia, Swanya Victor, Ndegwa Njiru, Faith Waigwa, Amos Kisilu, John Njomo, George Wandati Andrew Muge, Julia Omwamba, Eric Naibei na Willis Echesa.

Tayari, mawakili wa Bw Gachagua wamepinga uwepo wa Bw Orengo kuwakilisha Bunge la Taifa.

Bw Njiru alisema suala kama hili liliibuliwa wakati wa hoja ya kumtimua aliyekuwa naibu gavana wa Kisii Robert Monda na kwamba mahakama kuu iliamua kuwa mtu aliye katika kazi ya kuajiriwa hawezi kuwakilisha upande wowote mbele ya bunge.

Spika Kingi atafanya uamuzi baada ya Gachagua kusomewa mashtaka.

Maseneta nao wafuata ‘tabia’ ya wabunge

Kikao cha Seneti kikiendelea. Maseneta wameonekana kufuata mkondo wa wenzao wabunge wa kitaifa kwa kukosekana kazini wakati wa mijadala kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Picha|Maktaba

SENETI Jumanne ilizamika kuahirisha kikao chake kutokana na ukosefu wa idadi hitajika ya maseneta 15 jinsi inavyoamrishwa kwenye katiba.

Seneti ina maseneta 67 na idadi inayohitajika kuendesha shughuli zake ni maseneta 15 na zaidi. Kwa mujibu wa katiba, Bunge la Kitaifa nalo lazima liwe na wabunge 50 au zaidi ili kuendelea na vikao vyake.

Hii ni kinyume na mnamo Jumatatu ambapo maseneta walifika wote wakati wa kujadili hoja ya kumtimua Gavana wa Kericho Erick Mutai.

Kukosekana kwa idadi inayofaa ya maseneta kulitokea wiki moja baada ya Bunge la Kitaifa nalo kulazimika kutoendelea na vikao vyake kwa kuwa wabunge hawakuwepo.

Kinaya ni kuwa wakati wa kujadili na kuipigia kura hoja ya kumtimua Naibu Rais Rigathi Gachagua, wabunge 326 walikuwepo.

Siku hiyo hata kengele ambayo Naibu Spika Gladys Shollei aliamrisha ipigwe haikusaidia kitu kwa sababu wabunge hawakuwepo.

Jana, seneti ilifuata mkondo, kwa kuwa kulikuwa na chini ya maseneta 10 wakati wa kikao cha asubuhi. Licha ya Naibu Spika Kathuri Murungi kuamrisha kengele ipigwe kuwaamrisha maseneta waje kikaoni, bado idadi hitajika haikufika.

“Waheshimiwa maseneta, kutokana na kutotimia kwa idadi hitajika ya maseneta, naahirisha kikao hadi saa 2.30 leo (jana),” Bw Murungi akasema akiahirisha kikao cha jana.

Seneti ilikuwa imeorodhesha kusomwa kwa hoja 14 na miswada mitatu. Pia kulikuwa na miswada mitatu ambayo ilikuwa iangaziwe kwa sababu ilipendekezewa ifanyiwe marekebisho.

Miswada hiyo ilikuwa ni Mswada wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa 2023 na Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi, ambayo inadhaminiwa na Seneta wa Kericho Aaron Cheruiyot.

Pia kulikuwa na Mswada wa Kuzuia na Kudhibiti Saratani 2023 ambao unadhaminiwa na Seneta wa Nandi Samson Cherarkey.

Miswada mingine ambayo ilikuwa iangaziwe ni Usimamizi wa Fedha za Umma (Seneta Hamida Kibwana), Huduma za Dharura za Uokoaji wakati wa Moto 2023 (Mohamed Abass) na Uchukuzi wa Umma 2023 (Bonny Khalwale).

Miswada mitatu kuhusu Ripoti ya Maridhiano Nchini (NADCO), Mswada wa Vyama vya Kisiasa na Mswada wa Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi 2024 pia ilikuwa iangaziwe.

Kulikuwa na ripoti kadhaa za uchunguzi kutoka kwa kamati ambazo zilikuwa ziwasilishwe.

Kati ya ripoti hizo ni uajiri katika idara mbalimbali za serikali, kurefushwa kwa mikataba ya ununuzi na kusambazwa kwa kawi nchini, ripoti kuhusu mlipuko wa gesi Embakasi na pia kudadavuliwa kwa ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya fedha kwenye kaunti.

Hatua ya wabunge na maseneta kukosa kufika bungeni inaonyesha kuwa hawachukulii kwa uzito kazi zao.

Mwaka jana Bw Cheruiyot aliwachemkia maseneta, akisema anashangaa kwa nini wanapigania wachaguliwe kisha mwishowe wanatelekeza majukumu yao waliyopewa na Wakenya.

Korea Kaskazini yalipua barabara kuu na reli inayoiunganisha na Korea Kusini ili “kutenganisha kabisa” nchi zote mbili

g

Korea Kaskazini imelipua sehemu kadhaa za barabara na njia za reli zilizoiunganisha na Korea Kusini na vilipuzi siku ya Jumanne.

Miundombinu hii iliyopo katika sehemu ya kaskazini ya mpaka wa kijeshi, zilikuwa zimeundwa hapo awali kwa nia ya kuunganishwa nchi hizo tena siku zijazo na hazikufunguliwa kamwe kwa ajili ya safari.

g
Maelezo ya picha,Milipuko hiyo mikubwa iliharibu barabara na reli kadhaa kwenye mpaka baina ya nchi mbili

Tukio hilo lilitokea wakati wa mvutano uliosababishwa na malalamiko ya pande zote mbili.

Korea Kaskazini, ambayo tayari ilikuwa imeendeleza mpango wake siku zilizopita wa kuharibu barabara ili “kuzitenganisha kabisa” nchi zote mbili, iliishutumu Kusinikupelekandege zisizo na rubani katika eneo lake kueneza propaganda.

Kim Yo Jong, dada yake kiongozi Kim Jong-un, alitoa onyo la kulipiza kisasi dhidi ya nchi hiyo jirani, akionya kwamba “italipa gharama kubwa” kwa madai ya mashambulizi ya anga.

Israel yaushambulia mji mkuu wa Lebanon kwa mara ya kwanza baada ya siku tano

c

Usiku kucha kuamkia leo, Israel imefanya ashambulizi ya anga kwenye viunga vya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon, Beirut. Hii ni mara ya kwanza kwa mji mkuu kulengwa kwa kipindi cha karibu wiki.

Israel imesema imepiga ghala la chini la ardhi linalotumiwa na Hezbollah kuhifadhi silaha. Wakati huo huo, inasema roketi 50 zilirushwa kuelekea mji wa Safed kaskazini mwa Israel usiku kucha.

Mashambulizi ya mjini Beirut yamekuja baada ya mamlaka ya Lebanon kuripoti kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yaliwaua watu kote mashariki na kusini mwa nchi.

Haya yanajiri baada ya Israel kutoa agizo lake la kwanza la kuuhama mji wa Dahieh katika muda wa wiki moja, na kuwaamuru wakaazi kuondoka eneo moja huko Harek Hreik.

Baada ya kulishambulia jiji hilo kwa mashambulizi ya kila siku na kutoa amri kadhaa za kuhama, Israel ilisitisha mashambulizi mjini Beirut wiki iliyopita, ingawa operesheni yake ya ardhini kusini mwa Lebanon, na mashambulizi ya anga katika maeneo mengine ya nchi, yaliendelea.

Tuchel akubali kuwa meneja ajaye wa England

c
Maelezo ya picha,Thomas Tuchel aliondoka Baynern Munich mwezi Mei baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kushindwa kushinda taji la Bundesliga

Kocha wa zamani wa Chelsea Thomas Tuchel amekubali kuwa meneja ajaye wa Uingereza.

BBC imeambiwa na vyanzo viwili tofauti kwamba Mjerumani Tuchel atakuwa meneja wa tatu wa kudumu asiye Mwingereza wa timu ya wanaume ya Uingereza baada ya Sven-Goran Eriksson na Fabio Capello.

Uingereza imekuwa bila meneja wa kudumu tangu Gareth Southgate ajiuzulu kufuatia kushindwa kwa Three Lions kwenye fainali ya Euro 2024 dhidi ya Uhispania.

Lee Carsley, ambaye Chama cha Soka kilimteua kwa muda, atasalia katika nafasi yake kwa mechi mbili za mwisho za Ligi ya Mataifa ya Uingereza dhidi ya Ugiriki na Jamhuri ya Ireland mnamo Novemba, huku Tuchel akitarajiwa kuchukua rasmi baada ya hapo.

Utambulisho rasmi wa Tuchel unatarajiwa kufanyika Jumatano huko Wembley.

Lengo lake kuu litakuwa kuiongoza England kupitia kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 ambalo litafanyika Marekani , Canada na Mexico.

Tuchel si mgeni katika la Uingereza akiwa ameiongoza Chelsea kati ya Januari 2021 na Septemba 2022.

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 51 alinyanyua mataji kama vile Champions League, Kombe la dunia la Fifa na Uefa Super Cup akiwa na The Blues kabla ya kutimuliwa.

Mahakama yakataa kuzuia kushtakiwa kwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua

g

Jopo la majaji watatu katika Mahakama Kuu liiliyoundwa kusikiliza maombi ya kutaka kusimamisha kesi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua imekataa kusitisha mchakato wa Seneti.

Wakati ikitoa uamuzi wake, jopo hilo lilioundwa na Jaji Mkuu Martha Koome kusikiliza maombi matano ya kuzuia kushtakiwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Wakati wakitoa uamuzi wao, jopo hilo liliyataja mashitaka hayo kuwa ya mapema na ya kutarajiwa na kuongeza kuwa yangeathiri kanuni za mgawanyo wa madaraka.

“Ni maoni yetu kwamba hii sio kesi moja ambapo uingiliaji kati ni wa moja kwa moja. Masuala yaliyoibuliwa na wahusika yatatakiwa kuhojiwa kwa hivyo tunaona kwamba utekelezaji wa kanuni ya kikatiba ya mgawanyo utazingatiwa utazingatiwa vyema kwa kukataa ombi hilo katika hatua hii,” ilisema.

Hata hivyo jopo hilo lilieleza kuwa Gachagua naweza kufika mahakamani pindi mchakato utakapokamilika.

f

Tazama: Shambulio la Israel lilivyopiga kambi ya mahema ya wakimbizi katika hospitali ya Gaza

Maelezo ya video,Tazama: Shambulio la Israel lilivyopiga kambi ya mahema ya wakimbizi katika hospitali ya Gaza

Madaktari wa Palestina wanasema shambulizi la anga la Israel limepiga kambi moja ndani ya hospitali ya Al-Aqsa iliyopo Gaza.

Picha kutok shirika la habari la Reuters zinaonyesha watu wakizima moto katika kambi ya Wapalestina waliokimbia makazi yao.

Takriban watu wanne waliuawa katika hospitali ya mji wa Deir Al-Balah, madaktari wanasema.

Jeshi la Israel limesema liliwashambulia wanamgambo waliokuwa wakiendesha shughuli zao kutoka katika kituo cha amri ndani ya eneo hilo la hospitali.

Walioshuhudia shambulio la Israel kwenye hospitali ya Gaza waliona ‘watu wengi wakiungua’

g

Tahadhari huenda taarifa hii ikawasumbua baadhi ya watu

Mashahidi wa shambulizi la anga la Israel lililosababisha moto kwenye kambi ya hema katika eneo la hospitali ya Gaza wameishirikisha BBC hofu yao na namna walivyokosa la kufanya walipowaona watu wakijeruhiwa na kufariki kwa kuunguzwa na moto huo.

Mama mmoja aliliita “moja ya matukio mabaya zaidi ambayo tumeshuhudia”, huku msichana aliyejeruhiwa akisema alisikia watu wakipiga mayowe wakati watu walipokuwa wakibomoa hema lao kujaribu kuwatoa nje.

Mwanaume mmoja alisema “amevunjika moyo” kwani “hakuweza kufanya chochote” kusaidia wale walioungua hadi kufa.

Shambulio hilo lilipiga katika eneo la hospitali ya al-Aqsa iliyopo katika mji wa Deir al-Balah, katikati mwa Gaza, mapema Jumatatu, na kuwasha moto ulioteketeza makazi ya muda ya watu waliokimbia makazi yao.

Takriban watu wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.

BBC imethibitisha eneo la video inayoonyesha mtu ananayewaka moto. Video nyingine zilionyesha watu wakikimbia kuzima moto huku kukiwa sauti za mayowe zikisikia na milipuko ikituma ikirusha miali ya moto angani usiku huo.

Jeshi la Israel lilisema lilikuwa likiwalenga wapiganaji wa Hamas wanaoendesha shughuli zao ndani ya kituo cha miongozo ya kijeshi katika maegesho ya magari, ambapo moto ulizuka “huenda kutokana na milipuko ya pili”. Jeshi lilisema tukio hilo linachunguzwa.

Marekani yaipa Israel siku 30 kuongeza msaada wa Gaza la sivyo itakuwa katika hatari ya kukatwa kwa msaada wa kijeshi

g
Maelezo ya picha,Marekani inasema Wapalestina milioni 1.7 waliojaa katika eneo la al-Mawasi wako katika “hatari kubwa kufariki”

Marekani imeiandikia Israel barua, ikiipa siku 30 kuongeza ufikiaji wa misaada ya kibinadamu Gaza lasivyo ikabiliwe hatari ya kukatwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani.

Barua hiyo iliyotumwa siku ya Jumapili, ni onyo kali zaidi linalojulikana kwa maandishi kutoka kwa Marekani kwa mshirika wake na inakuja huku kukiwa na mashambulizi mapya ya Israel kaskazini mwa Gaza ambayo yameripotiwa kusababisha idadi kubwa ya vifo vya raia.

Inasema Marekani ina wasiwasi mkubwa kuhusu kuzorota kwa hali ya kibinadamu, na kuongeza kuwa Israel imekataa au kuzuia karibu asilimia 90 ya shughuli za kibinadamu kati ya kaskazini na kusini mwezi uliopita.

Israel inapitia barua hiyo, afisa mmoja wa Israel aliripotiwa akisema, akiongeza kuwa nchi hiyo “inachukulia suala hili kwa uzito” na inakusudia “kushughulikia maswala yaliyotolewa” na Marekani

Israel imesema hapo awali inawalenga wapiganaji wa Hamas kaskazini mwa nchi na haijazuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu.

Siku ya Jumatatu, shirika la kijeshi la Israel linalohusika na usimamizi wa vivuko vya Gaza, Cogat, lilisema malori 30 yaliyokuwa yamebeba msaada kutoka shirika la mpango wa chhakula duniani yaliingia kaskazini mwa Gaza kupitia kivuko cha Erez.

Marekani ndiyo nchi inayosambaza silaha nyingi zaidi kwa Israel, na jeshi la Israel limekuwa likitegemea zaidi ndege zinazotolewa na Marekani, mabomu, makombora ya masafa na mizinga ili kupigana vita dhidi ya Hamas huko Gaza katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

-Mashariki ya Kati: Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, amemuonya Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kwamba Tehran iko tayari kwa “jibu kali na la kujutia” ikiwa Israel itaishambulia nchi yake kulipiza shambulizi la makombora siku kadhaa zilizopita. Jamhuri hiyo ya Kiislamu ilirusha makombora karibu 200 dhidi ya Israel mnamo Oktoba 1, kulipiza mauaji ya washirika wake wawili, kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh, na kiongozi wa HizbullahHassan Nasrallah, pamoja na Jenerali wa Iran.

-Diplomasia: Umoja wa Ulaya unafanya mkutano wake wa kwanza na mataifa ya Ghuba leo hii Jumatano mjini Brussels. Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuongeza msukumo wa kidiplomasia unaolenga kuwasogeza karibu zaidi washirika wa nchi za Kiarabu. Mkutano huo pia unalenga kuuongeza nguvu uhusiano wa pande hizo mbili ili uwe wa kimkakati zaidi na hatua hiyo ni kwa sababu Umoja wa Ulaya unatambua ushawishi wa nchi hizo hasa katika migogoro ya Mashariki ya Kati na Ukraine. Nchi hizo ni Bahrain, Kuwait, Oman, Qatar, Saudi Arabia and the Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

-Tanzania: Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kuondoa hali ya kuzorota kwa haki za binaadamu kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 2024. HRW imesema kuwa tangu mwezi Juni mamlaka imekuwa ikiwamakata kiholela mamia ya wafuasi ya upinzani, kuzuia mitandao ya kijamii, kupiga marufuku vyombo binafsi vya habari, na imekuwa ikihusishwa na utekaji nyara na mauaji ya kiholela ya wakosoaji wanane wa serikali.

-Kiongozi wa chama cha Wiper nchini Kenya Kalonzo Musyoka akana taarifa za kampuni ya Adani kutoka India, kufadhili kampeni za kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, mwaka wa 2012.

Wakati huo Kalonzo alikuwa mgombea mwenza wa Raila kuwania kiti cha Urais.

Aidha amesema amemshauri seneta wa chama chake, Dan Maanzo, kumuomba radhi Raila Odinga ambae ni kiongozi wa Muungano wa Azimio.

Hapo awali seneta huyo amemtuhumu Raila kufadhiliwa na Adani.

90 wamefariki katika mlipuko wa lori la mafuta nchini Nigeria

Lori hilo lilianguka katika mji wa Taura na watu wakakimbia kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika.Lori hilo lilipinduka barabarani kabla ya kulipuka. Picha / wengine 

Takriban watu 90 wameuawa, na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa, na mlipuko mkubwa wa lori la mafuta katika jimbo la kaskazini magharibi la Jigawa nchini Nigeria, polisi wa eneo hilo wamesema.

Meli hiyo ilipinduka katika mji wa Taura na watu wakakimbia kuchota mafuta yaliyokuwa yakimwagika.

Ilikuwa inasafiri kutoka Kano kuelekea mji wa Nguru katika jimbo la Yobe.

”Takriban watu 94 walikufa. Waliungua kiasi cha kutotambulika na wengine 50 wamehamishwa kwa matibabu katika mji wa Ringim,” DSP Lawan Shiisu Adam, msemaji wa polisi katika jimbo la Jigawa, aliwaambia waandishi wa habari.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment