Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Ukraine imekanusha ripoti za vyombo vya habari siku ya Jumatatu kwamba inahusika na kuwahami waasi wanaopigana kaskazini mwa Mali na ndege zisizo na rubani.

Kwa mujibu wa gazeti la nchini Ufaransa la Le Monde, wapiganaji wa Tuareg katika taifa hilo la Afrika Magharibi, wanatumia ndege zisizo na rubani kutoka nchini Ukraine ambapo pia wanapata msaada kutoka kwa Kyiv.
Katika ripoti hiyo, wapiganaji hao wanatumia ndege hizo katika mapambano yao dhidi ya jeshi la Mali pamoja na mamluki wa Urusi, Wagner wanaodaiwa kuwasaidia wanajeshi wa serikali ya Mali.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Ukraine imekanusha vikali ripoti hiyo ya gazeti la Le Monde ikijitenga na mpango wowote wa kuwahami wapiganaji kaskazini mwa Mali.
Mali, ambayo ilikabiliwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 2020 na 2021, inapambana na makundi yenye silaha, mapigano mazito yakiripotiwa dhidi ya waasi wa Tuareg karibu na mpaka wa Mali na Algeria.

Mwezi Agosti, Mali ilitangaza kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi ya Ukraine kufuatia matamshi ya kyiv kwamba waasi walikuwa wamepata taarifa muhimu katika shambulio ambalo wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa Wagner waliuuawa kaskazini mwa nchi.
Urusi katika siku ya hivi karibuni imekuwa ikiimarisha juhudi zake za kupata ushawishi barani Afrika ikiwemo nchini Mali.
Moscow pia imeituhumu Ukraine kwa kuanzisha vita vingine dhidi yake kwa kuwaunga mkono wapiganaji inaosema wanapatikana katika mataifa rafiki wa Urusi barani Afrika.
Urusi imekuwa katika vita na nchi ya Ukraine tangu mwezi Februari mwaka wa 2020, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, wengi wao wakiwa ni raia wa Ukraine.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.