Kenya: Mahakama kuamua kuhusu kesi inayolenga kumtimua naibu rais

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mahakama nchini Kenya inatarajiwa hii leo kutoa uamuzi wake katika kesi inayolenga kulizuia bunge la senate kujadili na kupiga kura kuhusiana na mswada unaolenga kumtimua naibu wa rais Rigathi Gachagua.

Mahakama kuamua kuhusu kesi inayolenga kumtimua naibu rais Rigathi Gachagua
Mahakama kuamua kuhusu kesi inayolenga kumtimua naibu rais Rigathi Gachagua © Andrew Kasuku / AP

Katika tukio la kihistoria wiki iliopita, bunge la kitaifa lilipiga kura kumtimua Gachagua anayekabiliwa na makosa 11 ikiwemo ufisadi.

Gachagua mwenye umri wa miaka 59 amekanusha madai yote na kwa sasa ataendelea kuhudumu katika wadhifa wake hadi pale ambapo bunge la senate litaidhinisha kutimuliwa kwake.

Naibu huyo wa rais aliwasilisha kesi mahakamani akitaka bunge la Senate kujadili mswada huo siku ya Jumatano na Alhamis, akidai kwamba mpango huo haukufuata sheria na ulifanywa kwa haraka bila ya kuzingatia matakwa yote.

Mswada huo wa kumtimua naibu rais utahitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya maseneta ili kupita.
Mswada huo wa kumtimua naibu rais utahitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya maseneta ili kupita. © LUIS TATO / AFP

Jaji wa Mahakama kuu Enock Chacha anatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusiana na kesi hiyo saa nane na nusu kwa saa za Nairobi.

Hii inakuwa kesi ya kwanza katika historia ya Kenya inayohusu kutimuliwa kwa naibu wa rais tangu kuzinduliwa kwa katiba mpya mwaka wa 2010.

Siku ya Jumatatu Jaji Mkuu Martha Koome aliuunda japo la majaji watatu wanaotarajiwa kusikiliza kesi hiyo iliyoounganishwa na nyengine sita.

Rais Wiliam Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua baada ya kukabidhiwa cheti cha kushinda uchaguzi nchini Kenya, Agosti 15, 2022
Rais Wiliam Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua baada ya kukabidhiwa cheti cha kushinda uchaguzi nchini Kenya, Agosti 15, 2022 © citizen tv

Gachagua, mfanyabiashara mkubwa kutoka kabila la Wakikuyu, mojawapo ya makabila makubwa zaidi katika taifa hilo la Afrika Mashariki, kabla ya kuteuliwa kuwa naibu rais alikabiliwa na kashfa nyengine za ufisadi ambazo zilitupiliwa mbali baada yake kuchaguliwa kuhudumu katika wadhifa huo.

Katika wiki za hivi majuzi, amelalamikia kutengwa na rais na wandani wake na alikuwa akishutumiwa kwa kuunga mkono maandamano ya kupinga serikali yaliyoongozwa na vijana yaliyoshuhudiwa mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yakijiri, rais Ruto hajazungumzia hadharani kuhusu kuondolewa madarakani kwa naibu wake.Mswada huo utahitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya maseneta ili kupita.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment