Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Cameroon Paul Biya (kulia) akiwa na mkewe Chantal katika hafla iliyopita. Rais huyo hajaonekana hadharani kwa muda jambo lililozua gumzo kuhusu hali yake ya kiafya. Picha|Maktaba
SERIKALI ya Cameroon imepiga marufuku vyombo vya habari kupeperusha taarifa zozote kuhusu afya ya Rais Paul Biya, kufuatia uvumi kuhusu kifo chake.
Waziri wa Masuala ya Ndani Paul Atanga Nji aliwaambia magavana wa majimbo kwamba taarifa hizi “zimeibua wasiwasi na kuvuruga utulivi miongoni mwa raia wa Cameroon.”
“Kwa hivyo mjadala wowote katika vyombo vya habari kuhusu hali ya afya ya Rais umepigwa marufuku,” akasema.
Waziri Nji alionya kuwa “yeyote atakayevunja agizo hilo atakabiliwa vikali kwa mujibu wa sheria.”
Biya, 91, amesalia mamlakani kwa zaidi ya miongo minne (miaka 43).
Kiongozi huyo hajaonekana hadharani tangu Septemba 8, alipohudhuria mkutano katika ya China na Marais wa Afrika.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.