Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Shirikisho la mpira wa miguu nchini Nigeria (NFF) limesema litawarejesha nchini humo wachezaji wa timu ya taifa kutokana na madai ya kushugulikiwa vibaya wakati wakiwa nchini Libya kuelekea mechi ya kufuzu kwa michuano ya Afcon 2025.
Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa shirikisho hilo Ademola Olajire, wachezaji wameamua kwamba hawatacheza tena mechi yao dhidi ya Libya na kwamba mipango ya kuwarejesha nyumbani inaendelea.
Tayari Nigeria imeandikia CAF kulalamikia tuhuma za wachezaji wake kupewa mapokezi mabaya nchini Libya.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria walishikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa Libya kwa zaidi ya saa 15 tangu kutua kwa ndege yao siku ya Jumapili.
Ubalozi wa Nigeria nchini Libya umeripotiwa kushindwa kuingilia kati suala hilo kwa sababu wanahitaji kupata idhini ya kufanya hivyo kutoka kwa serikali ya Libya.

4pm | Kenya vs Cameroon
5pm | Gambia vs Madagascar
7pm | Liberia vs Equatorial Guinea
7pm | Togo vs Algeria
10pm | Eswatini vs Mozambique

Nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria William Troost-Ekong amethibitisha kwamba hawatacheza mechi hiyo na kwamba hawatakubali usafiri wa basi wa saa tatu kutoka katika eneo la Al-Abraq hadi Benina, eneo ambapo mechi hiyo ilikuwa imeratibiwa kuchezwa siku ya Jumanne kutokana na masuala ya kiusalama.
Siku ya Ijumaa, Nigeria ilipata ushindi wa bao moja bila ya jibu dhidi ya Libya kusini mwa mji wa Uyo nchini Nigeria.
Wanaoongoza kundi D wakiwa na alama saba baada ya kucheza mechi tatu wakati Libya wakiwa wa mwisho na alama moja.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.