Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kuna hatua fulani kwenye maisha yako utatakiwa uwe tayari kupigana “Vita ya Nafasi”.
Ni hivi, kuna kitu unakitaka ila hakitakufuata.
Kuna jambo unalitaka ila halitakuja kirahisi, ni lazima ulipiganie.
Miaka mingi sana iliyopita, mentor wangu aliwahi kuniambia, “You can’t Conquer what you don’t confront ”.
Yaani hauwezi kukishinda kile ambacho haukikabili.
Unaweza kudhani kuwa kwa sababu ya wema, ukarimu na upole basi kila unachohitaji utakipata.
Sio kweli, mambo makubwa yote kwenye maisha yanahitaji ujasiri wa kupambana.
Usipopambania unachokitaka utaishia kupata usichotaka.
Usipopigania malengo yako utaishia kutazama wengine wanatimiza ya kwao.
Kama ukikata tamaa basi Leo anzisha upya vita Tena.
“No retreat, No surrender” – Hakuna kurudi nyuma, hakuna kujisalimisha, hadi ndoto yako itimie.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.