Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mataifa ya India na Canada yamewafukuza wanadiplomasia wao, kutokana mzozo unaoendelea ambapo canada inatuhumu India kwa kutekelza mauwaji ya Hardeep Singh Nijjar, kiongozi wa vuguvugu linaloshinikiza kujetenga kwa Sikh, katika ardhi ya canada.

Waziri mkuu wa Canada, Justin Trudeau amesema canada imelazimika kuwatimua wanadiplomasia wa India nchini mwake baada ya taarifa kuonesha kuwa mawakala wa India walihusika moja kwa moja na kifo cha Hardeep Singh Nijjar.
Polisi wa Canada pia wanawatuhumu mawakala wa India kwa kuhusika na visa vya utekaji wa wanachama wa vuguvugu la Sikh, wanaoishi nchini Canada.
Hata hivyo India imekanusha madai hayo ya Canada na Kusema waziri mkuu Justin Trudeu anatafuta ushawishi wa kisiasa kupitia vuguvugu la Sikh.
India imekuwa ikituhumu kundi la Sekh kwa kujihusisha na visa vya kihalifu na kulitaja kuwa kundi la kigaidi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.